Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 6 Jumada II 1446 | Na: H 1446 / 063 |
M. Jumapili, 08 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hongera Ash-Sham na Watu wake kwa Kumpindua Mtawala dhalimu na Utawala wake, Sasa ni Mbele Kuelekea Khilafah Rashida
(Imetafsiriwa)
Asubuhi ya leo, Jumapili tarehe 8/12/2024 M, na katika siku ya 12 ya operesheni ya “Kuzuia Uvamizi”, wapiganaji waliweza kuingia katika mji mkuu wa Syria, Damascus, na kupindua utawala wa Bashar al-Assad, ambaye Reuters iliripoti - ikiwanukuu maafisa wa Syria – kwamba aliuacha mji mkuu na kuelekea kusikojulikana. Hivyo, wapiganaji wa upinzani waliweza kuikomboa Idlib, Aleppo, Hama, Homs na Damascus, na kuwaachilia maelfu ya wafungwa waliokuwa wakizuiliwa na utawala wa kihalifu katika vyumba vya chini vya jela zake ovu kwa miaka na miongo kadhaa. Ardhi ya Ash-Sham ilishangilia kwa furaha kutokana na kukombolewa kutoka kwa dhalimu na utawala wake, Takbira zilisikika kwa sauti kubwa katika pembe za Ash-Sham na viunga vyake, na Ummah ukatoka nje katika sherehe zilizojaza viwanja vya nchi hiyo na viwanja vya miji mingi duniani, karibu na mbali, kwa shangwe na furaha, kana kwamba ni Idd, na hivyo ndivyo ipasavyo.
Kuanguka kwa dhalimu Bashar na utawala wake ni ushindi mkubwa kwa wapiganaji, na afueni kubwa kwa Ash-Sham na watu wake, watoto wake, wanawake, wazee na wanaume, ambao utawala huo umewaonjesha mambo machungu zaidi: kufungwa jela, mauaji, kuhama, njaa na ubakaji katika matukio ambayo yalivunja nyoyo, katika kipindi cha zaidi ya miaka 13 ya mapinduzi, na miongo kadhaa kabla, ya utawala wa Bashar na baba yake mhalifu. Hongera Ash-Sham na watu wake kwa ushindi huu mkubwa, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu mwanzo na mwisho. Mwenyezi Mungu (swt) asema;
[قُلِ اللَّهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ بِيَدِكَ الْخَيْرُ إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Sema: Ewe Mwenyezi Mungu uliye miliki ufalme wote! Wewe humpa ufalme umtakaye, na humwondolea ufalme umtakaye, na humtukuza umtakaye, na humuangusha umtakaye. Kheri yote iko mikononi mwako. Hakika Wewe ni Muweza wa kila kitu.” [Al-i-Imran: 26].
Kinachopaswa kutajwa na kuonywa dhidi yake katikati ya furaha ya ushindi ni onyo dhidi ya kuridhika na kile kilichopatikana na kukomea hapo. Kupinduliwa kwa Bashar na utawala wake lazima iwe mwanzo, sio mwisho. Wapiganaji lazima wakamilishe safari ya kuelekea kuikomboa ardhi yote ya Ash-Sham ili kuiunganisha chini ya bendera ya Imam mmoja anayeitangaza kuwa ni Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ili Uislamu utabikishwe kikamilifu bila ya upungufu wowote, na kuifanya iwe ni dola ya Kiislamu yenye vyombo vyake vyote, katiba na maelezo yake yote, sio dola ya kisekula, jamhuri ya Kiislamu au utawala wa kifalme. Vyenginevyo, mihanga mikubwa iliyotolewa na watu wa Ash-Sham na wanamapinduzi wake haitaleta mabadiliko ambayo kwayo walijitokeza na kutamani yatokee.
Kukubali serikali ya kisekula au ya kidemokrasia au kuingia katika mapigano ya ndani ya makundi na kuigawanya nchi katika majimbo na wilaya kunamaanisha kupoteza juhudi zilizofanywa, maisha yaliyopotea, na pesa zilizomalizika, na nchi itabaki katika mikono ya ukoloni wa Marekani na sura yake mpya ambayo itafadhiliwa na Uturuki ya Erdogan. Kinachoitwa dola ya taasisi ni muundo wa mfumo wa kibepari ili kuunadi miongoni mwa wanamapinduzi na wapiganaji walioijaza Ash-Sham kwa nyimbo na wakaandika maneno yake kwa damu yao kwamba ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Hebu wanamapinduzi na wapiganaji na waendelee na njia ya kuelekea kung'oa ukoloni kutoka Ash-Sham bila kuacha kambi, vikosi, watu au vyama, ili Ash-Sham ibaki kwa ajili ya Waislamu tu. Wanapaswa kukata mafungamano yote na zana za Amerika katika eneo hilo: Uturuki, Iran, Iraq na watawala wengine wa Waislamu, ili uamuzi wao uwe uamuzi wa kibinafsi ambao hakuna mtu mwenye mamlaka juu yao, ili juhudi zao zisije kupelekea yale mapinduzi mengine yaliyopelekea, ili Ash-Sham iregee kuwa ni nyumba ya Uislamu, na waumini wafurahie ushindi wa Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[الَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمْ فَإِن كَانَ لَكُمْ فَتْحٌ مِّنَ اللهِ قَالُواْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ وَإِن كَانَ لِلْكَافِرِينَ نَصِيبٌ قَالُواْ أَلَمْ نَسْتَحْوِذْ عَلَيْكُمْ وَنَمْنَعْكُم مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ فَاللهُ يَحْكُمُ بَيْنَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَن يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]
“Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [An-Nisa: 141].
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |