Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  8 Muharram 1446 Na: H 1446 / 01
M.  Jumapili, 14 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utawala wa Hasina kwa Kutumikia Uingereza, Unashiriki katika Vita vya Wakala ili Kulinda Utawala wa Junta wa Myanmar unaoungwa mkono na Uingereza ambao uliua Waislamu wa Rohingya

(Imetafsiriwa)

Mamia ya wanajeshi wa Kikosi cha Walinzi wa Mipaka ya Myanmar (BGP) na Jeshi kwa mara nyengine tena wanakimbilia Bangladesh kwa makaazi salama kutokana na mapigano makali yanayoendelea kati ya kundi la waasi la Arakan Army na junta ya kijeshi ya Myanmar huko Rakhine [Dainik Janakantha, Julai 12, 2024]. Utawala wa Hasina unalijaza tena jeshi la serikali ya junta kwa kuwarudisha wanajeshi wauaji ambao wanakimbia kila mara. Kwa sababu hiyo, vikosi vya wauaji (ambao mikono yao imetapakaa damu ya Waislamu wa Rohingya) wanatumia ardhi yetu kama “eneo la kuzuia" kuwakandamiza waasi. Kwa kuongezea, meli tatu za kivita zilizosheheni silaha nzito na makombora ya chokaa zimewekwa katika bahari ya Bangladesh karibu na St. Martin, kupigana na Jeshi la Arakan ambalo ni muungano wa makabila yenye silaha nchini humo, na milio ya risasi nzito na makombora ya kurushwa kutoka meli hizi zimesababisha hofu kote kisiwani [Daily Us Time, Juni 14, 2924]. Kijana, Ali Johar, alipigwa risasi iliyofyatuliwa kutoka Myanmar alipokuwa akirejea kutoka Kisiwa cha St. Martin kwenye trela [Yamuna TV, Juni 13, 2024]. Juni 16, 2024 taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Inter-Services Public Relations (ISPR), Bangladesh ilisema kuwa, “jeshi la Myanmar linaendesha operesheni ya pamoja dhidi ya Jeshi la Arakan katika Jimbo la Rakhine kwa kuzingatia mzozo wa ndani unaoendelea nchini Myanmar. Mapigano haya kati ya jeshi la Myanmar na Jeshi la Arakan yalisababisha kurusha risasi kiholela kwenye boti za Bangladesh katika mpaka wa Mto Naf na maeneo ya mito.” Katika hali hiyo, serikali ilikatisha usafiri wote wa kuelekea bara na kisiwa muhimu cha St. Martin na kuwazuia wakazi wa kisiwa hicho, badala ya kupeleka vikosi vya kijeshi katika eneo la bahari jirani, ikiwa ni pamoja na St. Martin, ili kuhakikisha usalama wa umma. Kwa hiyo, kuna upungufu mkubwa wa chakula pamoja na dawa. Kwa hakika, serikali iliunda hali hii ili kuunda eneo la uslama kwa jeshi la wanamaji la serikali ya junta kukandamiza vikundi vya waasi wenye silaha wa Myanmar. Ikikosolewa na wataalam wa kijeshi na usalama, serikali ilituma jeshi la wanamaji na walinzi wa pwani kwa jina moja la kufuatilia mwenendo wa meli za Myanmar, na kusababisha kisiwa cha St. Martin kutengwa na harakati za kawaida za watu kutoregeshwa. Kwa hivyo, Hasina katika utumishi wa bwana wake Uingereza, amehusika katika vita vya wakala kulinda utawala wa junta unaoungwa mkono na Uingereza (ulioua Waislamu wa Rohingya), na kuusaliti Umma wa Kiislamu.

Enyi Watu! Kama mulivyoona hapo awali, utawala wa Hasina uliwarudisha Waislamu wa Rohingya waliokimbia makaazi yao kutokana na vita vya ndani, lakini haukuwarudisha Wanajeshi wa BGP (wauaji wa Waislamu) waliokimbia kutoka Myanmar wakishambuliwa na waasi. Kwa kuwachukulia kama wafungwa wa vita kwa mujibu wa ushauri wa wachambuzi wa masuala ya usalama na kile kinachoitwa sheria ya kimataifa, utawala wa Hasina haukuweka shinikizo kwa utawala wa kijeshi kuwaregesha makwao Waislamu wa Rohingya, bali ulikaribisha jeshi hilo la mauaji kwa maua. Na bila kuchelewa kuwarudisha nchini mwao kusaidia kujaza Jeshi la serikali ya junta. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قَاتِلُوا الَّذِينَ يَلُونَكُمْ مِنَ الْكُفَّارِ وَلْيَجِدُوا فِيكُمْ غِلْظَةً وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ]

“Enyi mlio amini! Piganeni na wale makafiri walio karibu yenu, na wakute ugumu kwenu. Na jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu yu pamoja na wacha- Mungu.” [Surah At-Tawbah: 123]. Kwa hivyo, serikali ya Hasina, katika kuihudumia Uingereza, inausaidia utawala wa junta unaoungwa mkono na Uingereza na kukiuka ubwana wan chi hii na kutelekeza maslahi ya ndugu na dada zetu Waislamu wa Rohingya.

Enyi Watu, mnajua kwamba utawala wa junta nchini Myanmar unaoungwa mkono na Uingereza kuwafurusha halaiki ya Waislamu wa Rohingya wa jimbo la Arakan, kimpangilio umekuwa ukishambulia kwa miongo mingi kwa kuunda mizozo ya kidini ya makasisi wa Kibudha, kuteketeza majumba, kuwauwa wanaume wa Rohingya, kuwachinja Watoto, kuwabaka wanawake, kupora na kuua. Na serikali ya Hasina inaulinda utawala wa junta wa Myanmar kutokana na upinzani wao kwa kuwafungia mamilioni ya Waislamu wa Rohingya kwa jina la kutafuta hifadhi. Kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu (swt), mabudha hao wajinga sasa wanahusika katika mizozo ya kikabila na wamenaswa ndani ya mtego wa mkakati wa siasa za kieneo wa Marekani.

[وَمَا أَصَابَكُمْ مِنْ مُصِيبَةٍ فَبِمَا كَسَبَتْ أَيْدِيكُمْ وَيَعْفُو عَنْ كَثِيرٍ]

“Na misiba inayo kusibuni ni kwa sababu ya vitendo vya mikono yenu. Naye anasamehe mengi.” [Ash-Shura: 30]. Na kwa sababu ya mzozo wa maslahi wa makafiri na pia hasira za watu, kiti cha utawala cha msaliti Hasina kiko ukingoni mwa kuporomoka.

Enyi Watu! Mwenyezi Mungu (swt) anaharamisha kukabidhi uhai na mali ya watu wa nchi hii kwa watawala hawa wajinga, «وَلَا تُؤْتُوا السُّفَهَاءَ أَمْوَالَكُمُ الَّتِي جَعَلَ اللَّهُ لَكُمْ قِيَامًا» “Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu.” [Surah An-Nisa: 5]. Na pendekezo la kuanzisha uhusiano na Jeshi la Arakan na kundi la vibaraka wa Marekani la BNP litaendeleza pakubwa maslahi ya siasa za kieneo ya Marekani. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam (Khalifa) ni ngao watu hupigana yake na hujihami kwake” (Sahih Muslim). Njia pekee ya kuhifadhi ubwana wa nchii hii na kurekebisha hali ya Waislamu wa Rohingya ni kuiunganisha tena Arakan na ardhi yetu. Hivyo basi, ni lazima mara moja musonge katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir na muwatake imara maafisa wa jeshi kuipa nusra (nguvu) Hizb ut Tahrir kwa ajili ya lengo hili.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu