Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
| H. 26 Jumada II 1447 | Na: H 1447 / 035 |
| M. Jumatano, 17 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Unyanyasaji wa Kimpangilio wa Kijinsia Dhidi ya Wanawake wa Sudan Hautoi Jibu lolote kwa Kukosekana kwa Dola Inayojali Heshima ya Mwanamke Mwislamu
(Imetafsiriwa)
Mnamo Alhamisi tarehe 11 Disemba, shirika, ‘The Strategic Initiative for Women in the Horn of Africa’, liliripoti kuwa limerekodi karibu matukio 1300 ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake katika majimbo 14 nchini Sudan tangu vita vianze nchini humo mnamo Aprili 2023, huku Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vikilaumiwa kwa 87% ya visa hivi. Lilielezea unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake ukitumika kama silaha ya kimfumo katika mzozo huo, likisema “umeenea, unarudiwa rudiwa, unakusudiwa na mara nyingi unalenga”. Ubakaji ulichangia robo tatu ya matukio yaliyorekodiwa, huku visa 225 vikihusisha watoto, baadhi wakiwa na umri wa miaka 4. Matukio yalitokea majumbani, maeneo ya umma na pia yalijumuisha kizuizini cha muda mrefu cha wanawake ambao waliteswa, kubakwa na genge na ndoa za kulazimishwa. Mnamo Jumapili tarehe 7 Disemba, vikundi vya matibabu vya Sudan viliripoti kwamba watoto na wanawake kadhaa walinyanyaswa kingono na kubakwa walipokuwa wakikimbia kukamatwa kwa El Fasher huko Darfur na RSF Oktoba hii. Mnamo Mei mwaka huu, Medecins Sans Frontieres (MSF) iliripoti kwamba katika eneo la Kusini mwa Darfur pekee, wafanyikazi wake waliwatibu manusura 659 wa unyanyasaji wa kijinsia kati ya Januari na Machi mwaka huu pekee, zaidi ya theluthi mbili kati yao wakiwa wamebakwa. Mratibu wa Dharura wa MSF, Clair San Filippo, alisema: “Wanawake na wasichana hawajisikii salama popote pale. Wanashambuliwa majumbani mwao, wanapokimbia ghasia, wanapopata chakula, wanapokusanya kuni, na kufanya kazi shambani. Wanatwambia wanahisi wamenaswa.”
Kile ambacho dada zetu nchini Sudan wamepitia katika mzozo huu ni cha kutisha kupita maelezo, ikiwa ni pamoja na kubakwa mbele ya watoto wao na jamaa zao na kukabiliwa na njaa, mateso na aina zote za unyanyasaji wa kinyama na wanamgambo. Unyanyasaji huu wa kingono wa kupangwa unarudia kile ambacho dada zetu wa Palestina wamepitia katika magereza ya uvamizi wa Kiyahudi; kile ambacho dada zetu wa Rohingya wamepitia mikononi mwa vikosi vya Myanmar; kile ambacho dada zetu wa Kashmir wamepitia kwa askari wa uvamizi wa India; na kile ambacho dada zetu wa Uyghur wamepitia katika kambi za mateso za serikali ya China.
Mtume wetu mpendwa (saw) aliwaonyesha Waislamu kwa zama zote, thamani kubwa inayotolewa kwa hadhi ya mwanamke wa Kiislamu katika Uislamu na umuhimu mkubwa wa kulinda hili kila wakati - alipowafukuza kabila zima la Kiyahudi, Banu Qaynuqa kutoka dola yake mjini Madina kutokana na unyanyasaji wao kwa mwanamke mmoja wa Kiislamu. Viongozi wa Waislamu wa zamani walifuata mfano wake wa kutetea heshima ya mwanamke Muislamu, kama vile Khalifah Al-Mutassim aliyetuma jeshi kumuokoa mwanamke mmoja Muislamu huko Amuriyah, Uturuki, ambaye alikamatwa na kutendewa vibaya na Warumi; na Khalifah al-Walid bin Abdul Malik aliyemtuma jenerali mkuu, Muhammad ibn Qasim na jeshi la kutisha kuwaokoa kundi la wanawake Waislamu waliofungwa na mfalme mkandamizaji wa Kibaniani wa India, Raja Dahir.
Kwa hivyo kama Ummah, tulifikiaje hali kama hiyo ambapo heshima ya dada zetu inakiukwa kwa wingi kote ulimwenguni, miili yao ikitumika kama silaha za vita, na bado hii haileti jibu kutoka kwa serikali yoyote, mtawala au jeshi katika nchi za Kiislamu?!!
Mtume (saw) amesema:
«الْإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ»
“Imam (Khalifa) wa watu ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake.” Leo, kwa kukosekana kwa Dola ya Khalifah, na mfumo wa Kiislamu anaoutawala – Khilafah kwa njia ya Utume – mwanamke wa Kiislamu amekuwa windo la kila nguvu, utawala na chombo fisadi, bila mlinzi wa kulinda heshima na damu yake. Mgawanyiko wa ardhi zetu katika dola za kitaifa, zilizotenganishwa na mipaka bandia ya kikoloni, umetufanya tugawanyike na dhaifu kiasi kwamba hakuna dola inayofanya kazi ya kuwalinda dada zetu. Kama Waislamu, haitoshi kumwaga machozi kuhusu hali mbaya ya dada zetu, au kuhisi maumivu kuhusu thamani yao, tunawajibishwa na Mwenyezi Mungu (swt) kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah ambayo itamaliza jinamizi hili ambalo dada zetu wanavumilia. Kwa hivyo, pazeni wito kwa dharura kwa ajili ya kuregea kwa Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt), ambao utaunganisha ardhi zetu, majeshi yetu, rasilimali zetu na kuweka ulinzi wa heshima ya wanawake waumini kama nguzo muhimu ya dola.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[وَالَّذينَ كَفَرُواْ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ إِلاَّ تَفْعَلُوهُ تَكُن فِتْنَةٌ فِي الأَرْضِ وَفَسَادٌ كَبِيرٌ]
“Na wale walio kufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe. Msipo fanya hivi itakuwako fitna katika nchi na fisadi kubwa.” [Al-Anfal: 73].
Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Kitengo cha Wanawake |
Address & Website Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info |



