Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  12 Jumada II 1441 Na: 1441 H / 009
M.  Jumanne, 07 Januari 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ukumbusho wa Ukombozi wa Konstantinopoli

Uzinduzi wa Kampeni kwa Anwani “Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia…inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!”
(Imetafsiriwa)

Konstantinopoli... mji maarufu kwa kuta zake ambazo ulikuwa umepandwa ndani ya akili za Waislamu.

Kuzishinda kuta zake lilizingatiwa kuwa ni lengo kubwa na zawadi kubwa ingelipewa wale tu wanaostahiki sifa za mitume.

Mji huo ambao uliingia katika kumbukumbu siku ulipofunguliwa alfajiri mnamo 12 Jumada al-Awwal 857 H, ukurasa unaovutia katika historia ya Ummah wa Kiislamu. Ukurasa ambao umekuwa kumbukumbu inayostahiki kutathminiwa kila Ummah unapokabiliwa na matatizo makubwa.

Na kwa nini isiwe hivyo? Ilhali ni ukurasa wa historia inayotoka kwa Ummah wa Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) aliousifu na kutia umuhimu kwake na kuuchagua kutoka katika mifano na mafunzo ya kuchukulia kwa ajili yetu, kutoka katika historia yetu na mustakbali wetu ili tuweze kuurudia wakati muhimu. Amesema (saw): «لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ فَلَنِعْمَ الْأَمِيرُ أَمِيرُهَا وَلَنِعْمَ الْجَيْشُ ذَلِكَ الْجَيْشُ»Mutaifungua Konstantinopoli, Amiri wake ni Amiri bora, na jeshi bora ni jeshi hilo!

Kwa sababu hii, na katika kipindi hichi kigumu ambapo Ummah wa Kiislamu unapitia, tumechagua kuzindua kampeni hii kuhusiana na ukumbusho wa ufunguzi wa Konstantinopoli ili kuweza kuwatizama kwa kina “wanaume na hali zao” za tukio hilo lenye baraka, ili tuweze kupata mafunzo na kupata mwangaza katika njia ya Ummah leo. 

Ama kuhusu wanaume... lengo lilikuwa ni kutimiza bishara ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) ya ufunguzi wa mji wa Heraclius kwani lilikuwa ndio lengo lao msingi kwa kizazi chao. Amiri Muhammad al-Fatih na babake Sultan Murad II na walimu wake wawili, mwanasheria Ahmad bin Ismail (Saeed) al-Kurani na Sheikh Akshamsaddin na pamoja nao jeshi la Waislamu katika sehemu hiyo ya ardhi za Uislamu, walifahamu kwamba suala nyeti wakati wao lilikuwa ni ufunguzi wa Konstantinopoli, na ni lazima liwe suala msingi linalowashughulisha na hawakutakiwa kuliwacha kattu na kufuata jingine, na kwamba masuala yote yako chini ya suala hilo. Kwa nini wasiwe na utambuzi huo ilhali wameisoma Hadith ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) inayosema kwamba:«لَتُفْتَحَنَّ الْقُسْطَنْطِينِيَّةُ...» Mutaifungua Konstantinopoli...”

Hivyo basi ilikuwa kwao wao ni amrisho la Mtume (saw) na mama wa masuala yote ambapo nafsi zao walitakiwa kuzitoa muhanga kwa ajili yake.

Muhammad al-Fatih, aliyekuwa na miaka 21 pamoja na jeshi lake la wapiganaji na wajuzi, walijitolea juhudi zao kubwa kupatiliza uwezo waliopewa na Mwenyezi Mungu (swt) aliowaruhusu Waislamu. Walizisoma na kuzitafiti njia na mipango mpaka Mwenyezi Mungu (swt) akawaongoza katika njia iliyokuwa bora na yenye kufana. Mwenyezi Mungu alifungua njia kwa ajili yao, kwa kile ambacho Hakumpa yeyote kabla yao katika Ummah. Walitengeza mizinga mikubwa katika zama zao! Na kuzisukuma meli za baharini kupitia ardhini! Na wakajenga makasri ndani ya ardhi za adui wao kwa kasi mno. Wakamshangaza adui wao kutokana na kuzibadilisha midani za vita katika vitendo vyao vote na uangalifu wao.

Ama kuhusu hali zao, Sultan Muhammad al-Fatih alikuwa na dola ya Kiislamu iliyopangilia uongozi na nguvu za Ummah kupitia asasi zake, kwa hiyo aliweza kupata nguvu, tajriba na uwezo mkubwa na kuzitumia katika kufikia malengo ya kufikia lengo lake.

Na dola hii ilikuwa na kila sifa za dola iliyokuwa inamridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw). Ubwana ndani yake ulikuwa ni Shari’ah na hukm zilikuwa ni za Mwenyezi Mungu (swt) katika uendeshaji wa mambo ya Ummah, na wala dola ya Baizantino na sheria zake hazikuwa na usemi ndani ya mambo ya utungaji sheria ndani ya nchi za Waislamu.

Sultan ilikuwa huru kutokamana na uingiliaji kati wa nje, kwa maana vikosi vya jeshi na usalama vilikuwa vinalinda ardhi yake na utiifu wake ulikuwa ni kwa Ummah wa Kiislamu, na hakuna nchi ya kigeni ilikuwa na ushawishi juu ya safu za vikosi vya kijeshi na usalama vya Kiislamu.

Msingi wa kisiasa ulikuwa umekitwa katika Uislamu na utiifu wake ulikuwa ni kwa Uislamu na Waislamu na haukuchukua chochote kutoka kwa hadhara nyingine isipokuwa hadhara ya Kiislamu, na haukuchukua kutoka kwa nchi za kigeni chochote isipokuwa kinachoruhusiwa na Uislamu kutokamana na ufundi kama vile teknolojia ya silaha.

Uchumi wa nchi ulikuwa uko katika msingi wa nguvu zake, sarafu yake ilikuwa dhahabu na fedha na uchumi wake haukuhusishwa au haukutegemea nchi yoyote ya kigeni.

Suala msingi la Ummah katika zama hizi

Leo, juhudi, ari, ujuzi, nguvu, uwezo, rasilimali na utayari wa kujitolea muhanga, yote yapo miongoni mwa vijana wa Ummah wa Kiislamu, lakini wametapakaa na hawajaungana, kinyume chake wengi wao wanatumiwa vibaya na kuunganishwa kwa yasiyokuwa maslahi ya Waislamu. Sababu ya kutokea haya ni kukosekana kwa dola ya Kiislamu inayotawala kwa Uislamu na kulinda maslahi ya Ummah wa Kiislamu.

Kwa sababu ya yote haya, suala msingi la Ummah wa Kiislamu katika zama hizi limekuwa ni suala la kurudisha dola ya Kiislamu, Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume.

Kutokana na hilo, tunatangaza, kwa jina la Mwenyezi Mungu, na kwa baraka Zake, uzinduzi wa kampeni ya habari ya kiulimwengu kwa anwani, Ukombozi wa Konstantinopoli Bishara Njema Ikatimia... inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!

Tukikumbuka pamoja na Ummah wa Kiislamu ukumbusho mkubwa na kuwakumbusha lile ambalo ni kubwa zaidi, kutimiza bishara ya Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa kusimamisha Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

 Mha. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu