Siku baada ya siku, matukio na misimamo inafichua ushahidi mwingi wa dola za kikoloni za kikafiri kuwaogopa Waislamu, ikiwemo umbile vamizi la Kiyahudi. Pia inaonyesha kwamba wanapoamiliana na Waislamu, wanawachukulia kwa uzito mara elfu moja. Baada ya zaidi ya karne moja, baada ya kuvunjwa kwa Khilafah, kugawanyika kwa Waislamu na kuwa maumbo dhaifu, nyenyekevu, ikifuatwa na udanganyifu na uvamizi wa kifikra, kujitenga kwa Waislamu na imani yao, kuporwa mali ya Waislamu, kupanuka kwa ushawishi wa wakoloni hao makafiri katika ardhi zao, na kudhoofika kwao na kudhalilika, baadhi wanasema: Waislamu kamwe hawatainuka tena, na baada ya haya yote, tunasikia na kuona kauli kutoka kwa viongozi wa Magharibi na viongozi wa umbile vamizi la Kiyahudi, ambazo zinaonyesha hofu yao ya Uislamu na hofu iliyojaa nyoyoni mwao kutoka kwa Waislamu katika hali hii.