Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 14 Muharram 1444 | Na: 1444 H / 02 |
M. Ijumaa, 12 Agosti 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir/ Wilayah Bangladesh iliandaa Maandamano dhidi ya Ongezeko Lisilo na Kifani na la Kitatili la Bei ya Mafuta Lililofanywa na Serikali kwa Ushirikiano na IMF
(Imetafsiriwa)
Leo Ijumaa (Agosti 11, 2022) baada ya swala ya Ijumaa Hizb ut Tahrir/ Wilayah Bangladesh iliandaa mikusanyiko ya maandamano katika majengo ya misikiti mbalimbali jijini Dhaka na Chittagong, chini ya kichwa: “Kwa Ushirikiano na IMF, Serikali bila huruma imeongeza Bei ya Mafuta; Ukombozi wetu kutokana na Kutawaliwa Kiuchumi na Dola za Kimagharibi za Kikafiri unawezekana tu chini ya Khilafah”. Wazungumzaji katika mkusanyiko huo walieleza jinsi taasisi za Kimagharibi kama vile IMF na Benki ya Dunia zilivyozitia nchi za ulimwengu wa tatu, zikiwemo za Kiislamu, ndani ya mtego wa madeni, zikiangamiza msingi wa uchumi wa nchi, kuzifanya zitegemee kikamilifu nchi za kigeni, na kuwaruhusu mabepari wa kigeni kulimbikiza utajiri mkubwa. Hapo awali, wazungumzaji walifichua uwongo na hadaa kwamba serikali iliamua kupandisha bei ya mafuta, wakitoa sababu kama vile kupanda kwa bei katika soko la kimataifa, hasara za serikali au ulanguzi wa mafuta hadi India, ili kuficha suala la njama hizo za IMF.
Kisha wazungumzaji walifichua sera za IMF kwa kusema: Taasisi hatari inayojulikana sana ya Kirasilimali IMF daima huchukua fursa ya kulazimisha ajenda ya Ukoloni na sera ya Kirasilimali ya ubinafsishaji iliyo lemaza uchumi wetu, hasa sekta yetu ya nishati. Kwa kufuata sera ya IMF, tawala zote za kilimwengu mtawalia kamwe hazijawahi kuwekeza katika kampuni ya utafiti wa mafuta ya serikali (BAPEX) na kuruhusu makampuni ya kigeni ya Kikoloni kama vile Chevron, ConocoPhillips, nk, kupora madini yetu ya gesi na mafuta chini ya Mkataba wa Ushirika wa Uzalishaji (PSC). Walikabidhi sekta ya uzalishaji umeme kwa makampuni ya kigeni yenye uchu (kama vile Palli Biddut inayomilikiwa na kampuni ya Marekani) na makampuni ya ndani (kama vile Summit Group). Zamani Wakoloni wangevamia ardhi hizo kwa ajili ya maliasili na madini. Lakini sasa katika ‘ulimwengu huru’ wa leo, taasisi kama vile IMF na WB wakishirikiana na watawala vibaraka wasaliti hupora rasilimali za nchi na kulemaza ubwana wao wa nishati ili waendelee kuwa tegemezi kwa huruma ya Makafiri. Kwa hivyo, tunaona kwamba kipote cha mabwenyenye na watawala wafisadi wanaoungwa mkono na Magharibi wanajitajirisha katika sekta ya nishati kupitia mpango muovu wa ubinafsishaji wa IMF ilhali watu wa kawaida wanabeba ushuru wa bei inayoongezeka ya mafuta. Hivyo basi, kimaumbile, IMF haishinikizi serikali kuacha kutoa ‘malipo ya kawi’ kwa kipote cha Mabepari wachache, bali inalazimisha kuondoa kile kinachoitwa ruzuku kwenye mafuta jambo ambalo linafanya maisha kuwa magumu kwa raia. Haya yote yanapaswa kuwa funzo tosha kwetu sisi Waislamu kwamba maendeleo na ustawi kamwe hauwezi kupatikana kupitia kutegemea IMF au mfumo wowote wa kirasilimali au mfumo au dola iliobuniwa na mwanadamu, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyotukumbusha ndani ya Qur’an:
(مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاءَ كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتًا وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنْكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ)
“Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Al-Ankabut: 41].
Hatimaye wasemaji walisema: Enyi Watu, lazima mulinganie kusimamisha tena Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume iliyo ahidiwa kwa sababu ni Khilafah pekee ndiyo inayoweza kuwatoa watu katika masaibu haya. Khilafah haitakuwa na haja ya kuweka ruzuku katika sekta ya nishati kwa kuwa nishati na madini ni katika kigawanyo cha ‘mali ya umma’ chini ya Uislamu; watu watapata hizi moja kwa moja kwa gharama ya chini au bila malipo. Itapangilia uchumi wake kulingana na maagizo ya Sharia na haitaruhusu wakoloni au taasisi zao kama IMF au Benki ya Dunia kuingilia kati maswala ya kiuchumi ya Dola. Khalifah kamwe hatazigeukia taasisi hizi za kibeberu kuinusuru kwa sababu Khilafah kamwe haitatoa nafasi kwa mfumo wa fedha wa dolari usio na thamani ya kidhati. Uchumi utajengwa juu ya bidhaa na huduma halisi na sarafu itaegemezwa juu ya dhahabu na fedha. Kwa hivyo, hakutakuwa na mfumko wa bei kama huu au kuongezeka kwa ghafla kwa bei ya bidhaa msingi.
Mfumo wa Kirasilimali umetufikisha kwenye ukingo wa maangamivu, umetufanya tuwe na madeni kwa dola za Kimagharibi na kuleta mateso kwa watu. Lakini ikiwa hatutamtegemea yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt), Yeye (swt) anaahidi kutufungulia njia ya kutoka katika matatizo haya:
(فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَى)
“basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.” [Taha: 123].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |