Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 4 Safar 1441 | Na: 1441 H / 003 |
M. Alhamisi, 03 Oktoba 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kusitishwa kwa Muda kwa Tovuti za Hizb ut Tahrir Hivi Majuzi
(Imetafsiriwa)
Licha ya majaribio na njama zote zinazo fanywa na maadui wa Waislamu ili kuiondosha fikra ya Khilafah kutoka kwa akili za watu, fikra imekuwa ndio rai amma kwa Ummah wote Waislamu. Na bado "ulinganizi wa kusimamisha Khilafah" unaendelea kuzitia wasiwasi serikali za Kimagharibi na taasisi zake za kisiasa na kifikra na wanafanya kazi kwa bidii kwa kutumia njia zote ili kuzuia rai amma kutofikia ulinganizi huu wa baraka (Da'wah).
Mashirika ya "kibiashara ya kiufundi" yamejiunga na kundi la uadui ilhali yanadai kuwa hayaegemi mrengo wowote! Mashirika haya yamekubali kutumika kama zana za kisiasa katika mikono ya serikali ambazo zina uadui wa wazi dhidi ya fikra ya Khilafah. Cloudflare (baada ya miaka mingi ya huduma), ikifuatiwa na Stackpath, kwa ghafla yamekata DNS, ulinzi wa Tovuti na uwasilishaji wa huduma kutoka kwa tovuti za Hizb ut Tahrir pasina kutoa ilani ambayo imepelekea kwa tovuti hizo kufungwa mara mbili ndani ya miezi miwili iliyopita, ikimaanisha kuwa kampuni mbili ambazo zilitoa ahadi ya kuzilinda tovuti zetu wao wenyewe ndio waliozisitisha! Kwa hiyo ni usaliti na urongo wa aina gani huu?!
Inaoneka kwamba mawazo ya bwana wa sasa wa White House Donald Trump – ambaye amekuwa maarufu kwa uadui wake dhidi ya Waislamu na aghalabu pasina aibu hukiuka ahadi zake na kutumia urongo kusitisha nyingine. Inaonekana kuwa mawazo yake yamepenyeza katika kampuni hizi mbili na hatujui ikiwa yamejipenyeza katika mashirika mengine ya kibiashara na kiufundi ndani ya Amerika!
Na ili kuhalalisha mashambulizi yao, kampuni ya kwanza ilidai kuwa Hizb ut Tahrir ni chama kilichopigwa marufuku, na ile nyingine ikadai ukiukaji wa "Sera ya Matumizi Yanayokubalika"!
Licha ya kuwasiliana na kampuni zote mbili na kuwaonyesha ushahidi kamili na nyaraka rasmi kuhusu uharamu wa waliyofanya na kuwathibitishia kwamba Hizb ut Tahrir ni chama cha kifikra cha kisiasa kinachofanya kazi wazi ndani ya nchi nyingi duniani na katika miji mikuu maarufu, ambapo kinafanya makongamano, maandamano na kueneza fikra zake ndani ya jamii na kwamba chama hakitumii nguvu na kinafahamika katika kushikamana na njia yake kwa miongo saba na hili linajulikana na kutajwa kisiasa ndani ya kumbukumbu za kimataifa…
Na licha ya kuzionyesha kampuni zote kwamba Hizb ut Tahrir sio chama kilichopigwa marufuku isipokuwa katika nchi baadhi ambazo duniani zinatambulika kama nchi za kidikteta ambazo zinazuia kupeana nafasi ili kufanya amali za kisiasa, kama baadhi ya nchi za Mashariki ya Kati…
Na licha ya kuwaonyesha kwamba chama kinafanya kazi kihalali na wazi ndani ya nchi ambamo kampuni hizo mbili zimo…
Licha ya yote hayo, majibu ya kampuni hizo mbili yalikuwa ni kutuhamisha kwa kitengo cha kisheria ambacho kinajificha nyuma ya pepe ambayo inapokea jumbe na maswali lakini hawajibu! Ambayo inaweza kutajwa kuwa ni njama ya kunyamaza kinyama.
Ni sera ya Donald Trump kutumia urongo ambayo inaonekana kuchukuliwa na kampuni hizo mbili. Au inawezekanaje kwa kampuni mbili za kimataifa ambazo makao makuu yake ni Marekani (nchi ambayo ni maarufu kwa kufuata sheria na kusikiza kesi) itajaribu kwenda kinyume na sheria zake?! Itawezekana vipi wao kufanya hivyo kama si kwa kuwa rais wa nchi hiyo ameweka wazi sera ya usaliti na ukiukaji wa ahadi?!
Hili si chochote bali ni mwanzo wa kampeni mpya dhidi ya fikra ya “Khilafah kwa njia ya Utume” na ulinganizi wa kuisimamisha. Lau ni chochote, basi inaonyesha kufilisika kifikra kwa wahalifu waovu. Jaribio la kutunyamazisha ni tangazo la wazi la kushindwa kwa Wamagharibi mbele ya Hizb ut Tahrir inayobeba mfumo wenye nguvu, uliowazi na msafi.
Hizb ut Tahrir ni kundi la watu binafsi mukhlisina, walioitikia mwito wa Mwenyezi Mungu (swt):
[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ] “Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Al-i Imran:104].
Na hivyo leo, baada ya miongo saba tangu uzinduzi wake na uchangamfu wake juu ya “fikra” na “njia,” kundi hili hakika limekuwa taifa miongoni mwa mataifa (Ummah miongoni mwa Ummah), limekuwa taifa lililothabiti linaloifahamu njia yake ndani ya Ummah mtukufu unaojitolea kufanya kazi kuelekea katika siku adhimu za Khilafah.
Kampeni hii ya serikali ya Marekani na washirika wake katika mashirika maovu ya kiuhalifu, lau ni chochote, inaonyesha kufilisika kifikra kwa wahusika. Jaribio la kuinyamazisha midomo yetu ni tangazo la wazi la kushindwa kwao mbele ya Hizb ut Tahrir inayobeba mfumo wenye nguvu, bora, uliowazi na msafi. Na kufunga akaunti hazitodhoofisha Hizb ut Tahrir na idadi ya wale walio na hamu nao na kujua ukweli wa kile wanachokibeba na wale wanaotaka kufanya kazi nao na kuwanusuru, idadi za watu hawa zinaendelea kuongezeka kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) asema
[وَقَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَلِلَّهِ الْمَكْرُ جَمِيعاً يَعْلَمُ مَا تَكْسِبُ كُلُّ نَفْسٍ وَسَيَعْلَمُ الْكُفَّارُ لِمَنْ عُقْبَى الدَّارِ] “Na walipanga kabla yao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye mipango yote. Yeye anajua inayo chuma nafsi. Na makafiri watajua ni ya nani nyumba ya mwisho Akhera” [Ar-Ra’d:42]
Mha. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizb-ut-tahrir.info |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info |