Alhamisi, 07 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  23 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 028
M.  Ijumaa, 14 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Maisha Yenu Yanawezaje Kuwa Mazuri Wakati Wanawake Walio Huru Wako Katika Magereza ya Mayahudi, Wakiteswa na Heshima Zao Zikivunjwa?!
(Imetafsiriwa)

Kituo cha Haki za Kibinadamu cha Palestina kilifichua, kulingana na ushuhuda mpya uliokusanywa na mawakili na watafiti wa kituo hicho kutoka kwa wafungwa kadhaa walioachiliwa huru kutoka Ukanda wa Gaza kutoka magereza na vituo vya uzuizi vya umbile la Kiyahudi, utaratibu na mpangilio wa mateso ya kingono, ikiwemo ubakaji, kuvua nguo, kulazimishwa kurekodi filamu, na unyanyasaji wa kingono kwa kutumia zana na mbwa, pamoja na udhalilishaji wa kisaikolojia wa makusudi unaolenga kuponda utu wa binadamu na kufuta kabisa kitambulisho cha mtu binafsi. Kituo hicho kinathibitisha kwamba kile kilichosemwa katika ushuhuda huu hakiwakilishi matukio maalum ya kibinafsi ya pekee, bali kinaangukia ndani ya sera ya kiserikali inayotekelezwa katika muktadha wa uhalifu unaoendelea wa mauaji ya halaiki dhidi ya wakaazi wa Ukanda wa Gaza, ambao ni zaidi ya watu milioni mbili, miongoni mwao maelfu ya wafungwa waliofungwa katika magereza na kambi zilizofungwa kutokana na ufuatiliaji wa kimataifa, ikiwemo Kamati ya Kimataifa ya shirika la Msalaba Mwekundu.

Ripoti hiyo ilirekodi ushuhuda wa kutisha unaohusiana na visa vya ubakaji vilivyofanywa na vikosi vya uvamizi dhidi ya Wapalestina, wakiwemo wanawake waliokamatwa kutoka maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Miongoni mwa visa vilivyonakiliwa katika ripoti hiyo ni ubakaji wa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 42 ambaye alikamatwa alipokuwa akipita katika moja ya vituo vya ukaguzi vilivyowekwa kaskazini mwa Gaza mnamo Novemba 2024. Katika ushuhuda wake kwa timu ya kituo hicho, alizungumzia kufanyiwa aina nyingi za mateso na unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na kubakwa mara nne na wanajeshi Kiyahudi, pamoja na kutukanwa mara kwa mara kwa lugha chafu, kuvuliwa nguo na kurekodiwa uchi, kupigwa shoti ya umeme, na kupigwa sehemu zote za mwili wake.

Ushuhuda wa kushangaza na wenye uchungu mkubwa ulisimuliwa na wafungwa walioachiliwa huru, hasa kile kilichosimuliwa na mfungwa huyo mwanamke ambaye ushuhuda wake ulionekana katika ripoti hiyo. Wanaume na wanawake wanakamatwa, kuteswa, na heshima na hadhi yao inakiukwa bila sababu yoyote isipokuwa kwamba wanatoka Ukanda wa Gaza, ambao unafanyiwa mauaji ya halaiki na adhabu ya pamoja ambayo sura zao zinaendelea hadi sasa. Ushuhuda huu unaonyesha ukatili, uhalifu, udhalimu, na upotovu wa umbile la Kiyahudi na wanajeshi wake, ambao walikuwa wakijinadi kwa ulimwengu kama “jeshi lenye maadili mema zaidi,” huku wanajeshi wake na Ben Gvir wakijigamba walichofanya na kuhusu mateso wanayopata wafungwa na wafungwa wanawake katika magereza ya Mayahudi, hasa kambi ya Sde Teiman ambako watu wa Gaza

Umbile hili limepita kiasi katika uhalifu na ukatili wake lilipoona usaliti, kimya, na hata ushirikiano wa watawala wa Waislamu dhidi ya watu wa ardhi iliyobarikiwa na hasa watu wa Gaza. Watawala hawa wasaliti, pamoja na mfumo wa kihalifu na kinafiki wa kimataifa unaoongozwa na Amerika, walifanya juhudi kubwa kuwaachilia huru wafungwa wa Kiyahudi waliokuwa wakizuiliwa Gaza, na hata kukimbilia kutafuta miili ya wale waliokufa miongoni mwao na kuitoa chini ya kifusi, bila kupepesa kope au kusema neno hata moja, achilia mbali kujitahidi kuwasaidia wafungwa na wafungwa wanawake katika magereza ya Mayahudi, na bila kujali kuwatoa maelfu ya mashahidi waliokuwa bado chini ya kifusi.

Umbile hili halifu linasubutu kufanya uhalifu wake na kukiuka heshima ya wanawake huru lilipoona Ummah na majeshi yake kimya kuhusu yale linayowatendea ndugu na dada zao huko Al-Quds, Ukingo wa Magharibi, na Gaza, wakiwatelekeza na kuwaacha kuwa mawindo rahisi mbele yake; na lilipowaona kuwa kimya kuhusu watawala wao wahalifu wasaliti wanaolipa umbile hilo halifu njia za uhai, wakililinda, wakifunga mipaka, na kukuzuieni kuwanusuru.

Enyi Waislamu: Sentensi moja tu kutoka kwa mwanamke mzee mwenye huzuni kuhusu kukamatwa kwa mwanawe “Ee Mansur, watu wote wanafurahi isipokuwa mimi” ilimfanya Al-Hajib Al-Mansur arudi nyuma na jeshi lake na kuwataka wasishuke kutoka kwenye farasi wake, na akaandamana nao ili kumwachilia huru mwanawe na mateka wengine kutoka kwenye ngome walimokuwa wamezuiliwa. Na ulinzi wa wanawake Waislamu na kuhifadhi heshima yao ulimfanya Qutaybah ibn Muslim kukataa fidia, akiamuru kuuawa kwa yeyote anayewashambulia Waislamu, na kusema maneno yake maarufu, “Wallahi, mwanamke Muislamu hataogopa kamwe kwa sababu yenu.” Na kilio cha “Wa Mu'tasimah!” Kutoka kwa mwanamke Muislamu kilitosha kwa Al-Mu‘tasim kukusanya jeshi kubwa ili kumwachilia huru. Na kilio cha wanawake huru kilimfanya Muhammad ibn Al-Qasim kutikisa kiti cha enzi cha mfalme wa Sind kwa sababu aliizuia meli ya wanawake Waislamu na kuwachukua mateka. Na kabla ya yote hayo, kufunuliwa kwa uchi wa mwanamke Muislamu kulimfanya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) awafukuze Banu Qaynuqa‘ kutoka Madina. Je, Ummah na majeshi yake wamenyimwa wanaume, mashujaa wanaolinda dini yao na wanawake wao huru?! Muna nini, enyi Waislamu, ni nini kimewapata? Je, mumepatwa na udhaifu na kuegemea kwenye maisha ya kidunia?! Je, ghera ya kukinga Dini ya Mwenyezi Mungu na matukufu yake imepotea kutoka nyoyoni na akilini mwenu?! Na kisha, enyi majeshi maisha yenu yanawezaje kuwa mazuri wakati hii ndio hali ya wanawake wenu huru?! Je hamuizingatii Siku ambayo mutasimama mbele ya Mwenyezi Mungu, Naye atakulipeni kisasi kwa kuhalifu amri yake na kuwatelekeza waja Wake?!

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu