Jumatano, 08 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  2 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 03 / 1444 H
M.  Jumatatu, 22 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Australia Yamkaribisha Muuaji wa Gujarat, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi

(Imetafsiriwa)

Australia inatarajiwa kumkaribisha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa ziara ya siku tatu kuanzia leo. Hii ni ziara ya pili ya Modi nchini Australia tangu alipokaribishwa mara ya kwanza mnamo 2014.

Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema katika Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa leo: "Ninafurahi kuwa mwenyeji wa Waziri Mkuu Modi kwa ziara rasmi nchini Australia, baada ya kupokea makaribisho mwanana nchini India mapema mwaka huu."

Pia aliendelea kueleza kusudi msingi la ziara hiyo aliposema: “Australia na India zinashirikiana katika kujitolea kwa Indo-Pasifiki yenye utulivu, salama na yenye ufanisi. Kwa pamoja tuna dori muhimu katika kuunga mkono ruwaza hii.”

Hizb ut Tahrir / Australia ingependa kusema yafuatayo:

1. Narendra Modi aliwekwa madarakani kwa kutegemea mauaji ya Waislamu yaliyoratibiwa huko Gujarat mwaka wa 2002, ambayo baadaye yalienea kote India na kupanuka baada ya kukwea kwake madarakani. Modi alituzwa kwa sera zake za chuki dhidi ya Uislamu kwa kuungwa mkono na kukumbatiwa na nchi kama Australia.

2. Ukumbatiaji wa Australia wa India chini ya Modi unatokana hasa na hamu ya kudumisha utawala wa Amerika katika Asia Pasifiki, kama sehemu ya juhudi nyingi za Amerika zinazolenga kukabiliana na ukuaji wa China katika eneo hilo.

3. Uhalifu wa Modi dhidi ya Waislamu nchini India ni wa kushutumiwa kama vilevile uhalifu wa China dhidi ya Waislamu huko Turkestan Mashariki. Ukweli kwamba Australia iko tayari kuzikumbatia nchi zote mbili kwa ajili ya umuhimu wa kiuchumi na kisiasa hauonyeshi tu jinsi maisha ya Waislamu yasivyo kuwa na budi kwa Australia, lakini jinsi Australia imekuwa isiyojali kila mara kwa mateso ya Waislamu kama matokeo ya sera zake zenyewe au sera za nchi zake marafiki.

4. Ziara ya Modi nchini Australia ni kofi usoni mwa Waislamu wote, ambao kwa pamoja wanahuzunishwa na uhalifu unaotendwa dhidi ya ndugu zao nchini India, na kuweka wazi madai matupu ya kuheshimiana ambayo mara nyingi husifiwa chini ya madai ya Australia ya mafanikio ya dhana ya tamaduni nyingi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu