Alhamisi, 22 Muharram 1447 | 2025/07/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Haya ndiyo Matendo ya Umoja wa Mataifa... Mutaendelea Kuwahadaa Wananchi Mpaka Lini? Ni Kipi Kipya? Yako wapi Mabadiliko, Ee Wizara ya Ujenzi na Mabadiliko?

Mnamo Jumapili, tarehe 29/6/2025, jijini Sana'a, Waziri wa Masuala ya Kijamii na Leba, Samir Baja'ala, alifanya mkutano na kamati za maandalizi ya Kongamano la Vyama vya Ushirika la 2025, litakaofanyika mapema Julai 2025. Mkutano huo ulihudhuriwa na Ali Al-Razami, Katibu Mdogo wa Wizara ya Sekta ya Maendeleo na Nasser Al-Kahili, Mkurugenzi wa Afisi ya Masuala ya Kijamii na Afisi ya Leba katika Sekretarieti Kuu.

Soma zaidi...

Uamuzi wa Mahakama ya Upeo Unaipa Zinaa Nafasi sawa na Ndoa

Mahakama ya Upeo imeamua kuwa watoto waliozaliwa nje ya ndoa na baba Waislamu wana haki ya kurithi mali ya baba yao, jambo linaloashiria maendeleo makubwa katika tafsiri ya sheria za kibinafsi za Kiislamu nchini Kenya. Hii ni baada ya Mahakama ya Juu mnamo Jumatatu tarehe 30 Juni kutupilia mbali rufaa ya Fatuma Athman Abud Faraj, ambaye alitaka kuwatenga watoto wa marehemu mumewe, Salim Juma Hakeem Kitendo, katika mali yake kwa madai kwamba walizaliwa nje ya ndoa inayotambulika ya Kiislamu.

Soma zaidi...

Ongezeko la Wanamgambo nchini Sudan Linasonga Kaskazini!

Tangu Ijumaa, tarehe 27/6/2025, vyombo vya habari vimeripoti kuwa Rais wa Eritrea Isaias Afwerki amekubali kutoa mafunzo kwa wapiganaji elfu 50 kutoka majimbo ya Kaskazini na Mto Nile katika mafunzo ya juu ya kijeshi, kulingana na ombi lililowasilishwa na mkuu wa Jimbo la Kaskazini, Mohamed Sayed Ahmed Al-Jakoumi, mkuu wa Upande wa Kaskazini wa Makubaliano ya Juba ya Amani ya Sudan.

Soma zaidi...

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Diya')

Kwa imani kamili juu ya qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kutaka malipo kutoka Kwake, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan inaomboleza kwa kuondokewa na mmoja wa wabebaji wake wa Da’wah: Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Diya'), ambaye alifariki dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo Alhamisi, tarehe 1 Muharram 1447 H sawia na 26 Juni 2025 M, akiwa na umri wa miaka 89, baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo alikuwa na subira na kwa kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu.

Soma zaidi...

Kuna Tofauti Kubwa kati ya Utu chini ya Uislamu na Udhalilifu chini ya Ukandamizaji wa Tawala za Kitumwa

Kamati ya Kuu ya Mitihani ya Cheti cha Sudan ilitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na mashirika husika kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu na kusaidia kuwawezesha wanafunzi wote wa Sudan kufanya mitihani, hasa katika maeneo yaliyoathiriwa na vita na hali ngumu ya kibinadamu. (SUNA, Juni 26, 2025)

Soma zaidi...

Trump na Netanyahu Wanajigamba na Kujisifu Huku Watawala Wetu Wakikaa Kimya Mithili ya Wafu Makaburini Mwao!

Vita kati ya Iran na umbile la Kiyahudi vimemalizika, na jinai za Mayahudi mjini Gaza hazikukoma wakati wa vita hivyo, wala hadi wakati huu. Marekani ilifanya ujanja wa kiusanii, ikidai kuwa imeangamiza uwezo wa nyuklia wa Iran. Hatua hii imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kukutana na wale wanaojiita mawaziri wa Troika wa Ulaya, ambao walikuwa sehemu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran kabla ya Marekani kujitoa katika mazungumzo hayo wakati wa muhula wa kwanza wa Trump. Iran pia ilifanya mbwembwe za kiusanii kwa kurusha makombora kadhaa katika Kambi ya Kimarekani ya Al Udeid nchini Qatar, baada ya kuifahamisha Marekani kuhusu hilo, kama Trump mwenyewe alivyosema.

Soma zaidi...

Jinsi Dola Kubwa Zinavyozaliwa Utotoni mwao

Ni kweli kwamba dola kubwa hazizaliwi ghafla mara moja, lakini hakuna shaka kwamba zinajengwa juu ya itikadi ambayo kwayo mfumo huchipuka. Wakati wa kuzaliwa kwake, fikra yake ilijumuishwa katika kundi ambalo lilijitolea mhanga mali zake za thamani zaidi na kuiunga mkono kivitendo ndani yake. Hili lilizaa dola yake, ambayo ilijizatiti kujitengenezea njia kuelekea uongozi wa kimataifa kwa msingi wa itikadi yake, kufikia haki na rehema kulingana na viwango vya asili ya kimungu katika miongo michache tu. Ni lazima kwa Ummah ambao kwa hakika unataka kurudisha nafasi yake ya hadhi miongoni mwa mataifa, si tu duniani kote, kuregea kubeba ujumbe wake kwa ulimwengu na kulazimisha uongozi wake wa kifikra na utawala wake juu ya fikra za dhulma, ubabe, na utumwa, na kufikia ukombozi wa kifikra na wa kimada. Umma huu lazima uvuke hisia, mambo ya kijuujuu, na lugha ya maneno hadi vitendo.

Soma zaidi...

Serikali ya Hindutva ya India Inaendelea Kutumia Shirika la Kitaifa la Uchunguzi kwa Kazi yake Chafu

Mnamo tarehe 14 Juni 2025, Shirika  la Kitaifa la Uchunguzi (NIA) lilifanya uvamizi ulioratibiwa katika maeneo matatu huko Bhopal, Madhya Pradesh, na miwili huko Jhalawar, Rajasthan, kuhusiana na kesi ya Hizb ut Tahrir (HuT). Operesheni hiyo ililenga kukusanya ushahidi zaidi dhidi ya HuT. NIA ilidai kuwa uvamizi huu ulisababisha kukamatwa kwa "vifaa vya kidijitali na nyenzo za hatia" (vitabu na vifaa vya kuandikia tunavyodhania). Kabla ya uvamizi huu, Jharkhand (jimbo) ATS ilikuwa imewaweka kizuizini watu wawili kuhusiana na kesi ya Hizb ut Tahrir. Serikali ya India ilipiga marufuku kinyume cha sheria Hizb ut Tahrir mnamo tarehe 10 Oktoba 2024, ikitaja juhudi zake za kusimamisha "Khilafah" ya kimataifa kupitia ugaidi na itikadi kali.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu