Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  21 Sha'aban 1443 Na: 1443 H / 16
M.  Alhamisi, 24 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kampeni ya Uzushi ya Mashirika ya Haki za Wanawake ya kuunganisha kwa uongo Ubaguzi na Unyanyasaji wa Wanawake na Sheria ya Mirathi ya Kiislamu ni Kuondoa Mabaki Yoyote Yaliyosalia ya Hukmu za Uislamu katika Jamii.

 (Imetafsiriwa)

Mnamo Machi 10, 2022, Bangladesh Nari Pragati Sangha (BNPS), shirika la ndani la haki za wanawake, limedai marekebisho ya sheria zilizopo za familia na kutunga sheria mpya nchini Bangladesh ili kuhakikisha haki sawa kwa wanawake katika urithi na mali ya familia. Katika tukio hilo, walitoa hasira zao kwa Uislamu kwa kusema hakuna sheria ya kiraia au jinai nchini inayodhibitiwa na dini isipokuwa sheria ya mirathi. Hawa wanaojiita wanaharakati na masekula wapagani wanatetea kwamba ili kukomesha ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake ni lazima hali yao ya kiuchumi iimarishwe kwa kuhakikisha haki sawa kwa rasilimali na mali zote zikiwemo mirathi. Wanaharakati hawa wadanganyifu na duni wanaounga mkono Magharibi hawana wasiwasi kamwe kuhusu haki za kimsingi za watu, ilhali hawaachi juhudi zozote za kuuhujumu Uislamu huku wakijaribu kwa uongo kuunganisha ubaguzi na unyanyasaji unaoendelea wa wanawake na sheria za Kiislamu. Wako kwenye dhamira ya kupiga vita mabaki yoyote ya hukmu za Uislamu katika maisha yetu kwa kuzibadilisha na sheria za Magharibi kafiri kwa nia ya kuwafanya Waislamu wa Bangladesh kuwa masekula. Hivyo, wanaongoza kampeni kama hizo za kashfa dhidi ya Uislamu kwa kuutaja kuwa ni adui wa wanawake. Wanajua kabisa kuwa sheria iliyopo ya mirathi sio sababu ya ubaguzi na ukandamizaji dhidi ya wanawake. Bali ni mfumo wa utawala wa kisekula ambao huleta taabu katika maisha ya wanawake. Je, sheria ya mirathi ya Kiislamu ndiyo sababu ya ufyatulianaji risasi unaohusishwa na uzazi na ubaguzi mwingine wa kijinsia sehemu za kazi nchini Bangladesh? Je, tumeona yeyote kati ya wanaharakati hawa wasio na thamani wakiihesabu serikali kwa mateso yote ya hivi majuzi yasiyovumilika ya wanawake waliokusanyika kununua bidhaa za kampuni ya Trading Corporation of Bangladesh (TCB) na kutopata chochote hata baada ya kusimama kwenye foleni ndefu kwa masaa mingi? Je, unyonyaji wa wanawake wetu katika viwanda vya nguo kwa ajili ya kuwaongezea faida Mabepari walafi unawabughudhi?

Ukweli wa mambo ni kwamba hadhara ya Kimagharibi inawapeleka wanawake katika dimbwi la giza kwa jina la ‘usawa’ na ‘uwezeshwaji’. Lakini je, hadhara ya Magharibi yenyewe imepata mafanikio yoyote kwa wazo lake la kile kinachoitwa ‘usawa’? Wamewapotosha wanawake wao kwa dhana potovu kwamba familia, uzazi, na ndoa za kitamaduni ni sababu kuu za ukandamizaji wa wanawake ambao wanahitaji 'kukombolewa' kutoka kwao. Hii imesababisha migogoro kati ya wanaume na wanawake katika maisha yao ya ndoa na majukumu ya wazazi ambayo imesababisha zaidi kusambaratika kwa familia katika nchi za Magharibi na hatimaye kuharibu familia zao na muundo wa kijamii. Hatimaye, ‘usawa’ wa Magharibi umeongeza mizigo ya wanawake na majukumu ya wanaume na kuwasukuma katika mzunguko usio na mwisho wa shida na mateso. Wanawake wao sasa wanahujumu familia ya kiasili na thamani kuu ya uzazi vilevile, kwa hivyo hadhara ya Kimagharibi inateseka kutokana na kupoteza kizazi. Kwa hakika, hadhara ya Kimagharibi ‘imewakomboa’ wanawake lakini kwa kuwageuza vyombo vya ngono, na kuwatumia wanawake kuendeleza ajenda zao za kisiasa. Na sasa yale yanayoitwa makundi ya haki za wanawake yanafanya kazi bila kuchoka ili kupandikiza mawazo yaliyooza na maadili ya Urasilimali wa Kimagharibi katika jamii yetu ili kuleta maafa kwa wanawake, watoto na muundo wa familia zetu. Baada ya kushindwa kuchafua akili za Waislamu kwa mawazo yao fisidifu na batili ya kiliberali, mashirika haya ya udhia sasa yanajaribu kufanya mapambano ya kisheria.

Enyi Watu! Hakuna anayeweza kukataa kwamba wanawake wanavumilia mateso makali siku hizi. Sio sheria ya mirathi ya Kiislamu bali kukosekana kutabikishwa Uislamu kwa ukamilifu wake kupitia mfumo wa Dola ya Khilafah ambako kunaleta madhara na taabu kwa wanawake. Ama kuhusu urathi, kuna hali 34 zinazoweza kutokea za urathi miongoni mwa jamaa katika sheria ya Kiislamu. Kati ya hizo, mwanamke hurithi sehemu sawa na mwanamume katika hali 11, na katika hali 4 pekee ndizo mwanamke hupokea nusu ya hisa ya mwanamume. Katika hali nyengine 14, mwanamke hurithi hisa zaidi ya mwanamume. Hivi ndivyo Uislamu ulivyoonekana kuwa rehma kwa wanawake na ukahakikisha haki zao katika urithi. Umar ibn al-Khattab (ra) amesema: "Wallahi katika Jahiliyyah, hatukuwajali wanawake mpaka Mwenyezi Mungu (swt) alipoteremsha yanayohusiana nao yale yaliyoteremshwa, na akawagawia aliyoyagawa."

Uislamu unatoa dira sahihi ili kuinua hadhi ya wanawake ambao wanacheza dori muhimu ya kuleta utulivu katika familia na nyumba. Kwa kueleza kwa uwazi ukweli kwamba wanaume na wanawake hawafanani kwa maumbile na sifa zao, Uislamu unapanga dori, haki, na majukumu yao kwa namna ambayo watakamilishana ili kuhakikisha utulivu wa kijamii. Wanawake chini ya Uislamu watapata elimu, kujihusisha na biashara, na kufaulu katika maeneo yao ya taaluma. Wanaweza kushika wadhifa wowote wa Serikali isipokuwa ule wa kutawala. Moja ya haki muhimu sana ambazo wanawake wa Kiislamu wangepata ni haki yao ya kujihusisha na kazi za kisiasa na kujadili mambo ya Ummah kuwa mjumbe wa Baraza la Ummah. Umar bin Al-Khattab (ra), Khalifa wa pili wa Uislamu, angeshauriana na Al-Shifa binti Abdullah juu ya masuala mbalimbali ya kisiasa kutokana na akili na utambuzi wake, na mara nyingi alipendelea maoni yake kuliko wengine. Kwa hivyo, wanawake kama hao waliowezeshwa kikweli wanaweza kuhakikishwa tu kwa kutabikisha mfumo wa Kiislamu wa kisiasa, kiuchumi, kielimu, na kimahakama chini ya nidhamu ya utawala ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kupitia utabikishaji huu mpana wa mfumo wa Kiislamu, Khilafah itarudisha hadhi na heshima wanayostahiki wanawake. Kwa sababu Khilafah inayokaribia sio tu kwamba itatekeleza baadhi ya sheria bali pia itatoa mtazamo wa maisha kwa wanaume na wanawake ambao utaifanya hadhara ya Kiislamu kuwa ya kipekee na yenye nuru. Mwenyezi Mungu Subhana wa Ta’la asema,

[وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنْ الْمُنكَرِ وَيُقِيمُونَ الصَّلاَةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَيُطِيعُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَئِكَ سَيَرْحَمُهُمُ اللَّهُ إِنَّ اللَّهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ]

"Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu, na hushika Sala, na hutoa Zaka, na humt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao Mwenyezi Mungu atawarehemu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hikima." [Surah At-Taubah: 71].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu