Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  25 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 05 / 1444 H
M.  Jumatano, 14 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Serikali ya Australia Yatafuta Kupiga Marufuku Nembo za Uislamu kwa Kisingizio cha Ugaidi

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Australia leo imeashiria kuanzishwa kwa sheria inayolenga kuharamisha nembo za chuki.

Mark Dreyfus, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Majimbo, alisema hivi leo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari: “Serikali ya Albanese leo imeanzisha mageuzi ya kina ili kulinda jamii dhidi ya wale wanaotaka kueneza chuki na kuwachochea wengine kufanya vitendo vya ugaidi.” Aliendelea kusema Mswada huo "utafanya kuwa ni kosa la jinai kuonyesha hadharani alama za Nazi na Dola ya Kiislamu au biashara ya vitu vyenye nembo hizi.

Sheria hii daima ilikusudiwa kuharamisha nembo ya Nazi, lakini bila kupitwa na fursa, serikali ya Leba imeongeza kwa siri hatua ambazo zinaharamisha nembo za Kiislamu, pamoja na kupanua uingiliaji wa mapema na vifungu vya kuzuia sheria zilizopo za ugaidi.

Hizb ut Tahrir / Australia inasema yafuatayo:

1. Serikali ya majimbo ya Leba inalenga kupanua, kama inavyofanya siku zote, vita dhidi ya sera za ugaidi za miongo miwili iliyopita. Uhusiano wake na Uislamu na Waislamu unahukumiwa kwa sera zake, sio maneno yake, na kwa kipimo hiki, inafeli vibaya ambapo haijawahi kuonekana.

2. Vita dhidi ya ugaidi (WOT) daima vimekuwa vita dhidi ya Uislamu, vikitumia vita dhidi ya ugaidi kama barakoa kuficha hamu ya nchi za Magharibi ya kuwatenganisha Waislamu kutokana na matakwa yao ya kimfumo, kisiasa na kiitikadi. Kiini cha WOT siku zote kimekuwa ni kuondoa siasa, kuingiza usekula na kuusambaratisha mwili wa Kiislamu.

3. Maneno ya Leba kuhusu Uislamu na Waislamu ni ishara tupu zinazofunika sera zake za kupinga Uislamu. Huku ikipeleka hadharani na mara kwa mara wapambe wake wa Kiislamu tangu kushika wadhifa, serikali ya Leba imekuwa ikijishughulisha na watu faraghani ikipanga njia za kupanua udhibiti wake juu ya jamii na kutenganisha na kuharamisha zaidi kanuni muhimu za imani ya Kiislamu.

4. Jaribio la kupiga marufuku bendera inayotumiwa na "IS" ni mgeuko mbaya zaidi, na kuashiria sifa kwa ubora zaidi. Inaifanya jamii ya Kiislamu na jumuiya pana zaidi kuwa limbukeni kwa kupunguza vita dhidi vya ugaidi kuwa nembo, badala ya kuendeleza mazungumzo ya wazi na ya uaminifu kuhusu matokeo ya uingiliaji kati wa Magharibi duniani kote.

5. Bendera inayotumiwa na ‘IS’ ina maneno na picha zinazopendwa na kila Muislamu. Utumiwaji shirika wa maneno haya na upande wowote haupunguzi umuhimu wake katika Uislamu, wala tishio la kutiwa hatiani kwa kujihusisha nayo halitaondoa utakatifu wake kwa Waislamu.

At-Tirmidhi na Ibn Majah wamesimulia kutoka kwa Ibn Abbas aliyesema«كَانَتْ رَايَةُ رَسُولِ اللهِ ﷺ سَوْدَاءَ وَلِوَاؤُهُ أَبْيَضَ» Bendera ya Rayah ya Mtume Mohammad (saw) ili ni nyeusi, na bendera yake ya Liwaa ilikuwa ni nyeupe.

Na katika riwaya nyengine kutoka kwa Ibn Abbas (ra): «كَانَ مَكْتُوبًا عَلَى رَايَتِهِ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ مُحَمَّدٌ رَسُولُ اللَّهِ» Iliandikwa katika bendera yake (saw): La Ilaha Illa Allah, Muhammad Rasul-Allah”.

6. Jamii ya Kiislamu haitakubali kamwe kwa serikali yoyote kuamuru ni mambo gani ya Uislamu yanakubalika na ni mambo gani yanapaswa kuharamishwa, na tunakataa kwa nguvu zote jaribio lolote la kulazimisha mamlaka kama hayo juu ya mambo yetu ya kidini.

7. Kinaya cha jaribio hili la hivi punde la kuingilia maeneo ya Waislamu haipaswi kupotea kwa mtu yeyote. Ikiwa tunatazamia kuharamisha nembo, basi kwa hakika tutakuwa tunatazamia kuharamisha bendera ambayo uingiliaji kati wa wakoloni wa Magharibi daima umetokea na unaendelea kutokea, nazo ni msalaba na Union Jack.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu