Jumanne, 08 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 042
M.  Ijumaa, 01 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ushenzi ni Ufaransa na Historia yake ni Mbaya na Nyeusi, Ewe Macron
(Imetafsiriwa)

Utovu wa nidhamu wa Rais wa Ufaransa Macron umefikia kilele chake kwa kauli zake za kishenzi alizozitoa katika Bunge la Morocco mnamo siku ya Jumanne, 29/10/2024; kuwakashifu Mujahidina nchini Palestina, wanaotetea ardhi na haki zao, kama “washenzi”, na kudai kwamba umbile, halifu vamizi la Kiyahudi lina haki ya kujilinda.

Ama kuhusu Mfalme wa Morocco, hakunyosha hata kidole kwenye kauli za dharau za mgeni wake. Lau angekuwa na chembe ya uanaume wa Kiarabu na ari ya Uislamu, angemueka kizuizini hadi aondoe kauli zake za kishenzi na kuomba msamaha kwa kuzisema. Juu ya uovu wake, alivielekeza vikosi vya usalama kuwavamia waandamanaji waheshimiwa waliopinga dhidi ya kauli za mgeni huyo mkorofi!

Ama kuhusu wajumbe wa bunge la Morocco japokuwa wengi wao walipinga baadaye na kukemea kauli za Macron, ingekuwa bora wangemjibu moja kwa moja baada ya kusikia kauli zake, na kumzuia asiendelee na uchafu wake, au watoke nje ya ukumbi na wamwache akibweka peke yake.

Tunapongeza misimamo ya watu waheshimiwa wa Morocco, ambao hawakukaa kimya kuhusu kauli hizi za jeuri, na walionyesha kuzikataa kwao kwa njia mbalimbali. Wengi wao hata walitoka kuonyesha kutoridhishwa kwao nazo na kupita kwao bila jibu kutoka kwa serikali shiriki ya Morocco.

Ama kuhusu Macron, lazima tusimame kidogo ili kumkumbusha historia ya kishenzi ya nchi yake, na kuteka hisia za rai jumla ya ulimwengu kwa baadhi ya uhalifu wa kishenzi wa Ufaransa katika historia, ili kila mtu aweze kuona ni nani mshenzi:

1- Ufaransa ilikuwa na nafasi kubwa katika Vita vya Msalaba ambavyo ilivianzisha dhidi ya nchi za Waislamu katika Zama za Kati, kwa kutekeleza jinai mbaya zaidi dhidi ya Waislamu na dhidi ya wanadamu, hivyo mshenzi ni nani?!

2- Wakati wa uvamizi wa Ufaransa wa Misri 1798-1801 M, ilifanya jinai mbaya zaidi dhidi ya watu wa Misri, na kuharibu mji wa Alexandria juu ya vichwa vya watu wake. Katika mapinduzi ya pili ya watu wa Misri dhidi yake, Kleber aliharibu vitongoji vya Cairo kwa mizinga, akaua idadi kubwa ya wanamapinduzi, akazuia chakula kutoka kwa wakaazi wa mji huo, na akaamuru kuchinjwa kwa wafungwa na kutupa miili yao kwenye Mto Nile wakati wa usiku, pamoja na kuwabaka wanawake. Jumla ya Wamisri waliouawa na Ufaransa ilizidi elfu hamsini, hivi mshenzi ni nani?!

3- Ama kuhusu jinai za Ufaransa dhidi ya watu wa Algeria wakati wa kuikalia kwa mabavu kuanzia mwaka 1830 hadi 1962, mijeledi ya vitabu haitosha kuzitaja, ikiwa ni pamoja na kuuchoma kwao mji wa Laghouat mwaka 1852 na kuteketeza zaidi ya theluthi mbili ya wakaazi wake 4,500 kwa usiku mmoja. Baada ya kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, wakati watu wa Algeria walipoasi dhidi yake, iliua zaidi ya watu 45,000 na kushambulia kwa mabomu vijiji 44. Mnamo 1955, Wafaransa walikusanya Waalgeria 1,500 katika uwanja wa michezo wa mji, kisha wakawaua na kuwazika kwenye mitaro kwa wingi. Mnamo 1957, waliyeyusha miili ya nembo za upinzani kwa mafuta yanayochemka wakiwa hai, pamoja na kubomoa misikiti, kuteketeza Quran na kuwaua waumini. Kwa hiyo, mshenzi ni nani?!

4- Mnamo mwaka 1899 M, katika moja ya miji ya Mali, kamanda wa Ufaransa aliwakusanya kina mama wote na watoto wachanga na akaamuru wauawe kwa kuwachoma mikuki. Kisha jeshi la Ufaransa likapora pesa, mifugo, na farasi. Hivi, mshenzi ni nani?!

5- Waislamu kwa jumla na hasa wananchi wa Morocco hawasahau jinai iliyofanywa na Ufaransa mwaka 1907 mjini Casablanca ilipoiangamiza kabisa kwa kujibu mapinduzi dhidi yake, katika kile kinachojulikana kama Mauaji ya Casablanca. Sasa, mshenzi ni nani?!

6- Majeshi ya Ufaransa yalifanya uhalifu wa kutisha nchini Chad mnamo Novemba 1917, walipowaalika wanazuoni na wasomi kukutana nao ili kufikia njia ya pamoja ya kuelewa na kusimamia mambo ya nchi. Wanazuoni na mashekhe wa nchi hiyo waliitikia mwaliko huu, lakini majeshi ya Ufaransa yaliwasaliti kwa njia mbaya zaidi, yaliwashambulia kwa mapanga; karibu wanazuoni 400 bora zaidi wa Chad waliuawa. Kwa hiyo, mshenzi ni nani?!

7- Ama kuhusu jinai zake nchini Syria wakati wa kuikalia kwa mabavu kuanzia mwaka 1920 hadi 1946, ni nyingi. Ilishambulia kwa mabomu vitongoji na nyumba juu ya vichwa vya wamiliki wake, kuwakata vichwa na kuwaua wanamapinduzi, kuwabaka wanawake, na wakaazi waliohama kutoka vijiji na miji. Hivyo, mshenzi ni nani?!

8- Mnamo 1947, vikosi vya Ufaransa vilifanya mauaji dhidi ya watu wasio na hatia nchini Madagascar. Hivi, mshenzi ni nani?!

9- Tusisahau jinai zake katika nchi za Burundi, Bosnia na Herzegovina, na kuibadilisha kwake Guyana barani Amerika Kusini kuwa uhamisho kwa wapinzani na kambi ya mateso, na uhalifu mwingine wa kinyama ambao hauhesabiki. Kwa hiyo, mshenzi ni nani?!

10- Ufaransa ndio nchi pekee duniani ambayo mji mkuu wake unajumuisha kile kinachoitwa “Makavazi ya Binadamu”, ambayo yana mafuvu 18,000 ya wanamapinduzi wa Kiislamu ambao vichwa vyao vilikatwa, na mafuvu yao yakahifadhiwa katika makavazi hayo. Sasa, mshenzi ni nani?!

Hii ndio sura yenu halisi ya kuchukiza, na historia yenu nyeusi, mbaya, Ewe Macron. Nyinyi mliounda hadhara yenu juu ya maiti za wasio na hatia, na mafuvu ya wazee, watoto na wanawake, na mliopora mali za watu huko nyuma. Bado nyinyi mnaishi kwa kupora mali zao, halafu mnafika katika ardhi za Uislamu kuwatuhumu wamiliki wa ardhi wanaoihami ardhi yao kwa unyama, wallahi, hii ni moja ya dhambi kubwa!

Jambo baya zaidi ni kwamba hukupata mtawala hata mmoja wa nchi za Waislamu ambaye angekuhutubia kama “mbwa wa Warumi” kama Harun al-Rashid alivyofanya kwa Nicephorus, mfalme wa Ufaransa, ambaye hakuweza kujibu hata kwa neno moja kwa hotuba hiyo, lakini badala yake alijisalimisha na kutii na kulipa Jizya kwa dola ya Kiislamu. Tunakupa habari njema kwamba Khalifa, mtu ambaye atakuhutubia kwa hotuba kama hiyo, anakuja, na kisha Ufaransa italipia gharama ya jinai zake dhidi ya Waislamu, na dhidi ya ubinadamu na wanadamu, na utarudi, ukiwa umefedheheka, kulipa jizya kwa dola ya Khilafah Mwenyezi Mungu akipenda. Labda Khalifa ajaye ataweka fuvu lako pamoja na fuvu la Netanyahu badala ya mafuvu ya Waislamu kwenye makavazi yenu.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu