Jumanne, 29 Safar 1446 | 2024/09/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia Yawasilisha Barua ya Wazi kwa Waziri wa Sheria

Asubuhi ya Alhamisi, tarehe 01/06/2023, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia, akiwemo Mkuu wa Afisi ya Kisiasa Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Yassin bin Yahya, na mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano Ustadh Mwanasheria Fathi Al-Khamiri, na mjumbe wa Afisi ya Habari Ustadh Ahmed Al-Tatar, walimkabidhi Waziri wa Sheria, Bi Leila Jaffal, barua ya wazi kuhusu kukithiri kwa kukamatwa mara kwa mara kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Tunisia.

Soma zaidi...

Uhalifu wa Kivita wa Mkongwe wa Vita Aliyepambwa Zaidi wa Australia ni Akisi ya Sera ya Vita ya Serikali

Madai ya uhalifu wa kivita dhidi ya mkongwe wa vita aliye hai nchini Australia, Ben Roberts-Smith, yalipatikana kuwa "kweli kabisa" na jaji wa Mahakama ya Shirikisho. Jaji huyo alihitimisha kuwa madai ya kuwashambulia na kuwaua Waafghani wasio na hatia na wasio na silaha yalithibitishwa, na kwamba alileta fedheha kwa nchi yake na jeshi la Australia kwa kuvunja 'kanuni za maadili na kisheria' za ushiriki wa kijeshi.

Soma zaidi...

Ujasusi wa Ufaransa Waikanyaga Sheria na Kufichua Ukweli kuhusu Nchi ya Maarifa na Uhuru kwa Kuomba Kufanyika Sensa ya Watoro Shuleni siku ya Idd al-Fitr!!

Gazeti la kila siku la Ufaransa la La Dépêche lilichapisha mnamo Ijumaa, Mei 19, 2023, habari iliyosema kwamba takriban shule mia moja huko Toulouse na vitongoji vyake zilipokea barua pepe kutoka kwa polisi wa Ufaransa wakiomba kiwango cha utoro wa wanafunzi mnamo Aprili 21, 2023, ambayo ilisadifu kuwa ni sikukuu ya Idd al-Fitr.

Soma zaidi...

Bandari Mpya ya Miungano "Uadui kwa Wakimbizi"

Kwa kuwa hapakuwa na mgombea ambaye asilimia ya kura zake zilizidi 50 + 1 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili, Mei 14, raundi ya pili ya uchaguzi itafanyika mnamo Jumapili, Mei 28. Kwa sababu ya kauli zilizorushianwa kati ya miungano, vyama na viongozi wakati wa mchakato wa uchaguzi, jamii iligawanywa katika sehemu mbili, na watu wakawa maadui wa kila mmoja.

Soma zaidi...

Jeshi la Al-Kinana ni Ngao ya Uislamu na Msaidizi wa Ummah Hivyo ndivyo lilivyokuwa na hivyo ni lazima Lirudi Kuwa

Hayat Washington ilisema kwenye tovuti yake, Jumatatu, 22/5/2023, kwamba vyombo vya habari vya Nigeria viliripoti kwamba Shirika la Miradi ya Huduma ya Kitaifa ya Wizara ya Ulinzi ya Misri inakusudia kuwekeza katika sekta ya kilimo katika jimbo la Ogun (magharibi).

Soma zaidi...

Australia Yamkaribisha Muuaji wa Gujarat, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

Australia inatarajiwa kumkaribisha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ziara ya siku tatu kuanzia leo. Hii ni ziara ya pili ya Modi nchini Australia tangu alipokaribishwa mara ya kwanza mnamo 2014.

Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema katika Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa leo: "Ninafurahi kuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu Modi kwa ziara rasmi nchini Australia, baada ya kupokea makaribisho mwanana nchini India mapema mwaka huu."

Soma zaidi...

Marekani Inasisitiza Kuikalia Anga ya Afghanistan, Sisi Tunasisitiza Kusimamishwa Khilafah!

Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM), Jenerali Michael Kurilla aliwasilisha ripoti kwa Bunge la Congress kuhusu operesheni yao ya kijasusi kuanzia robo ya kwanza ya mwaka huku akisema kuwa Taliban wana dhamira kubwa ya kuiangamiza Dola ya Kiislamu-Khorasan (IS-K) nchini humo, lakini kulingana na yeye, Taliban hawana uwezo wa kuzuia mashambulizi ya kigaidi ya mustakbali ya kundi hilo lililotajwa. Hivyo basi, Marekani inaongeza juhudi za uchunguzi juu ya anga ya Afghanistan.

Soma zaidi...

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Mhandisi Ismail Al-Wahwah (Abu Anas)

Kwa imani na kujisalimisha kwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Jordan inaomboleza kwa Waislamu kwa jumla, na watu wa Jordan na Waislamu hasa wa Australia, mmoja wa wanachama wanyoofu, wenye subira na waheshimika wa hizb, mwenye misimamo imara yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw), na sisi hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.

Mwanafikra wa kisiasa kutoka kizazi cha zamani cha wanachama wa Hizb ut Tahrir

MhandisiIsmail Al-Wahwah (Abu Anas)

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu