Alhamisi, 11 Sha'aban 1445 | 2024/02/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  4 Rabi' II 1444 Na: 1444 H / 10
M.  Jumamosi, 29 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Onyo la Hasina na Mshauri wake wa Kawi kuhusu Baa la Njaa na Ukosefu wa Umeme linaonyesha kuwa Serikali yake inafilisika pamoja na Sera za Benki ya Dunia IMF

(Imetafsiriwa)

Mara baada ya Sheikh Hasina kuwataka wananchi wajiandae kwa matumizi ya taa za kandili-karabai, ndipo mshauri wake wa masuala ya kawi Taufiq-e-Elahi akawashauri watu wachukue ahadi ya kutotumia umeme mchana. Baada ya kupeleka uzalishaji wa viwanda na kilimo ukingoni mwa kuporomoka pamoja na mateso makubwa ya watu wa kawaida kutokana na ‘kukatizwa kwa umeme’, washauri wake wa kejeli na mawaziri sasa wanawaomba wananchi kuziokoa sekta hizi. Ni dhahiri kwamba sekta ya umeme imeporomoka kwa kasi kutokana na ufisadi wa serikali yake na sera ya kukabidhi uzalishaji wa umeme kwa washirika wa Kibepari. Wanasiasa wa kisekula, wasomi, na wanauchumi wamedanganyika sana kupata kiungo cha mgogoro huu wa kawi ambao ni matokeo ya sera za ukoloni mamboleo za WB-IMF. Tangu miaka ya 80, Benki ya Dunia (WB) na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) zilitekeleza "Makubaliano ya Washington" nchini Bangladesh na zimefungua mlango wa uporaji wa sekta zetu za kawi na Mabepari wa hali ya juu kupitia programu kubwa za ubinafsishaji. 'Mkataba wa Kugawanya Uzalishaji' wa WB (PSC) umehakikisha kuwa sehemu kubwa ya rasilimali zetu za kawi iko mikononi mwa nchi adui, kama vile Chevron ya Marekani, ONGC Videsh ya India nk. Kwa hivyo, mamlaka yetu ya kawi daima bado iko hatarini na katika rehema ya Magharibi kafiri. Tangu mwaka wa 1987, tumesalimisha maeneo yetu ya mafuta na gesi kwa dola za Wakoloni moja baada ya nyengine badala ya kujaribu kujenga uwezo wetu wa kuvinjari kawi katika nchi kavu na baharini. Tunanunua kawi yetu wenyewe kutoka kwa makampuni ya kigeni kwa dolari za Marekani kwa bei za kimataifa. Sera hizi zimefanya sekta yetu ya kawi kulemazwa ingawa tumejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi za kawi asilia. Uingiliaji kati wa ukoloni mamboleo umezidisha mgogoro wetu wa kiuchumi na kawi na kutuacha katika matatizo makubwa. Kwa upande mmoja, serikali inatii maagizo ya Wakoloni ya kupunguza utoaji wa gesi chafuzi licha ya kuwa Bangladesh ni mtoaji mdogo sana wa gesi hiyo na hivyo kupuuza akiba yetu ya ndani ya makaa ya mawe na teknolojia safi ya makaa ya mawe kwa ajili ya uzalishaji wa umeme (“John Kerry anaisifu Bangladesh kwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, mipango ya kuhafifisha”, Dhaka Tribune, 23 Oktoba 2022), lakini kwa upande mwingine, wanaagiza makaa ya mawe ghali kila mwaka ili kutimiza maslahi ya wafanyibiashara! Zaidi ya hayo, serikali pia iko tayari kulipa mara nne kwa kampuni ya Adani ya India kwa kawi ya makaa ya mawe ya gharama kubwa ambapo ilitangaza kukata ruzuku ya chakula kwa maskini kwa karibu dolari milioni 100 kuonyesha kisingizio cha kupanda kwa gharama za mafuta duniani.

‘Mafanikio’ ya ajabu ya serikali ya Hasina ni ufujaji wa mali ya watu na ulanguzi wa fedha za nchi kupitia upatilizaji matumizi ya sera za WB-IMF za kufungua biashara na uwekezaji wa kigeni, kudhibiti shughuli za kiuchumi, na kubinafsisha mashirika ya serikali. Sera zao za kubadilisha uchumi wetu ambao kwa kiasi kikubwa ulijitosheleza kwa chakula kuwa waagizaji wa vyakula wa kudumu zimeharibu sekta yetu ya kilimo. Kwa kufuata sera hizi za kujiua za WB-IMF na kuhatarisha usalama wetu wa chakula, Hasina sasa anawaonya wananchi kuhusu baa la njaa linalo wakodolea macho! Mbali na hilo, serikali hii ya kisekula ya kirasilimali  imeizamisha nchi nzima ndani ya deni la nje ili tu kutumikia maslahi ya kipote cha mabwenyenye, na sasa inawaomba wananchi wawe tayari kwa mgogoro unaokuja wa akiba na kufilisika kwani haitaweza kulipa bili za maduhuli ya mahitaji katika miezi ijayo. Wanajaribu kuficha ukweli kwamba ndani ya mwaka jana wakati akiba ya Dolari za Kimarekani bilioni 10 zilipungua (kutoka Dolari Bilioni 46 hadi Bilioni 36), serikali yao imewezesha ukopaji mkubwa kutoka nje wa kipote cha Mabepari wa ndani ambao umeruka hadi Dolari za Kimarekani Bilioni 17 kutoka dolari bilioni 11 (sharebiz.net, 25 Oktoba 2022). Hivi sasa wajumbe wa IMF wako nchini Bangladesh na watakaa jijini Dhaka hadi Novemba 9 huku kukiwa na hofu inayoongezeka juu ya akiba ya fedha za kigeni na deni la umma. Wameanzisha mazungumzo na serikali ili kupunguza ruzuku na vishajiisho ambazo zitafanya maisha ya watu wa kawaida kuwa duni. Wanachojali tu ni kuadhibu umati kupitia kukaza kanda za fedha, maarufu kama "mipango ya kupunguza matumizi ya umma" na sera za kukomboa masoko ambazo zitaifanya miguu ya Mabepari kuwa imara zaidi. Tutaona watu wengi wakiathirika zaidi na kushuka kwa mapato halisi na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kutokana na "vifurushi vyao vya uokozi". Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ بَدَّلُواْ نِعْمَةَ اللّهِ كُفْرًا وَأَحَلُّواْ قَوْمَهُمْ دَارَ الْبَوَارِ]

“Hebu hukuwaona wale walio badilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo?” [Surah Ibrahim: 28].

Enyi Waislamu, je, bado mutawatumainia watawala hawa wasaliti, bado mutawaomba umeme, na bado mutategemea kwamba wataleta unafuu kwenye riziki yenu? Je, bado mutawatazama ili mupate njia ya kutokea, ingawa hamuna shaka kwamba watawala hao watumwa ni mikuki ya Wakoloni makafiri ambao mfumo wao angamivu wa Kirasilimali unageuza ustawi wetu kuwa taabu bila kuchoka? Badala yake, munapaswa kudai mara moja kutoka kwa maafisa wa dhati wa jeshi kuondoa uungaji mkono wao kutoka kwa watawala hawa vibaraka. Wakumbushe kwamba watawala hawa wanafurahia uhuru huo wa kuharibu maisha na riziki zetu kwa kupitia tu kupanda migongoni mwao. Watakeni ‘Nusrah’ yao (msaada wa kimada) kwa ajili ya chama chenye ikhlasi na shupavu cha Hizb ut Tahrir. Kwa sababu ni chama hiki pekee ndicho kimeeleza kwa uwazi jinsi kitakavyo chukua jukumu kwa ajili ya watu kwa kutabikisha Hukmu za Shariah kwa ukamilifu chini ya mfumo wa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hakuna nafasi ya ubwenyenye ndani ya Uislamu na chini ya Khilafah hakutakuwa na wigo wa kukabidhi maliasili za umma kwa makampuni ya ndani na nje ya nchi. Raia chini ya Dola ya Khilafah, bila ya kujali rangi na dini zao, watakuwa wanufaikaji wakuu wa maliasili na madini. Na tofauti na mfumo wa kisekula wa Ubepari, Khilafah inayokaribia itaangalia usimamizi wa sekta hii ya kawi kwa niaba ya raia wake na kutoa haki sawa kwa rasilimali hizi. Khilafah haitaruhusu kundi lolote kuzigeuza neema hizi za Mwenyezi Mungu kuwa taabu kwa jina la ubinafsishaji. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُواْ وَاتَّقَواْ لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاء وَالأَرْضِ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Surah Al A’raf: 96].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu