Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
H. 28 Jumada II 1444 | Na: 1444 H / 17 |
M. Jumamosi, 21 Januari 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ziara ya Donald Lu nchini Bangladesh Inafichua Sura ya Halisi ya Demokrasia na Urithi wa Watawala wa Kisekula wa Utiifu kwa Mabwana wa Kikoloni
(Imetafsiriwa)
Ndani ya wiki moja ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Marekani kwa Asia Kusini, Admiral Eileen Laubacher, afisa mwengine wa ngazi ya juu wa Marekani Donald Lu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Asia ya Kusini na Kati, alitembelea Bangladesh kwa siku mbili kuanzia Januari 14 hadi Januari 15. Lu alikuwa na mikutano mingi na maafisa wakuu wa serikali na wawakilishi wa 'mashirika ya kiraia' na kujadili masuala mbalimbali tofauti ikiwemo uchaguzi ujao, haki za binadamu, demokrasia, usalama, na masuala mengine ya nchi hizi mbili na ya kikanda. Lakini kati ya haya, Mkakati wa Indo-Pasifiki (IPS) na mikataba miovu ya ulinzi ya Marekani - Mkataba Mkuu wa Usalama wa Taarifa za Kijeshi (GSOMIA) na Mkataba wa Upataji wa Huduma Mtambuka (ACSA) - yalitawala mikutano hiyo kutokana na kuongezeka kwa maslahi ya stratejia ya kieneo ya Marekani katika Ghuba ya Bengal. (“Momen, Lu kujadili IPS, masuala mengine huko Padma leo”, The Bangladesh Observer, 15 Januari, 2023). Wakati huu kulikuwa na onyesho lisilokuwa na aibu la utumishi wa kisiasa kuelekea Amerika wakati wa ziara ya Lu. Vyama vya upinzani ambavyo viko chini ya dhulma ya serikali vilifurahishwa na ujio wa 'mwokozi wao Amerika'. Walikuwa na furaha kwamba ujumbe mkali wa Lu kwa serikali ya Hasina ungehakikisha uchaguzi huru, wa haki na jumuishi. Wanahisi kuwa wanastahili vyema kuwa madarakani kutumikia maslahi ya Marekani. Kwa upande mwingine, serikali ya kitumwa ya Hasina ilikuwa imejiandaa kikamilifu na kazi zao za ziada pia ili kuifurahisha Amerika. Ili kulinda kiti chake cha enzi, serikali ilisema mara moja kabla ya ziara ya Lu kwamba Bangladesh haikuwa na shida kujiunga na jukwaa la Indo Pasifiki la Amerika (Daily Jugantor, Januari 14, 2023). Pia, kama mtumishi mtiifu, Waziri wake wa Mambo ya Nje alikuwa akijivunia kumsambazia Lu taarifa mpya jinsi walivyokuwa wakitekeleza sehemu yao kwa mafanikio katika Vita vya Marekani dhidi ya Uislamu kwa kisingizio cha kupambana na wanamgambo na misimamo mikali ya Kiislamu.
Enyi Watu, mnachoshuhudia ndio sura ya halisi ya demokrasia ambayo Amerika inaikuza katika nchi za Kiislamu. Watawala wa kisekula na wanasiasa watiifu katika ardhi zetu ni sehemu ya demokrasia hii. Huu ndio ‘uhuru’ ambao Marekani inausafirisha kwa nchi nyingine ‘huru’ ambapo wanasiasa duni na wapole wanasubiri kwa hamu uingiliaji kati wa bwana wao (Marekani). Na watawala wanalazimishwa kukubali matakwa ya Marekani ya kubaki madarakani. Enyi Watu, Watawala hawa wa kisekula na wanasiasa wanasalimisha ubwana na rasilimali za Ummah kwa mkoloni Kafiri kwa kuhusika katika mbio hizi za panya zisizo na mwisho za madaraka. Mazingira ya kisiasa yaliyojikita katika ziara ya Donald Lu yalithibitisha mpango halisi wa demokrasia katika ardhi yetu, ambayo si chochote ila utawala wa Marekani katika mfumo wa IPS, ACSA na GSOMIA. Na kwa jina la 'haki za binadamu' na 'demokrasia', Amerika ya Kikoloni inapeleka zana za kulazimisha kuishinikiza Bangladesh kwa maslahi yake ya kijiografia. Ukombozi wa Waislamu kutokana na ukandamizaji wa ksekula na taabu ni jambo lisilofaa katika demokrasia ya Marekani. Umma huu mtukufu kamwe haustahiki kutawaliwa chini ya watawala vibaraka wasaliti kama hao wa kisekula. Waislamu lazima wajitahidi kwa ajili ya mfumo mpya wa dunia chini ya kivuli cha Khilafah Rashida iliyoahidiwa kwa njia ya Utume ambayo itawatoa kwenye giza hili la magharibi hadi kwenye nuru. Na Mwenyezi Mungu ‘Azza wa Jal anaahidi hilo ndani ya Quran,
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An-Noor 24:55]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Bangladesh |
Address & Website Tel: +88 01798 367 640 www.ht-bangladesh.info |
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd |