Ijumaa, 08 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  20 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 027
M.  Jumanne, 11 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Rais wa Slovenia Hajui Historia, au Anaipuuza!
(Imetafsiriwa)

Hii ilikuwa katika mahojiano na Kituo cha Al Jazeera mnamo 9/11/2025, ambayo kituo kilitangaza kikamilifu asubuhi ya 10/11/2025. Kutoka ardhi ya Waislamu huko Qatar, Rais wa Slovenia, Nataša Pirc Musar, anasema: “Israel ina haki ya kuwa na dola.” Swali linaloelekezwa kwa rais ni: Ni nani aliyelipa umbile hili haramu la Kiyahudi haki hii? Na je, kuna mtu yeyote anayesoma historia na hajui jinsi umbile hili lemavu lilivyoanzishwa katika ardhi iliyobarikiwa ya Palestina? Je, mauaji ya Mayahudi dhidi ya Waislamu, watu wa Palestina, yanaondoka akilini mwa msomaji yeyote adilifu wa historia? Umbile hili lemavu lilisimamishwaje juu ya mafuvu na maiti za watu wengi wa Palestina? Na watu wake walihamishwaje mwaka wa 1948, kisha tena mwaka wa 1967? Na hiyo ilikuwa kwa msaada wa Uingereza na baadhi ya nchi za Ulaya na usaliti wa watawala wa dola jirani ya Palestina!

Baadhi ya misimamo iliyochukuliwa na nchi yake dhidi ya umbile la Kiyahudi haitamtetea Rais wa Slovenia, kama vile kuelezea uhalifu wake huko Gaza kama mauaji ya halaiki, au kutangaza kukataa kwa Slovenia kuruhusu maafisa wake wawili kuingia katika eneo lake, au kuzuia usafirishaji na uingizaji wa silaha kupitia Slovenia, au msimamo wake kuhusu makaazi ya Mayahudi huko Palestina, au misimamo mengine ambayo baadhi ya nchi za Ulaya na zengine zilichukua kwa aibu baada ya kashfa kubwa iliyosababishwa kwao na umbile la Kiyahudi na uhalifu wake huko Gaza unaofanya mwili kusisimka. Yote hayo hayatamtetea yeye au watawala wengine wowote duniani ambao hawajafanya chochote kuzuia uhalifu huo.

Wala utambuzi wa watawala wasio na maana wa Waislamu wa umbile la Kiyahudi, iwe waziwazi au kwa siri, hautamtetea, wala kuanzisha mahusiano nalo, wala kushindwa kwao kuwanusuru watu wa Gaza, wala msimamo wa mfumo wa kimataifa unaodhibitiwa na dola kubwa. Haijalishi ni wangapi wanaounga mkono batili, hautakuwa haki; batili itabaki kuwa batili, na haki itabaki kuwa haki.

Umma wa Kiislamu unahifadhi misimamo hii katika kumbukumbu yake na hautaisahau. Na Rais wa Slovenia, aliyewapa Mayahudi haki ya kuwa na dola nchini Palestina, ajue kwamba Siku ya Hesabu imekaribia tutakaposimamisha dola ya pili ya Khilafah kwa njia ya Utume hivi karibuni, Mwenyezi Mungu akipenda. Na ingawa Khilafah Uthmaniyya haikufanikiwa kueneza Uislamu nchini Slovenia katika karne ya kumi na nne wakati wa Vita vya Ottoman-Habsburg, Khilafah ijayo itafanya hivyo, na itamhisabu kila mtu mwenye wadhifa kwa wadhifa wake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu