Afisi ya Habari
Denmark
H. 9 Muharram 1447 | Na: 01 / 1447 H |
M. Ijumaa, 04 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mjadala juu ya Upandaji wa Malori ya Kuhitimu Unafichua Chuki iliyokithiri ya Vyombo vya Habari na Wanasiasa wa Denmark dhidi ya Uislamu
(Imetafsiriwa)
Wiki hii iliyopita kumeshuhudiwa vurumai kubwa la vyombo vya habari na kisiasa kutokana na machapisho ya mitandao ya kijamii ambapo Waislamu waliwapongeza wahitimu wa mwaka huu huku pia wakiwasilisha mtazamo wa Kiislamu kuhusu kupanda malori ya kuhitimu yenye sifa ya ulevi na tabia mbaya.
Ukumbusho huu wa Kiislamu, ambao kwa jumla umekuwa wa kuridhisha na uliojadiliwa vyema, umezusha mtafaruku katika vyombo vya habari vya kitaifa na miongoni mwa wanasiasa katika wigo wa kisiasa katika Christiansborg. Wakisukumwa na chuki yao kubwa dhidi ya Uislamu, wameanzisha mashambulizi ya kibinafsi dhidi ya Waislamu waliotajwa, akiwemo mwanachama mmoja wa Hizb ut Tahrir / Denmark. Ijapokuwa ni jambo rahisi la kueleza maadili ya Kiislamu na kuwahimiza Waislamu wenzao kuzishikamana nayo kwa fahari, baadhi ya waandishi wa habari na wanasiasa waovu wamejaribu kuwanyamazisha Waislamu kwa kuyaburuza maisha yao ya kitaaluma ndani ya suala hilo.
"Wataalamu" waliojitangaza kibinafsi na pamoja na walioajiriwa na serikali, pamoja na wanasiasa wa taaluma ambao kwa muda mrefu walifichua kuwa hawana maadili wala adabu, wamejipanga kuchangia katika kuwachafulia jina Waislamu wanaokataa kusalimisha au kukaa kimya kuhusu maadili yao ya Kiislamu. Maneno ya kawaida kuhusu udhibiti hasi wa kijamii, hofu, na kutengwa yanatupwa kiliberali.
Waziri wa Uwiano, Kaare Dybvad Bek (Social Democrats), pia alijiunga na mahojiano ya watu wasio na akili katika BT mnamo 2 Julai 2025. Alielezea utamaduni wa unywaji pombe wenye matatizo waziwazi miongoni mwa vijana wa Denmark kama “[…] sehemu ya utamaduni wetu, na nadhani mtu anapaswa kuukubali badala ya kujaribu kuunda tatizo kutokana nao.” Kwa waziri huyo, kukataa hili ni "inaogofya" pamoja na kufanya iwe "vigumu kuona jinsi mtu anavyoweza kuwa sehemu ya jamii ya Denmark."
Tangu wakati huo, Waziri wa Utamaduni - na dereva wa zamani wa cocaine - Jakob Engel-Schmidt (Moderates) pia ametafakari, akijiteua mwenyewe mwamuzi wa maadili wa kile ambacho Waislamu wanapaswa kuamini ili kukubalika nchini Denmark.
Mtu anapaswa kujiuliza hasira hii kubwa ya kisiasa imekuwa wapi kwa siku 637 za mauaji ya halaiki yanayoungwa mkono na Denmark nchini Palestina. Na juu ya kile ambacho vyombo vya habari vinavyounga mkono mauaji ya halaiki na wanasiasa wanafikiria kuwa wanasimama wanapojaribu kuhubiri "maadili" kwa Waislamu. Kama kawaida, linapokuja suala la semi za Kiislamu, uhuru wa kujieleza unaosifiwa sana ghafla unakuwa vigumu kupatikana.
Kwa vijana wa Kiislamu, tunasema:
Pongezi za dhati kwenu nyote ambao, licha ya shinikizo kutoka kwa wenye nguvu na wenye chuki, mnashikilia imara maadili yenu ya Kiislamu na kukataa kutishwa. Kupitia msimamo wenu, nyinyi ni mifano ya kuigwa kwa vijana wengine karibu nanyi na mifano angavu ya vijana walio na maadili ya kweli na uadilifu wa kibinafsi - muhimu zaidi kuliko alama (grade) yoyote ya shule. Wale wanaotaka kukiponda kitambulisho chenu cha Kiislamu wanakosa hata adabu au ubinadamu wa kimsingi. Msikate tamaa wanapojaribu kukuchafulieni majina. Shirikini kikamilifu katika jamii na mubebe Uislamu wenu pamoja nanyi kwa maneno na vitendo - hii ndiyo tiba yenye ufanisi zaidi dhidi ya chuki na uongo. Msihuzunike wanapojaribu kukuaibisheni au kukutisheni. Wanadhoofisha tu kile kinachojulikana kama "uhuru" wao wenyewe na kufichua jinsi kweli misingi yao ilivyo dhaifu. Si wao, ila ni Mwenyezi Mungu ndiye anaye kuruzukuni mafanikio – na Yeye yu pamoja nanyi daima. Mna kila sababu ya kujivunia, kwani nyinyi ni fahari ya jamii yote ya Kiislamu!
Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Denmark
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Denmark |
Address & Website Tel: |