Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  23 Jumada II 1442 Na: 1442 H / 16
M.  Ijumaa, 05 Februari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Al Jazeera Haijafichua Chochote Kipya kuhusu ‘Serikali ya Kijambazi ya Hasina;

Kile Ambacho Vyombo vya Habari Vinapaswa Kufichua ni Demokrasia ya Kirasilimali – Mazingira Mwanana ya Majambazi kama Hao

(Imetafsiriwa)

Kitengo cha Upelelezi cha mtandao wa Al Jazeera kimedai kufichua ufisadi mkubwa wa kisiasa wa serikali ya Hasina kupitia msururu wa rekodi za siri ("Wanaume wote wa Waziri Mkuu", aljazeera.com, 1 Februari 2021). Makala hayo yalifichua jinsi mtandao wa magenge yalio karibu na Waziri Mkuu Hasina unavyoshirikiana na vikosi vya usalama na vikosi vya kijeshi vya Bangladesh kuwateka nyara wapinzani na kuchuma mamilioni ya rushwa kwa ubadilishanaji wa kandarasi za serikali. Makala hiyo yalirekodi filamu kwa siri za ndugu mkuu wa sasa wa Jeshi la Bangladesh waliopatikana na hatia wakikiri kutumia kikosi mashuhuri cha Rapid Action Battalion (RAB) na polisi kwa ajili ya ulinzi wao wenyewe na kuwa "majambazi" wao.

Ukweli wa mambo ni kwamba habari hizi za ufisadi wa kisiasa na utawala wa genge la Hasina sio jambo la kushangaza kwa watu nchini Bangladesh. Huku ukweli ni ukiwa siri hizi zilizofichuka, jaribio la 'kuzifichua' sio jambo geni, na sababu pekee ya msukosuko katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni kwa sababu vyombo vya habari vya ndani ya nchi "vilivyo fungwa mdomo" haviwezi hata kutaja majina haya au shughuli hizi. Jukumu halisi la vyombo vya habari linapaswa kuwa kuwajulisha watu yale ambayo hawajui na kuwaelekeza mielekeo sahihi wakati watu wanapokuwa kwenye shida. Lakini, sio Al Jazeera wala vyombo vyetu vikuu vya habari ndani ya nchi vimefichua wapangaji halisi wa uhalifu huu, Wakoloni wa Kimagharibi, ambao wanaendelea kutoa msaada kwa serikali ya kihalifu ya Hasina. Kwa kuwa ni sehemu muhimu ya hadhara ya Kirasilimali ya Kimagharibi, vyombo hivi vya habari kamwe havitawafichua Wakoloni na ajenda zao ovu. Wakoloni hawa wameendelea kuunda mazingira ya kisiasa ya nchi zote za Kiislamu tangu kuvunjwa kwa Khilafah mnamo 1924. Wamekuwa wakizilazimisha serikali za kihalifu kama Ligi ya Awami na BNP kuendeleza na utawala wao katika nchi zetu. Pindi serikali moja wa kihalifu inapoteza uaminifu na watu kujitahidi kuing'oa, vyombo vikuu vya habari hupata sifa kwa kuidhalilisha serikali hiyo. Hutoa njia tu kwa serikali nyengine ya kihalifu kwa njia hii ili kuficha mfumo fisadi wa Kirasilimali unaounda na kudumisha wahalifu hawa. Kwa hivyo, ikiwa vyombo vya habari hivi vinadai kuwa viaminifu na vya kweli, vinapaswa kuwafichua wahalifu hawa wakuu wa Kikoloni. Lazima vitoe wito kwa watu kupambana na ubabe wa kimagharibi kupitia kuachana na Demokrasia yao iliyooza ya Kirasilimali, shina la uovu wote.

Enyi Maafisa wenye ikhlasi katika Jeshi la Bangladesh! Mnawezaje kuishi maisha ya heshima na uadilifu wakati mnampa uongozi kiongozi wenu mafia na majenerali wengine wasaliti? Wapo kuwatumikia wakoloni makafiri pekee kwa kuwalinda vibaraka wao katika nchi zetu. Wakoloni watauweka hai uongozi huu wa kijambazi wa kiraia na wa kijeshi ili tu kuhakikisha utawala wao. Wanaiua roho yenu ya kuulinda Umma kwa kukupelekeni pia kwenye uchochoro wa giza wa ufisadi na vitisho, kama vile walivyofanya kwa jeshi la polisi. Maafisa wenzenu wengi ambao hapo awali walikuwa waaminifu sasa wamekuwa mafuasi sugu wa (RAB) waliovaa mavazi meusi wa serikali hii ya kijambazi. Kila siku inayopita, mnapoteza imani mbele ya Umma kwa dori yenu nyumbani na ng'ambo. Serikali hii umewasukuma kufanya urafiki na adui jirani Mshirikina India, ambayo ilikuwa nyuma ya mauaji ya ndugu zenu huko Pilkhana. Wamewafanya kuwa kikosi cha mamluki kwa ajili ya wakoloni kupigana vita vyao katika kile kinachoitwa Misheni za Kulinda Amani za UN. Wanawageuza kwa utaratibu kuwa vyombo vya rushwa vya serikali ili watu waanze kuwachukia. Pia, wanaichana roho yenu ya kutekeleza Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuwafanyeni jeshi la utumwa la Magharibi

Enyi Maafisa! Zingatieni wito wa Hizb ut Tahrir. Ujira mnaopokea sasa kwa utiifu wenu kwa maadui hawa wa Mwenyezi Mungu (swt), itakuwa ni njia ya udhalilifu mkubwa na mateso mbele ya Mwenyezi Mungu Al-Haseeb (Mhasibu) siku ya Kiyama. Je! Hakuna yeyote kati yenu anayeweza kusema 'inatosha' na kuwatupa majambazi hawa kwenye jaa la historia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu? Unganisheni mikono yenu na chama cha kweli cha Hizb ut Tahrir na muipe usaidizi wenu wa kimada (Nusrah) ili kuing'oa Demokrasia ya Kirasilimali inayoungwa mkono na Magharibi kutoka kwa ardhi yetu milele na kusimamisha tena Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

  [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

"Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele." [Surah Al-Anfaal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu