Marekani Yaendesha Uharibifu... Na Watawala ni Watiifu kwa Miradi Yake ya Kikoloni!
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mamlaka zilizofuatana juu ya nchi yetu hazikujiepusha na kutii mashinikizo ya Marekani, kwa kukubali kushiriki katika kuimarisha mkakati wake wa kikoloni katika kuitawala dunia nzima, ikiwemo kanda yetu ya Waarabu na eneo letu la Afrika. Hii ni kama vile kusainiwa na utawala wa Sebsi juu ya uamuzi wa Barack Obama wa kuipa Tunisia hadhi ya Mshirika Mkuu Asiyekuwa mwanachama wa NATO, au kufungua nchi yetu kwa mpango wake barani Afrika kwa kuandaa, kwa mwaka wa nane mfululizo, mazoezi ya kijeshi ya African Lion 2025, ambapo Jenerali Dagvin Anderson, kamanda wa Kamandi ya Marekani ya Umoja wa Mataifa Afrika (AFRICOM) alisema mbele ya Kamati ya Huduma za Silaha katika Bunge la Congress la Marekani kwamba Morocco na Tunisia ni miongoni mwa washirika wenye uwezo mkubwa wa kusafirisha usalama barani humo.
 
			



 
  
  
  
  
  
  
  
  
 