Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  10 Jumada II 1446 Na: H 1446 / 064
M.  Alhamisi, 12 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Matukio ya Uhalifu Yanayofichuliwa Katika Magereza ya Dhalimu wa Ash-Sham Yanapasa Kuwasha Moto Nyoyoni mwa Wana wa Ummah Kuwateketeza Watawala
(Imetafsiriwa)

Katika siku chache zilizopita baada ya kutoroka kwa dhalimu Bashar na kuanguka kwa utawala wake muovu, matukio ya uchungu na makali yalifichuliwa ambayo yalivunja nyoyo za Waislamu. Kwani waliona kwa macho yao ukubwa wa jinai na ukatili ambao utawala wake uliamiliana nao kwa ndugu na dada zao katika vituo vya uzuizi na magereza: kuanzia na kuwekwa kwao kizuizini kwa miongo kadhaa katika magereza ambayo yalikosa mahitaji msingi zaidi ya kibinadamu, kisha njaa, ukandamizaji na mateso ya kikatili ambayo magereza hayo na kuta zinayazungumzia, na seli, nguzo na zana za mateso zinazosimulia hadithi zao, na miili ya wahasiriwa waliopatikana wamekufa na kukatwakatwa inamfichua. Na hadithi zilizosimuliwa na wale walioachiliwa huru kuhusu kiwango cha mauaji yaliyokuwa yakifanyika ndani ya magereza hayo, kuwa ilifikia makumi kila siku katika gereza moja, haswa katika Gereza la Sednaya, pango la ukatili na uhalifu, na hadithi za udhalilishaji, kunyimwa, kuteswa, kudhalilishwa na kubakwa, hadithi ambazo zimechana nyoyo za wasikilizaji kwa hofu kubwa, hadi kila mtu akajiuliza, je, wale waliofanya uhalifu huu wote kwa watu hao dhaifu ni binadamu? Ili kustahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na adhabu chungu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَاناً وَإِثْماً مُّبِيناً]

“Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.” [Al-Ahzab: 58].

Huu sio uhalisia wa utawala wa Al-Assad pekee, bali ni uhalisia wa tawala zote zenye madhara zilizoko katika nchi za Waislamu. Zote zimetenda jinai na zinaendelea kutekeleza jinai dhidi ya Ummah wetu tangu mkoloni kafiri Magharibi alipozilazimisha juu ya shingo zake.

[وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَن يُؤْمِنُوا بِاللهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ]

“…Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa.” [Al-Buruj: 8]

Serikali zinazotawala katika nchi zetu zote ni mifumo ya kipolisi inayojikita katika ukandamizaji, ukatili na dhulma. Zote zina uadui sawa kwa Ummah na matarajio yake ya ukombozi na kutawaliwa na Uislamu. Haziachi jinai yoyote ili kuzuia Ummah usipate tena mamlaka yake na kusimamisha Khilafah yake. Matukio haya ya dhulma na mateso ambayo Waislamu wote wameyaona lazima yawashe ndani ya nyoyo zao moto wa chuki dhidi ya watawala, haupaswi kuzimwa kabla hawajakamata koo zao na kubomoa mifumo yao na kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume; ambayo ndani yake watafurahia maisha ya fahari na utu, na ndani yake khalifa atakuwa na huruma kwao na kuwahakikishia faraja yao.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi.” [Ar-Rum: 4]

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu