Alhamisi, 26 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Enyi Waislamu! Mahusiano ya Siri na Umbile la Kiyahudi Yanaonyesha kwamba Watawala wa Kisekula na Wanasiasa ndio Adui wa Waislamu na Uislamu

‘The New Age’ na magazeti mengine mashuhuri nchini Bangladesh yalichapisha ripoti mnamo Januari 11, 2023 kwamba serikali ya Bangladesh ilinunua kwa siri programu za ujasusi na zana za uchunguzi wa hali ya juu mwaka jana kutoka kwa kampuni inayoendeshwa na kamanda wa zamani wa kitengo cha teknolojia cha ujasusi cha umbile haramu la Kiyahudi 'Israel'. Serikali ya kinafiki ya Hasina imechagua kuwa mshirika na wale waliolaaniwa na Mola wa ulimwengu (swt).

Soma zaidi...

Serikali Inaiba Akiba ya Watu Iliyo Chumwa kwa Tabu kupitia Kuchapisha Pesa Mpya bila Uegemezi wa Mali Halisi; ni Kipimo cha Madini Mawili (Dhahabu na Fedha) cha Dola ya Khilafah pekee ndicho kinacho weza kumaliza Utawala wa Kifedha wa Urasilimali

Benki ya Bangladesh iliunda pesa mpya kwa zaidi ya Taka bilioni 500 katika kipindi cha Julai-Disemba kwa jina la usaidizi wa bajeti, ambazo ni za juu zaidi katika historia ya hivi majuzi (The Business Standard, Januari 03, 2023), ili kufidia pesa zilizoporwa kutoka kwa mabenki na kipote cha Mabepari.

Soma zaidi...

Wito kutoka kwa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia kwa Watu wetu nchini Tunisia

Mumeshuhudia jinsi demokrasia ilivyo fisidi maisha yenu, na kuifanya ardhi yenu kuwa mahali pazuri kwa matamanio ya nguvu zinazodhibiti jamii kwa pesa na ushawishi kwa jina la watu na kinyume na matakwa yao, na mukashuhudia usaliti wa kituo kizima cha kisiasa na shauku yao ya kuzitii serikali za kikoloni za Magharibi hadi zikaiingiza Tunisia chini ya usimamizi wa ukoloni na taasisi zake za kifedha, na juu yazo ni Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, chombo hatari cha wakoloni.

Soma zaidi...

Ubalozi wa Marekani waalika Kamati ya Walimu nchini Sudan kwenye Mkutano Watawala wa Sudan, mko wapi? Mumetuletea Fedheha Gani?!

Imeelezwa katika gazeti la Al-Sudani lililotolewa leo Jumanne tarehe 10/1/2023 na vyombo vyengine vya habari kwamba, Afisi ya Utendaji ya Kamati ya Walimu ya Sudan ilipokea mwaliko kutoka kwa Ubalozi wa Marekani jijini Khartoum kufanya kikao cha pamoja, na Kamati hiyo ilisema katika taarifa yake fupi jana jioni kuwa kikao hicho kinalenga kujadili baadhi ya masuala yanayohusu Elimu, na athari za mgomo wa sasa wa walimu.

Soma zaidi...

Mgogoro wa Kiuchumi wa Misri, kwa kweli, ni Mgogoro wa Kimfumo Ndio Mzizi wa Maradhi na Chanzo cha Mateso

Umaskini uliokithiri, ukosefu wa ajira uliogubika, machafuko ya kisiasa na kiuchumi, utajiri wa kupindukia kwa wachache kwa gharama ya watu wengi, kushuka kwa thamani ya pauni dhidi ya fedha za kigeni kusikokuwa na kifani, kula akiba za watu, kushuka kwa kiwango kikubwa cha maisha, kuongezeka kwa kasi kwa deni la umma, kupanda kwa bei kusiko na kifani, kupuuza rasilimali za kiuchumi na kimkakati kwa ajili ya maadui wa Ummah...

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu