Jumatano, 04 Rabi' al-awwal 1442 | 2020/10/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  21 Jumada I 1441 Na: 1441 H / 011
M.  Alhamisi, 16 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuhamisha Nidhamu ya Usimamizi wa Usambazaji wa Maji kwa Kampuni binafsi huko Purbachal ni Madhara Makubwa na Usaliti wa Uaminifu

Baada ya kuwapisha njia mabepari wafisadi kupora pesa za umma katika sekta ya umeme, serikali ya Hasina sasa imeamua kukabidhi usimamizi wa usambazaji wa maji katika mji mpya wa Purbachal kwa kampuni binafsi ambayo lengo lake ni kupata faida tu, sio kulinda watumiaji. Na hili linafanyika kote kwa jina la “kuleta ufanisi” katika sekta hii. Chini ya mpangilio huu mpya, muungano binafsi unaojumuisha Kampuni ya United Water (Suqian) ya Uchina na Delcot Water ya Bangladesh zita weka mtandao wa usambazaji wa takriban kilomita 320 kando ya barabara zinazofika kila ardhi katika mradi huo (Daily Star, Januari 09, 2020). Ili kuhalalisha mpango wa ubinafsishaji wa taasisi ya wakoloni IMF (Shirika la Fedha la Kimataifa), serikali hii ya kinafiki imezama chini sana kiasi ya kwamba hata haihisi aibu kujidhihirisha kuwa ‘haiwezi’ kuendesha nidhamu rahisi wa usimamizi wa maji. Ukosefu huu wa kutekeleza huduma ya msingi ya matumizi kwa umma umefunua asili ya kweli ya kinachojulikana kama 'muujiza wa maendeleo' ambao serikali hii inajivunia. Matokeo ya haraka ya ubinafsishaji wa usimamizi wa rasilimali hii ya kawaida yatakuwa ‘kuongezeka kwa bei’ kwani kampuni binafsi zitatia faida wakati wa kusambaza kwa watu wa kawaida. Kwa hivyo, watumiaji watalazimika kubeba mzigo wa malipo ya juu kwa mikopo ambayo hii kampuni binafsi itachukua kwa oparesheni zake ambazo ni pamoja na riba, ushuru na gharama za juu kwenye mtaji. Juu ya hayo, serikali hii inayopingwa na watu imekubali kutoa kiwango cha Tk 56 crore kila mwaka katika marekebisho ambacho kitaporwa kutoka katika mifuko ya watu.

Enyi Watu wa Bangladesh, uhalifu wa serikali ya Hasina unaendelea pasina kusita na tunasukumwa katika hali ngumu za maisha kila kukicha. Baada ya kupoteza kiasi kikubwa cha fedha za umma kwa kupendelea kampuni za kibepari katika sekta ya umeme, sasa iko tayari kutekeleza uhalifu mwingine katika sekta ya usimamizi wa maji ambao utatuletea shida zaidi kwetu. Ukweli wa mambo ni kuwa ‘ukuaji na maendeleo bandia’ ni simulizi ya serikali hii inayopumua pumzi zake za mwisho pamoja na majanga makubwa ya fedha. Kwa hivyo, kuvutia mikopo zaidi kutoka katika taasisi za kikoloni kama vile IMF, serikali ya Hasina inatekeleza miradi yake ya kubinafsisha rasilimali za umma ambayo haijawahi kunufaisha taifa lolote maskini, badala yake inaharibu kabisa uchumi wake tangu serikali hizo kulipisha kodi zaidi kwa watu ili kulipa mikopo hiyo. Dhulma hii na mateso hayatasimama ikiwa bado tunashuhudia kimya kimya utawala wa kibepari wa kidemokrasia na kukubali shida ambazo miradi hii ya IMF inazileta.

Khilafah ya Uongofu inayokaribia itahakikisha kwamba rasilimali za maji hazitochukuliwa kama ‘bidhaa’, badala yake ni ‘haki’ ya raia ambayo imewekwa na Shari’ah. Nidhamu ya Uchumi ya Kiislamu itavunja mara moja mikataba yote kama hiyo inayopingwa na watu pamoja na kampuni binafsi na kuchukua jukumu la kusimamia mali za umma na serikali kwa misingi ya ‘hukmu za kishari’ah’ kwa kuwa Uislamu hauruhusu kupeana umiliki wa rasilimali za umma kwa chama chochote cha kibinafsi kwani rasilimali hizi ni za umma. Mjumbe wa Mwenyezi (saw) amesema,

«الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ فِي الْكَلَإِ وَالْمَاءِ وَالنَّارِ»

“Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto (kawi).” [Abu Dawood]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu