Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  30 Muharram 1446 Na: 03 / 1446 H
M.  Jumatatu, 05 Agosti 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kama Umma Mmoja: Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa Kuangamizwa kwa Dhalimu Hasina na Tunawaombea Kuporomoka Madhalimu Wote Wanaoukandamiza Ummah

(Imetafsiriwa)

Baada ya majuma kadhaa ya ukandamizaji wa kikatili dhidi ya watu wa Bangladesh na dhalimu Hasina, genge la serikali yake, na wachungaji wake wa kigeni, alilazimishwa kidhalilifu kuikimbia nchi. Waislamu shupavu wa Bangladesh, wakiongozwa na wanafunzi jasiri, walivumilia ukatili usio na kifani na hatimaye kulazimisha kuondolewa kwake kupitia wimbi lisilozuilika la maandamano ambayo yalimshinda dikteta huyo.

Waislamu wa Bangladesh kwa mara nyingine tena wameangazia uwezo mkubwa ndani ya ummah, wakionyesha hatima isiyoepukika inayowangojea madhalimu wanaowafanyia ukatili raia wao. Ingawa huu ni ushindi wa aina yake, ummah lazima uzingatie mafunzo ya matukio kama hayo katika nchi kama Misri na Sudan. Misimamo ya kikoloni inaenea ndani kabisa ya rasilimali za ummah, ikinyakua kwa ujanja ushindi kwa kuwatupilia mbali madhalimu vibaraka wao pindi kufaa kwao kunapokwisha, ila kuwabadilisha tu kwa watu ambao uaminifu wao unabakia mapajani mwa dola za kigeni na zenye uadui.

Umma lazima uhakikishe kwamba rasilimali zake, kama vile majeshi, zinabakia chini ya udhibiti wake ili kwamba matakwa ya uadilifu wa kweli kwa wote—yanayojumuishwa tu ndani ya mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt)—yaweze kuasisiwa kwa uhuru kamili na umma wa Muhammad (saw).

Tunawapongeza Waislamu wa Bangladesh kwa subira na ustahimilivu wao, na tunaomba dua kwamba Mwenyezi Mungu (swt) awakubali mashahidi wengi na huu uwe ndio mwanzo wa mwamko mkubwa kwa Waislamu wa Bangladesh katika kusimamisha rehma na uadilifu wa Uislamu kwa watu wote.

[وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Quran 14:42]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu