Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  18 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 040
M.  Jumatatu, 21 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkataba wa Ummah Unatokana na Itikadi yake Safi, hautoki kwa Demokrasia Batili!
(Imetafsiriwa)

Chini ya mada “Enzi ya Kidemokrasia katika Ulimwengu wa Kiarabu: Ramani ya Mkakati wa Demokrasia,” kundi la wale wanaojiita wasomi wa Kiarabu wanafanya mkutano wa kutia shaka huko Sarajevo, ambapo wanajadili kile wanachoelezea kuwa ni suluhisho la kivitendo kwa migogoro ya udhalimu, ukandamizaji na kukosekana kwa uadilifu wa kijamii, na wanachunguza changamoto za kifikra na kisiasa zinazoletwa na vita dhidi ya Gaza. [Al Jazeera, 19/10/2024]

Wapendwa Mabwana Wenye Elimu: Methali ya kale ya Kiarabu inasema, “Anayejaribu kile kilichojaribiwa atajuta,” na tunasema kwamba umefika wakati wa watu wenye akili kutumia kanuni jumla ya, “Kilichojaribiwa kisijaribiwe.” Tunasema haya kwanza kwa mratibu wa mkutano huu, Rais wa zamani wa Tunisia Moncef Marzouki, ambaye aliijaribu demokrasia moja kwa moja wakati wa urais wake wa Tunisia baada ya Mapinduzi ya Jasmine mwaka 2011 na masaibu yaliyofuata nchini Tunisia, ambayo yalisababisha kuchaguliwa kwa rais wa sasa, Kais Saied, katika uchaguzi wa kidemokrasia. Tunamwomba ajibu kwa uaminifu: Je, demokrasia imeboresha hali ya nchi au imeifanya kuwa mbaya zaidi na kuzidi kushushwa hadhi? Hivi ndivyo ilivyo katika nchi za Misri, Yemen, Syria, Iraq, Jakarta, Malaysia, Jordan, na kwengineko...

Labda Marzouki na wasomi wenzake watasema kuwa hawakutekeleza demokrasia ya halisi, na hawakupata fursa ya kuitumia na kuhukumu kushindwa au kufaulu kwake. Hapa tunawakumbusha watu hawa wanaoshuhudia jinai zinazofanywa na umbile la “kidemokrasia” la Kiyahudi huko Gaza na Lebanon, kwamba ndilo umbile ambalo nchi za Magharibi zinajivunia kuwa demokrasia pekee katika Mashariki ya Kati. Kwa hivyo, demokrasia hii imeleta nini zaidi ya misukosuko, uharibifu na kifo?

Je, wasomi hawa hawajashuhudia, na imedhihirika kwa kila mtu mwenye akili timamu, dosari na ubatili wa tawala zinazotawala na mashirika ya kimataifa ambayo yameibuka kutoka kwao, na je, haijawabainikia wote kwamba nchi hizi za kidemokrasia hazijali lolote zaidi ya kupigana na watu wanaotafuta ukombozi kutokana na dhulma na ukoloni, na hasa Waislamu?

Wasomi waliokusanyika katika kongamano hili lenye kutia shaka wanadai kuwa suluhu ni “kuondokana na dhana potofu za siku za nyuma, na kuendelea kufikiria kuhusu suluhu za kweli zinazokidhi matarajio ya watu kwa ajili ya demokrasia, haki na ukombozi wa taifa.” Hatuna budi kuuliza hapa: Ni nani aliyekuteueni na kukuwakilisheni kuzungumza kwa niaba ya watu na kuwapotosha kwa kusema kwamba wanatamani demokrasia?! Watu hawa ni Waislamu ambao wamebeba itikadi safi (Aqidah) ambayo ndani yake unachipuza mfumo kamili na mpana wa maisha ambao Mwenyezi Mungu aliuteremsha kuwa ni rehma kwa walimwengu na uongofu kwa watu wote, na sio dhana potofu za udanganyifu wa kidemokrasia ambao ulimwengu umeushuhudia na kushindwa kwao na uovu na ufisadi waliouleta katika kipindi cha karne moja ambapo wametawala na kuihukumu dunia kwa sheria zilizotungwa na mwanadamu ambazo zimeeneza wasiwasi na hofu kote duniani, zikazusha vita, watu waliokimbia makaazi yao na watu wenye njaa ili waweze kufurahia neema za ardhi kwa gharama ya wanyonge?! Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللهِ حُكْماً لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ]

“Je, wao wanataka hukumu za Kijahiliya? Na nani aliye mwema zaidi katika kuhukumu kuliko Mwenyezi Mungu kwa watu wenye yakini?” [Al-Ma'idah 5:50]

Enyi mabwana, tunavuta mazingatio yenu kwenye ukweli kwamba biashara yenu katika kujitolea muhanga kwa Umma wa Kiislamu, iwe Palestina au kwengineko, haikustahiki nyinyi kuzungumza kwa niaba ya watu hawa, kwa sababu mumeitenganisha Dini na Aqidah yao na mambo yao ya maisha kwa kutabanni demokrasia na kuukataa Uislamu nyuma ya migongo yenu. Na fahamuni kwamba Mujahidina hawa wa Gaza hawahitaji mikufu ya uongo chini ya kauli mbiu isemayo: “Mtu bora wa Mwaka kwa Demokrasia na Kuishi pamoja”! Wamejitolea maisha yao ili neno la Mwenyezi Mungu liwe tukufu, sio kwa ajili ya demokrasia ya chuki ambayo vita hivi vya uharibifu huko Gaza vimedhihirisha kwa ulimwengu wote ushirikiano wa wanademokrasia na njama za tawala zao dhidi ya Waislamu na msimamo wao na Mayahudi katika uvamizi na dhulma yao.

Wapenzi wasomi: Mnajionea wenyewe upotoshaji wa watu, kama mnavyokiri, kama Marzouki mwenyewe alivyosema: “Ushirikiano wa tawala za Magharibi katika mauaji haya ya halaiki umechangia kupoteza zaidi imani miongoni mwa Waarabu juu ya demokrasia ambayo wamekuja kuiona kama fikra ya Kimagharibi ambayo imepoteza aaminifu wote,” na kama vile Tawakkol Karman alivyoeleza: “Udhaifu wa tawala hizo za Magharibi umefichuliwa na kuongezeka kwa mawimbi ya chuki, ubaguzi wa rangi, na uadui dhidi ya wakimbizi, na pia wameshindwa katika mtihani wa uhuru walipowakandamiza na kuwafunga wanafunzi wanaounga mkono Gaza na Palestina.” Huu unatosha kuwa ni ushahidi wa upotofu wenu, ushahidi wa kujitenga kwenu na Umma wa Kiislamu, na mfichuaji wa udanganyifu wenu.

Mnazungumzia demokrasia gani?! Na mnataka kutabikisha demokrasia gani?!

Demokrasia kwa ufupi ni mfumo wa ukafiri na hauna uhusiano wowote na Uislamu, na yeyote anayeilingania au kutaka utabikishwaji wake ni wa kutiliwa shaka na mpotoshaji, kwa sababu Ummah unatamani kurudisha heshima na fahari yake kupitia Uislamu na ushindi wa Mwenyezi Mungu tunapomnusuru Yeye na Dini Yake kwa kuregea kwenye umoja wetu katika mfumo wa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ndio maana tunakuombeni muregee kwenye fahamu zenu kwa kuutabanni Uislamu na mfumo wake, kwani hiyo ni haki na chochote kisichokuwa huo ni batili.

[المر تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ وَالَّذِيَ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ الْحَقُّ وَلَـكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لاَ يُؤْمِنُونَ]

“Alif Lam Mym Ra. (A.L.M.R.) Hizi ni Ishara za Kitabu. Na uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ni Haki. Lakini wengi wa watu hawaamini.” [Ar-Ra'd 13:1]

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu