Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  16 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 1444 H / 26
M.  Jumatatu, 05 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bajeti ya Kibepari ni Njia ya Uporaji wa Kinidhamu wa Pesa za Umma Kufadhili Uporaji na Ufujaji wa Kupangiliwa

(Imetafsiriwa)

Mnamo Juni 1, 2023, serikali ya Hasina ilizindua bajeti ya kitaifa inayoitwa "Kuelekea Bangladesh ya kijanja inayofuata maendeleo" kwa mwaka wa fedha wa 2023-24. Waziri wa Fedha AHM Mustafa Kamal aliweka bajeti ya Taka trilioni 7.6 ambayo ni asilimia 13.5 kubwa kuliko FY 23 yenye mwelekeo 'unaotarajiwa' wa kukabiliana na mfumko wa bei, kuzalisha ajira, na juhudi kuelekea 'Bangladesh ya Kijanja' kwa kushughulikia changamoto za mapinduzi ya nne ya viwanda yenye miradi mipya 40. Bajeti hii bado ni njia nyingine ya udanganyifu ya serikali hii ya Kibepari kushawishi uchaguzi ujao kwa kutumia uongo na ahadi za uongo.Waziri Kamal alisema bungeni kuwa lengo la bajeti hiyo ni kushughulikia matatizo ya watu waliotelekezwa na kuinua kiwango cha maisha yao zaidi kutoka katika hadhi ya sasa. Kiuhalisia tayari serikali imeshamomonyoa jumla ya kiwango cha maisha ya watu kwa kutumia Benki ya Bangladesh (BB) kuingiza Taka bilioni 700 pesa mpya katika mzunguko katika mwaka wa sasa wa fedha ili kusaidia matumizi yake ya bajeti ambayo yamesababisha shinikizo la mfumko wa bei. Kwa bajeti hii ijayo, imeweka tena lengo la kukopa Taka bilioni 1323.95 kutoka kwa mfumo wa benki ili kufidia nakisi yake ambayo itazidisha hali ya mfumko wa bei. Zaidi ya hayo, mgogoro wa gharama ya maisha ya watu utazidishwa zaidi kwani serikali inajipanga kuufurahisha Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF), ambao umeongeza mkopo wa dolari bilioni 4.7 dhidi ya hali ngumu zinazo athiri watu. Ili kutekeleza sharti la IMF la kukusanya mapato, serikali imeweka shabaha ya Taka trilioni 4.3 na kutangaza kuegemea zaidi katika kutesa watu kwa kodi ya moja kwa moja na kodi isiyo ya moja kwa moja (VAT) na kutoa ruzuku badala ya kukomesha uporaji, ufisadi na ulanguzi wa fedha unaofanywa na kipote cha mabwenyenye na watu wenye ushawishi. Watu tayari wanateseka kutokana na kile kinachoitwa miradi mikubwa ya umeme iliyopo ambayo imesababisha deni la dolari bilioni 2 kwa mwaka. Watu watatozwa kodi zaidi na zaidi ili kulipia riba za mikopo ya nje inayochukuliwa kwa ajili ya miradi mbalimbali mikubwa ya ‘maendeleo’ na malipo ya kiwango cha umeme wa IPPs ingawa upunguzaji wa shehena ya umeme unaoendelea nchini kote unafanya maisha ya watu kuwa ya dhiki. Kwa upande mmoja, waongo hawa wadanganyifu wanasema kwamba wanaongeza kiwango cha juu cha msamaha wa ushuru kwa Taka 350,000 kutoka Taka 300,000 ili kuwapa watu faraja, ambapo kwa upande mwingine wanatoza ushuru wa mapato wa Taka 2000 hata kama wanapata chini ya Taka 350,000. kwa mwaka. Zaidi ya hayo, kwa kusitisha usambazaji wa gesi asilia majumbani na kulazimisha watu kutumia gesi ya LP, sasa serikali katili ya Kibepari inaondoa msamaha wa ushuru wa bidhaa kutoka nje kwa mitungi ya LPG na kuongeza VAT (kutoka 5% hadi 7%) katika hatua ya uzalishaji wa ndani ili kuongeza mapato. Na sasa makampuni ya gesi ya LP kimaumbile yatahamisha mzigo huu begani kwa watu wa kawaida kupitia kuongeza bei ya gesi huku kukiwa na mgogoro mkubwa unaoendelea wa gharama ya maisha.

Enyi Watu! Utawala huu wa kibepari wa kisekula hautaacha kuwaibia watu maskini pesa za zilizochumwa kwa taabu kupitia njia ya ushuru wa kinyonyaji kwa jina la kupanga bajeti na kuzitumia kwa maslahi ya kipote cha mabepari na wanasiasa hadi tutakapoung'oa mfumo huu wa kibepari wa kisekula uliojengwa kwa hiari tu ya wanadamu. Tumekuwa wahanga wa dhiki na hali hii ya kudhalilisha kutokana na kuondolewa kwa Uislamu na mfumo wake wa kiuchumi katika medani ya maisha na kushikamana na mfumo wa urasilimali uliotungwa na mwanadamu. Kwa kuongozwa na hawaa zao wenyewe, tabaka tawala la mfumo huu halina wasiwasi wowote kuhusu kuweka hatua za kuwaadhibu watu kama vile kuweka programu za kubana matumizi au mizigo ya kodi. Haitoshi kupuuza tu bajeti za kirasilimali isipokuwa ung'oe mfumo wa Ubepari vile vile na badala yake uweke mtindo wa kiuchumi wa kimfumo wa Kiislamu chini ya kivuli cha Khilafah Rashida wa pili kwa njia ya Utume. Uislamu una mtazamo wa kipekee wa kiuchumi unaohakikisha mapato ya juu kwa dola bila kuwalemea wananchi. Kwa mujibu wa kanuni za fedha za umma za serikali ya Khilafah, Dola ya Khilafah haitategemea utozaji ushuru kwenye mapato na matumizi ya watu kama chanzo cha mapato. Katika Uislamu, mali ya watu binafsi ina utukufu na dola ya Khilafah haiwezi kuwapora raia wake kwa kisingizio cha "utozaji ushuru". Haiwaadhibu maskini na wasiojiweza ambao hawawezi kupata mahitaji yao ya kimsingi. Sekta za mapato na matumizi katika bajeti ya Dola ya Khilafah huamuliwa na hukmu za kudumu za Sharia. Al-Ghana'im (ngawira za kivita), Kharaj

(kodi ya ardhi), Fai (ngawira zisizo za vita) kutoka nchi mpya zinazoingia chini ya Khilafah, ushuru wa Jizya kutoka kwa wanaume wasiokuwa Waislamu wenye uwezo, mapato kutokana na mali inayomilikiwa na umma (mafuta, gesi, umeme, rasilimali za madini, malisho, mifereji, chemchemi, ardhi iliyohifadhiwa au Hima), mapato yatokanayo na sadaqah (ushr kutokana na mazao ya kilimo, zakat ya fedha taslimu, biashara ya bidhaa na mifugo) na kwa kutoza ushuru wa ziada ya utajiri wa matajiri ili tu kukidhi mahitaji maalum, Dola ya Khilafah itazalisha mapato makubwa. Muundo wa kipekee wa kampuni wa Uislamu unaweka kikomo uwezo wa kifedha wa makampuni binafsi kutawala viwanda vikubwa vya kuzalisha mapato na mitaji ya uchumi kama vile usafiri mkubwa, mawasiliano ya simu na ujenzi. Hivyo basi, Dola ya Khilafah kwa kawaida ingekuwa na nafasi kubwa katika sekta hizi ambazo zingeweza kuzalisha mapato ya kutosha kuangalia mambo ya wananchi. Kando na hayo, Dola ya Khilafah itazalisha mapato yanayohitajika kutoka kwa sekta na viwanda mbalimbali vinavyohusiana na mali za umma na zinazomilikiwa na serikali kama vile viwanda vya hali ya juu vya elektroniki na viwanda vya kutengeneza magari. Mapato yatokanayo na mali zinazomilikiwa na umma pamoja na taasisi zinazomilikiwa na dola yanatunzwa katika hazina ya serikali (Baitul Mal) na kutumika kwa ajili ya ustawi wa raia wote bila kujali rangi na dini kwa kuzingatia rai na ijtihadi ya Khalifa. Uzalishaji mkubwa wa mapato kama haya kutoka kwa rasilimali za Dola na za umma chini ya usimamizi wa karibu wa Dola utahakikisha kuongezeka kwa ugavi wa mali hiyo badala ya urundikaji wake kama inavyotokea katika mfumo wa Kirasilimali.

Zaidi ya hayo, Uislamu umeharamisha deni linalotokana na riba iwe katika mfumo wa bondi za hazina za ndani au mikopo ya nje. Kwa kufunga mlango wa mzunguko wa kiharibifu wa madeni kutoka kwa taasisi za kikoloni, Dola ya Khilafah itaukomboa uchumi wetu kutoka kwa utawala wa makafiri wa kikoloni. Matokeo yake, uhuru wetu wa kiuchumi utaregeshwa. Mwenyezi Mungu Subhana Wa Ta’la asema:

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنْ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Al-Araf: 96].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu