Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  28 Rajab 1445 Na: 1445 H / 023
M.  Ijumaa, 09 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tarehe 28 Rajab Mwaka huu ni Ukumbusho Mkubwa kuliko Miaka Yote Iliyopita kwamba Kuregea kwa Khilafah ni Hitajio la Haraka
(Imetafsiriwa)

Kumbukumbu ya kuanguka kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab inakuja mwaka huu ikiwa na athari zaidi ya kukumbukwa kuliko miaka iliyotangulia. Inakuja na jeraha la Palestina linalotiririka damu nyingi zaidi kuliko hapo awali, na kutukumbusha kwamba suala la kupotea kwa Palestina lilikuwa na bado lina uhusiano wa karibu na kuanguka kwa Khilafah. Tangu ilipovunjwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab mwaka 1342 H, tangu siku hiyo Palestina imekuwa chini ya ukaliwaji kimabavu wa moja kwa moja wa kikoloni, na hakuna aliyeikomboa kutoka katika nchi zilizoundwa na Sykes na Picot.

Kwa hakika, vita vya Gaza mwaka huu vinanyooshea kidole chake kwa Umma wa Kiislamu, na kuuliza, “Kwa nini humkutunusuru?!”, na Umma wa Kiislamu unajitazama, unashangaa na kuuliza, “Kwa nini hatukuweza kuwanusuru?” Jibu ni kwamba Umma wa Kiislamu hauko huru, bali ni mfungwa wa Sykes-Picot (makubaliano ya mipaka). Uhalisia wa nchi za Kiislamu ni kwamba ni jela kwa watu wao. Ni uhalisia ambao hauwezi kukwepwa, na yeyote anayevuka huingia kwenye mzunguko mchafu ambao hujilisha wenyewe. Mfungwa hawezi kumwachilia huru mfungwa mwingine.

Vita vya Gaza hivi leo ni ushahidi wenye nguvu zaidi kwamba Khilafah ni hitajio la haraka kwa Umma wa Kiislamu, kwani ina uwezo wa kukusanya majeshi ya Waislamu na kuyapeleka mahali yanapopaswa kuwepo. Haijuzu kwake kushindwa kuwanusuru Waislamu. Achilia mbali kwamba ardhi iliyobarikiwa ya Palestina daima imekuwa ikipata ushindi kutoka kwa Waislamu wote. Tangu utume wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), nyoyo za Waislamu zimeitamani ardhi hii iliyobarikiwa, kwani ni kibla cha kwanza kati ya vibla viwili, ardhi ya Safari ya Usiku na Kupaa mbinguni, ardhi ya Rabat, ardhi ya Ufufuo, uwanja wa vita wa mujahidina, na rekodi bora ya ushindi wa Uislamu.

Kwa hiyo, hivi sasa, wakati wa matatizo, na kwa kumbukumbu hii, kumbukumbu ya kuvunjwa kwa Khilafah, tunauomba Umma wa Kiislamu ufanye kazi ya kusimamisha Khilafah, tukikumbuka ukweli ulio wazi kwamba Palestina ilipeanwa kwa Wazayuni wakati Khilafah ilipovunjwa, na haitaregea isipokuwa kwa kurudi Khilafah. Hii inatosha (sababu) kwa Umma wa Kiislamu kufanya kazi kwa umakini na kwa makusudi ya kuiregesha.

Kwa Watu Wenye Nguvu na Ulinzi, tunasema:

Enyi Wanajeshi katika Majeshi ya Kiislamu, Umma unakuiteni, basi uungwana wenu uko wapi?! Umekupeni watoto wao kama askari kuwatumia, na ukakununulieni silaha kwa fedha zake, na leo unapiga kelele kwa kinywa kipana: “Mko wapi, enyi majeshi ya Waislamu?” Je, mtaunusuru kwa wema na utiifu kwa Dini yenu?

Enyi Askari katika Majeshi ya Kiislamu, msingoje amri za kuhamasishwa jeshi zitoke kwa watawala, kwani wamejiingiza ndani ya nyoyo zao usaliti mpaka wakawa ni tafsiri ya uhaini. Msingojee idhini ya Magharibi, kwani inataka kuwaweka ndani ya kambi, ili msisonge isipokuwa inapotaka kuwatumia kuua familia zenu na kuvunja nyumba zenu wenyewe. Bali mtegemeeni Mwenyezi Mungu (swt) pekee, ambaye amewatia nguvu askari Wake, na juu ya Ummah wa Kiislamu ambao umekuwa na bado unakuungeni mkono kwa pesa na uhai.

Kwa vyombo vya habari, wanamaoni, na wale walio na mimbari, kalamu, na majukwaa... Je, bado mungali hamjaelewa?!

Ni kweli mbili zisizoweza kuepukika: Palestina ilipotea wakati Khilafah ilipopotea, na mipaka ya Sykes-Picot ni gereza kubwa lililoundwa kuwafunga Waislamu ... Kwa hiyo, haijalishi munajaribu sana kiasi gani, haijalishi munatafuta kiasi gani, na haijalishi munajaribu kiasi gani, kweli hizi mbili ni minyororo miwili inayoufunga Ummah wa Kiislamu ardhini na kuzuia mwamko wake. Minyororo hii miwili iliundwa katika korido za mkoloni Kafiri Magharibi, na kwa hiyo munaona kwamba nchi za Magharibi zina nia kubwa ya kuhifadhi mambo haya mawili. Wanasiasa wa Kimagharibi na vyombo vyao vya habari vinakataza kuwasilisha Khilafah kama mfumo wa kisiasa na wanachuki kali na misingi yake, kama vile Sharia, jihad, na maisha ya Kiislamu. Nchi za Magharibi pia zimejiandaa kuwatambua watawala na serikali fisadi zaidi katika nchi za Kiislamu, na kupuuza jinai zao na hata kuwalinda dhidi ya uwajibikaji, mradi tu wahifadhi mipaka ya Sykes-Picot na kazi yake ya kijiografia; ambayo ni kuzikoloni na kuzigawanya nchi za Kiislamu. Kwa hiyo, muna kazi kubwa, ambayo ni kunyanyua ufahamu wa rai jumla katika Umma wa Kiislamu na kurekebisha dira yake kuelekea kufanya kazi ya kuiregesha Khilafah kwa kuwataka watu wa Nusra (msaada wa kimada) wachukue hatua, waondoe nchi kutoka kwa Sykes-Picot, na kusimamisha Khilafah. Kwa hivyo fanyeni hisa yenu na muwakumbushe watu kwamba ardhi iliyobarikiwa ya Palestina ilipotea wakati Khilafah ilipopotea, na kwamba makubaliano ya Sykes-Picot ni gereza kubwa lililoundwa kuwafunga Waislamu.

Kwa Ummah mzima wa Kiislamu:

Enyi Waislamu, hapana shaka kwamba damu inachemka katika mishipa yenu mnapotazama kuuawa kwa watu wa Gaza na kutelekezwa kwao na watawala. Hili ni makusudi, kwani wanataka kukufanyeni mujisikie wanyonge ili mufikiri hakuna suluhisho. Lakini ukweli ni kwamba suluhisho lipo, na linaanza na wito wenu mliouita wakati huu, ambao ni, “Mko wapi enyi majeshi ya Waislamu?!”, “Tufungulieni mipaka!”. Kwa hakika, suluhisho linaanza kwa majeshi ya Kiislamu kusonga, kuwaondoa watawala wasaliti, na kurudisha pigo la pili kwa umbile la Kiyahudi baada ya kupata pigo la kwanza kutoka kwa watu wa Gaza. Hatua hiyo inaweza tu kufanikiwa kwa kuvunja milango ya jela la Sykes-Picot na kufuta mipaka baina ya nchi za Kiislamu ili wote waende kuinusuru ardhi iliyobarikiwa ya Palestina, na hili ni jambo ambalo majeshi pekee katika nchi za Kiislamu yanaweza kufanya, kwa sababu wao ndio watu wenye nguvu na ulinzi. Hao ndio watu halisi wa Nusrah.

Kwa hakika, kusimamisha Khilafah ni hitajio la dharura kwa Umma wa Kiislamu, linaweza kufikiwa tu na majeshi ya Kiislamu, kwani wao wana uwezo wa kuinusuru Gaza na pia wana uwezo wa kusimamisha Khilafah. Kwa hiyo, fanyeni haraka kwa ajili ya kazi nzito mara moja ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55].

Mhandisi Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu