Ijumaa, 09 Muharram 1447 | 2025/07/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Maingiliano ya Ummah na Hotuba: “Khilafah Ndio Mfumo wa Utawala katika Uislamu”

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilitoa hotuba ya kisiasa katikati mwa soko kuu la Port Sudan mnamo Jumatatu, 23 Disemba 2024, chini ya mada: “Khilafah Ndio Mfumo wa Utawala katika Uislamu.” Hotuba hiyo ilitolewa na Ustadh Yaqub Ibrahim mwanachama wa Hizb ut Tahrir ambaye alisisitiza kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewawajibisha Waislamu kutabikisha hukmu za Uislamu na kupangilia nyanja zote za maisha yao kwa mujibu wake. Alieleza kwamba utabikishaji huu hutokea kupitia Bay’a halali kwa Khalifa ambaye anasimamisha Dini na kuifikisha kwa ulimwengu.

Soma zaidi...

Mfano Hatari Ambao Haupaswi Kupuuzwa

Katika mfano hatari katika historia ya mapinduzi, Huduma Kuu ya Usalama mjini Aleppo iliteka nyara wanawake kumi mnamo siku ya Jumamosi, 21 Disemba 2024. Wanawake hao walikuwa wamejitokeza wakiandamana, wakitaka utawala wa Uislamu na kuachiliwa huru waume zao, vijana wao na watoto wao waliotekwa nyara zaidi ya mwaka mmoja na nusu uliopita. Watu hawa wamefungwa jela na Jolani [al-Julani] mjini Idlib tangu Mei 7, 2023!

Soma zaidi...

Mkutano wa Waandishi Habari juu ya Sarafu na Mshtuko wa Nixon

Kabla ya kuanzishwa kwa sarafu, watu walitumia ubadilishanaji wa bidhaa kwa huduma. Kwa kuwa dhahabu na fedha zimezingatiwa kuwa madini ya thamani yenye kima cha asili kwa binadamu tangu nyakati za zamani, zilitabanniwa kama pesa, huku sarafu zikichongwa kwazo ili kurahisisha ubadilishanaji. Dhahabu, hasa, inajulikana kwa kuhimili kwake kuharibika kwa muda mrefu.

Soma zaidi...

Mahouthi Wanaendelea na Jinai na Uhalifu wao... Kuwakamata Wanachama wa Hizb ut Tahrir

Kuanzia Alhamisi, tarehe 10 Jumada al-Akhir 1446 H sawia na tarehe 12 Disemba 2024 M, wanamgambo wa Houthi walifanya uvamizi kwenye nyumba za wanachama wa Hizb ut Tahrir bila ya kuzingatia vifungu vya sheria ya Kiislamu au hata kanuni na desturi za kikabila! Walivamia nyumba zao katika kurugenzi tatu za Jimbo la Taiz (Taiziyah, Mawiah, na Khadir); na kuwakamata: Suleiman al-Muhajri, Khaled al-Hami (waliyemwekwa kizuizini miezi sita iliyopita kwa tuhuma za kubeba Dawah pamoja na Hizb ut Tahrir), Mhandisi Taqi al-Din al-Zayla'i, Amir al-Sabry, na Muhammad al-Faqih. Wafuasi watatu wa Hizb ut Tahrir pia walikamatwa: Abdul Malik al-Jundi, Abdul Qader al-Sarari, na Adnan al-Zayla'i, ambao wanasalia chini ya ulinzi wa wahalifu hao mpaka kufikia wakati wa kuandika taarifa hii.

Soma zaidi...

Chini ya Urasilimali Utunzaji wa Afya huwa kama Fadhila tu wala Hauchukuliwi kuwa ni Haki Msingi

Serikali imeanzisha Mamlaka ya Afya ya Kijamii (SHA) ili kusimamia bima ya afya ya jamii nchini. SHA ina hazina tatu za kifedha: Hazina ya Huduma ya Afya ya Msingi, Hazina ya Bima ya Afya ya Jamii na ile ya hali ya Dharura na Ugonjwa hatari. Watoa huduma za afya nchini Kenya wanaweza kuingia katika kandarasi na mamlaka ya SHA ili kutoa huduma za afya kwa walengwa.

Soma zaidi...

Mapinduzi katika Ulimwengu wa Kiislamu Yatapelekea kwenye Mabadiliko ya Kweli Pale tu Watu wenye Nguvu Watakapotimiza Wajibu wao wa Shariah kwa Kuwaondoa Madhalimu na kuupa Nusra Ummah

Baada ya mabadiliko makubwa katika utawala wa Syria, baada ya mabadiliko ya utawala nchini Bangladesh na Afghanistan, pamoja na mabadiliko ya utawala yaliyokuja kabla ya haya, makundi tawala yanaendeleza simulizi ya zamani kwamba mapambano yaliyopangwa ya watu dhidi ya watawala yanazua “machafuko, ufisadi na ukosefu wa utulivu.” Iwe ni mkuu wa Jeshi la Pakistan, Jenerali Asim Munir, au watawala wengine, wote wanadai kwamba hawataruhusu nchi zao kuwa “Libya, Syria, Iraq au Sudan” nyengine.

Soma zaidi...

Mabadiliko ya Kweli Yanaweza Tu Kuja Kutokana na Mradi Unaotokana na Aqidah ya Ummah. Ni nani Aliye Nao?

Umma wa Kiislamu umeishi kwa karne moja katika unyonge na udhalilishwaji, mfarakano na mgawanyiko, na utegemezi kwa nchi kubwa. Hii inatokana na matendo ya watawala Ruwabidha (wajinga watepetevu) ambao hawaheshimu udugu au ahadi yoyote, wanachojali tu ni kubakia kwenye viti vyao vibovu (vya utawala), kutekeleza mipango ya nchi za Kikafiri katika ardhi zetu ili kukazanisha udhibiti wao juu yetu na kupora mali zetu. Wamesimama dhidi ya kila mtu anayewapinga au kutokubaliana nao, au kujaribu kuwabadilisha, na kuwaweka chini ya kifungo, mateso, mauaji, na ukiukaji wa matukufu. Bashar al-Assad na utawala wake wa kihalifu sio wa mwisho wao, ambaye uhalifu dhidi ya watu wake ulifichuliwa na matukio ya hivi majuzi nchini Syria, uhalifu ambao ni wa aibu na kuwafukuza wale wenye maumbile yaliyo sawa.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir Inalingania Ukombozi wa Ardhi za Waislamu kutokana na Ukoloni

Hizb ut Tahrir imekuwa mada ya mjadala wa kijamii ndani ya duara zenye ushawishi za Pakistan. Mjadala huo unajumuisha kama tiba za Shariah kwa matatizo ambayo Hizb ut Tahrir inayawasilisha zinapaswa kutekelezwa ili kuepuka matatizo mengi ambayo Pakistan inakabiliana nayo. Kuna mjadala mkali kuhusu Hizb ut Tahrir yenyewe, ikiwemo kupigwa marufuku kwake nchini Pakistan na msimamo mkali dhidi yake katika suala la mateso, unyanyasaji na kifungo. Kwa maslahi ya mjadala wenye tija, mambo yafuatayo ni ya kuzingatiwa na wenye ushawishi kwa jumla na watunga sera, waandishi wa habari, mashirika ya haki za binadamu na ndugu wanasheria hasa.

Soma zaidi...

Uvamizi wa Umbile la Kiyahudi na Mashambulizi Yake ya Kiadui kwenye Ardhi ya Ash-Sham Jinai zinazoendelea ambazo ni Utawala wa Uislamu na Dola Yake ya Khilafah Pekee ndio Unaoweza Kusitisha na Kuvunja Nguvu yao

Tangu kuanguka kwa dhalimu Assad mnamo tarehe nane mwezi huu, makundi ya umbile la Kiyahudi yamekuwa yakishambulia ardhi ya Ash-Sham, na ndege zake zimekuwa zikivamia anga yake kwa mashambulizi ya angani yenye nia mbaya ambayo yalilenga miji kadhaa, na maeneo ya kijeshi. Mashambulizi haya yamefika katika mji wa Deir ez-Zor mashariki mwa Syria. Mashambulizi hayo ya chuki na kihalifu yamejikita kwenye maghala ya silaha, vikosi vya ulinzi wa anga katika maeneo ya kati na kusini, vituo vya utafiti wa kisayansi wa kijeshi, na viwanja vya ndege vya kijeshi, ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa kijeshi wa Al-Mazzeh viungani mwa Damascus.

Soma zaidi...

Matukio ya Uhalifu Yanayofichuliwa Katika Magereza ya Dhalimu wa Ash-Sham Yanapasa Kuwasha Moto Nyoyoni mwa Wana wa Ummah Kuwateketeza Watawala

Katika siku chache zilizopita baada ya kutoroka kwa dhalimu Bashar na kuanguka kwa utawala wake muovu, matukio ya uchungu na makali yalifichuliwa ambayo yalivunja nyoyo za Waislamu. Kwani waliona kwa macho yao ukubwa wa jinai na ukatili ambao utawala wake uliamiliana nao kwa ndugu na dada zao katika vituo vya uzuizi na magereza: kuanzia na kuwekwa kwao kizuizini kwa miongo kadhaa katika magereza ambayo yalikosa mahitaji msingi zaidi ya kibinadamu, kisha njaa, ukandamizaji na mateso ya kikatili ambayo magereza hayo na kuta zinayazungumzia, na seli, nguzo na zana za mateso zinazosimulia hadithi zao, na miili ya wahasiriwa waliopatikana wamekufa na kukatwakatwa inamfichua.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu