Jumanne, 25 Safar 1447 | 2025/08/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  20 Safar 1447 Na: 02 / 1447 H
M.  Alhamisi, 14 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Msako Mkali wa Amerika dhidi ya Mashirika ya Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano ya hivi majuzi na mtangazaji wa redio Sid Rosenberg, Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio alionyesha mchakato unaoendelea wa kuiorodhesha Ikhwan al-Muslimin na CAIR kama mashirika ya kigaidi. Waziri Rubio alisema kwamba uorodheshaji kama huo ulikuwa "katika kazi zao, na ni wazi kuna matawi tofauti tofauti ya Ikhwan al-Muslimin, kwa hivyo itabidi uliorodheshe kila moja yao."

Ingawa Rubio alikubali uorodheshaji kama huo unahitaji michakato ya kisheria kuhimili changamoto katika mahakama, maoni yake yanaonyesha mwelekeo unaokua wa kuzipa kibandiko mavuguvugu fulani ya Kiislamu - ya kigeni na ya ndani - kama tishio la usalama wa kitaifa na wapinzani kwa sera ya kigeni ya Amerika. Hii inaakisi kauli za awali za Waziri wa Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, ambaye alisema kwamba Mahmoud Khalil amelengwa kwa kuwa "mpinzani wa sera ya kigeni na maslahi ya usalama wa taifa ya Marekani."

Kwa miongo kadhaa, Waislamu nchini Marekani wamekuwa wakichunguzwa, kulengwa, kufanyiwa uhalifu, na kutishwa chini ya kivuli cha kupambana na ugaidi na usalama wa taifa. Matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu kutoka kwa tawala zilizopita, za Democratic na Republican, yamezua jinai za chuki dhidi ya jamii ya Kiislamu.

Hili sio tu kuhusu Ikhwan al-Muslimin au CAIR, bali linaathiri mashirika yote ya Kiislamu na jamii zetu wakati huo huo. Kulengwa kwa mashirika ya Kiislamu kwa sababu za kisiasa - hasa yale yanayotetea sababu za Kiislamu au utawala wa Kiislamu - hakuwezi kutazamwa kwa kutengwa na mwelekeo mpana wa uadui dhidi ya Uislamu.

Mtume (saw) na Maswahaba (ra) walikabiliwa na marufuku mithili ya hazo za kisiasa, kuhamishwa, na kampeni za kupaka matope mjini Makka - si kwa sababu ya vurugu, bali kwa sababu ya kulingania Uislamu.

Uislamu unatuwajibisha sisi Waislamu kuilinda Dini yetu, kusema ukweli, na kupangilia kwa pamoja ustawi wa Umma. Sisi Waislamu nchini Amerika lazima tusimame pamoja juu ya Haqq (ukweli), tuunganishe sauti zetu, tulindane sisi kwa sisi, na tukatae vitisho vilivyokusudiwa kutunyamazisha na kutufanya tufiche Dini yetu.

Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha:

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ] Hakika Waumini ni ndugu...” [Al-Hujurat: 10]

[وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاء بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَـئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللّهُ إِنَّ اللّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima. [At-Tawbah: 71].

Sisi, kutoka Hizb ut Tahrir, tunayashajiisha mashirika yote ya Kiislamu kuwa walinzi wao kwa wao. Hili halihusu shirika moja. Hili linahusu kuendelea kuwepo kwa kitambulisho chetu cha Kiislamu nchini Marekani.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Tanzia ya Anas Al-Sharif na Wenzake

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu