Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  16 Rabi' II 1442 Na: H 1442 / 11
M.  Jumanne, 01 Disemba 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pingeni Mbinu Chafu za Serikali ya Hasina za Kuficha Ufisadi wao, Utawala Mbaya na Mateso ya Watu kupitia Kuchochea Utata wa 'Kinyago Dhidi ya Sanamu'

Wakati bei ya mpunga iliyochumwa kwa kazi ngumu ya wakulima wanyonge ikiwa imeshuka kwa kiwango kisicho cha kawaida, bei zinazoongezeka za mahitaji yote ya kila siku ikiwemo mchele, viazi, mboga zinaleta mateso makubwa kwa watu, wafanyikazi wanapinga sera za kirasilimali za serikali kufunga viwanda vya makonge na sukari vinavyosababisha ukosefu wa ajira ulioenea, mustakabali wa wanafunzi hauna uhakika kwa sababu ya kufungwa kwa taasisi za elimu, pesa za umma zinasambazwa miongoni mwa warasilimali kwa jina la vishajiisho kupitia kuzibakisha hai siasa za virusi vya Korona, hofu iliyozidi inaundwa kwa jina ya wimbi la pili la virusi vya Korona ili kuwafanya watu kuwa waathiriwa wa biashara ya chanjo ya dolari milioni ya wafanyabiashara wafisadi, na maandamano dhidi ya ufisadi wa serikali yanalipuka, serikali ya Hasina inachochea moto wa mabishano kati ya kinyago na sanamu ili kuficha utawala wao mbaya na kushindwa kulinda riziki za watu. Kwa kuongezea, ingawa wasomi wa kiulimwengu daima ni wachangamfu dhidi ya sera za serikali na ufisadi, lakini wakati huu serikali imewajumuisha kwa ujanja katika vita dhidi ya Waislamu wanaopinga sanamu au kinyago.

Enyi watu, bila shaka, kuchonga 'sanamu au kinyago' sehemu ya umma ni 'munkar' na nidhamu ya kisekula ndio 'Ummul munkar' (mama wa uovu wote). Watawala wa kisekula daima wamekuwa wakikataa uwepo wa Muumba katika maswala ya maisha na Serikali na kuchukua ubwana na utakatifu wa Muumba kwao wenyewe. Matokeo yake, watawala wa kisekula huwaabudu viongozi wao wakuu na kulazimisha sura zao na sanamu zao kwa watu kwa kuzitungika mahakamani, maafisini na sehemu za umma, na kuwalazimisha wawaabudu kwa njia isiyo ya moja kwa moja. Mfano mzuri wa hili ni Wasovieti ambao walikana uwepo wa Mungu, waliwatukuza Lenin na Stalin na maneno na taarifa zao kwa njia ile ile tunayotukuza Quran na Hadith. Walikita masanamu makubwa kote nchini kujumuisha haya na kuzionyesha picha zao kwa lazima katika afisi zote za serikali na za umma. Vivyo hivyo, hapa pia unaona kwamba serikali ya sasa ya kisekula imeamuru kwamba ofisi zote za serikali na za umma lazima zionyeshe picha za Sheikh Mujib na Sheikh Hasina. Kitendo hiki cha utakuzaji kitakuwa wazi endapo tutazitazama sheria za kikafiri za nchi hii - kifungo cha juu cha miaka kumi kwa kukashifu dini yoyote, lakini kifungo cha juu cha maisha kwa kumchafulia jina Sheikh Mujib au Sheikh Hasina! Bila ya kutosheka na hili, sasa wamechukua hatua ya kuweka sanamu za Sheikh Mujib kote nchini. Machoni mwa Uislamu, vitendo hivi ni Jahiliyyat (ujinga), haramu kabisa na kinyume na 'Imaan. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[ذَلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ]

“Huyo ndiye Allah, Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu, hapana mungu ila Yeye, Muumba wa kila kitu. Basi muabuduni Yeye tu. Naye ni Mtegemewa wa kila kitu.” [Surah Al-An’am-102]. Kwa hivyo, hakuna wigo wa kuhalalisha shughuli hizi kupitia kutoa mifano ya sheria katika dola zengine za kisekula za Waislamu.

Enyi watu, serikali ya kisekula ya Hasina inatumia mbinu mbali mbali za kuficha ufisadi na mateso yao kwa watu, na wamekuwa wakichochea maswala tofauti, moja baada ya jingine, ili kuwapurukusheni kutokana nao. Mumeshuhudia jinsi katika nidhamu ya kisekula ya serikali hii tawala fisidifu inavyolinda maslahi yao wenyewe, kipote cha warasilimali na wakoloni wa makafiri, wakipora rasilimali za watu, na kukandamiza umati mkubwa. Mtume (saw) amesema,

«الإمام راع ومسؤول عن رعيته»

"Khalifa (imam) ni mchungaji na ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake". Kwa hivyo, bila kupoteza muda wenu katika mijadala ya sanamu au kinyago, takeni nukta moja ya kusimamishwa tena kwa Dola ya Khilafah kupitia kuiondoa serikali ya sasa ya kisekula na nidhamu wa kisekula ya kikafiri. Kwa mujibu wa ahadi ya RasulAllah (saw), Khilafah itasimamishwa hivi karibuni na unyanyasaji wote utatokomezwa kutoka kwa serikali na jamii milele:

«ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“kisha atauondoa (utawala wa kiimla) pendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” [Musnad Ahmad].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu