Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  7 Jumada II 1446 Na: H 1446 / 064
M.  Jumatatu, 09 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Marekani Yaogopa Kuangamia kwa Tawala za Vibaraka katika Nchi za Waislamu na Kuibuka kwa Khilafah
(Imetafsiriwa)

Marekani haiachi kuonyesha hofu yake ya kuangamia kwa tawala vibaraka katika nchi za Waislamu mara kwa mara. Hofu hii inaonekana kwenye ndimi za viongozi wake; Mshauri wake wa Usalama wa Kitaifa Jake Sullivan anathibitisha kwamba itafanya kazi kuimarisha Jordan, umbile la Kiyahudi (Kizayuni), na Iraq ili mzozo wa Syria usihamia kwao. Siku chache zilizopita, Waziri wake wa Mambo ya Nje Antony Blinken alisisitiza katika hotuba yake kabla ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO juu ya ulazima wa kuzuia kuregea kwa Dola ya Khilafah.

Yeyote anayefuata hali halisi ya nchi za Waislamu anatambua kwamba makaa yangali yapo chini ya majivu. Baada ya watu kuwaasi watawala wao katika kile kiitwacho Mapinduzi ya Kiarabu, na baadhi ya nchi kuwaondoa watawala wao wahalifu, nchi hizo kubwa kwa kushirikiana na vibaraka wao ziliweza kuyadhibiti mapinduzi hayo na kumbadilisha kibaraka mmoja badala ya mwengine. Hali za watu katika nchi hizo hazikubadilika, bali zilizidi kuwa mbaya zaidi kuliko walivyokuwa kabla ya mapinduzi. Hata hivyo, makaa hayo yalibakia chini ya majivu, na watu waliendelea kuitazamia siku watakapoziondoa tawala za vibaraka zilizowatawala bila ya sheria ya Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Khilafah ya kweli ambayo itawatawala kwa Uislamu. Kwa matukio ya hivi karibuni nchini Syria, Amerika haikuweza kuficha hofu yake ya mabadiliko ya kweli katika nchi za Waislamu, ambapo watu wangeinuka dhidi ya watawala wao dhalimu. Bali hofu ilijaa nyoyo za watawala wa Waislamu pia, hivyo mawaziri wa mambo ya nje wa Jordan, Iraq, Misri, Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na Iran walikimbia kukutana jijini Doha na kutangaza kwamba “mzozo wa sasa nchini Syria unawakilisha maendeleo hatari kwa usalama wa kikanda na kimataifa.”

Tunathibitisha kwamba hofu hizi ni za kweli, na kwamba Marekani na nchi kubwa wanalolihofia zaidi ni kuasisiwa Khilafah Rashida. Tunathibitisha kwamba hofu ya madhalimu wanaowatawala Waislamu ni ya kweli, na hivi sasa wanakuna vichwa vyao baada ya kuiona Marekani inawaacha vibaraka wake ambao watu wao waliwaasi, na haikuwanufaisha hata kidogo. Hatimaye, tunathibitisha kwamba Waislamu hawatatulia, na uamuzi wao hautatatuliwa mpaka wawaondoe watawala wao wahalifu, vibaraka, na wasimamishe dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na waondoe athari za wakoloni makafiri katika nchi zao, hilo litatokea hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda, na kesho iko karibu kwa wanaoiona.

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu