Jumapili, 26 Rajab 1446 | 2025/01/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  24 Rabi' I 1446 Na: H 1446 / 15
M.  Ijumaa, 27 Septemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ukatili wa Kiyahudi unaweza tu Kukomeshwa kwa Kuivunja Mipaka ya Mgawanyiko ya Dola za Kitaifa na kuyaleta Majeshi ya Kiislamu chini ya Bendera ya Shahada ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, leo (27/09/2024) iliandaa maandamano na matembezi ya kulaani katika majengo ya misikiti tofauti ya Dhaka na Chittagong kupinga mashambulizi ya kuendelea dhidi ya Palestina na Lebanon yanayofanywa na umbile haramu la Kiyahudi. Wanachama mbalimbali wa Hizb ut Tahrir walitoa hotuba katika mikusanyiko baada ya maandamano ambayo yalitembea katika barabara mbalimbali za maeneo tofauti tofauti ya mji, na kuhitimishwa kwa Du’a. Mukhtasari wa hotuba za wazungumzaji kwenye mikusanyiko hiyo umewasilishwa hapa chini:

Imepita takriban mwaka mmoja lakini umbile hilo haramu la Kiyahudi bado linaendelea na mauaji ya halaiki dhidi ya watu wa Gaza na Ukingo wa Magharibi mbele ya masikio na macho ya ulimwengu. Idadi ya mashahidi wetu tayari imezidi 40,000 na waliojeruhiwa inakaribia 100,000 katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Pasi na dalili za kukomesha mauaji haya ya kila siku ya watoto, wanawake na wazee wasio na hatia, umbile hilo haramu sasa limehamia kwenye kampeni nyingine kubwa ya ulipuaji wa mabomu kote nchini Lebanon, tayari limeua mamia ya watu na kuwahamisha zaidi ya 90,000. Hospitali za Lebanon zimejaa raia wasio na hatia, wakiwemo makumi ya wanawake na watoto, sawa na tunavyoona nchini Palestina.

Enyi Waislamu, tusiwe chini ya dhana yoyote potofu kwamba ‘Israel’ ni nguvu isiyoweza kuguswa na isiyozuilika. Badala yake, kipande hiki kidogo cha umbile lisilo na maana ilikuwa ni kiumbe cha Magharibi ili kiwe ni wakala wa ubeberu wao katika Mashariki ya Kati na kwengineko. Kwa hivyo, linapokea dhahiri uungwaji mkono wa kijeshi na wa kifedha usio na kifani kutoka kwa ulimwengu mnafiki na mapuuza wa Magharibi. Ili kulinda kiumbe chao haramu, Magharibi inayoongozwa na Marekani ikiwa ni pamoja na chombo chao cha kibeberu UN haijali hata kuua maadili yao wenyewe kama vile ‘uhuru’ na ‘haki za binadamu’, ambazo wanazieneza kidini katika ardhi za Waislamu kwa ajili ya ghiliba za kisiasa pekee.

Tunataka kukumbusheni kwamba kikwazo pekee cha kukomesha kabisa vita vya msalaba dhidi ya Waislamu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ni watawala vibaraka wa ardhi za Waislamu. Wasaliti hawa ndio walinzi wa mstari wa mbele wa umbile haramu la Kiyahudi. Huku watoto wetu wasio na hatia wakifa kwa njaa kutokana na mzingiro wa Wazayuni kuzuia usambazaji wa chakula, watawala wa vibaraka nchini Misri, Jordan, Morocco na UAE wanaendelea kusafirisha bidhaa za chakula kwa umbile la Kiyahudi. Watawala hawa wanaimarisha umbile hili la mauaji kupitia mikataba yao ya amani, kuhalalisha mahusiano, mahusiano ya kidiplomasia, na ushirikiano wa kiuchumi. Hao ndio wanaofanya kazi kama walinzi wa mipaka bandia ya dola za kitaifa iliyowekwa na wakoloni hawa juu yetu. Ili kutumikia ajenda ya Magharibi, wanatufanya tugawanyike na kutuzuia kusonga mbele kuwanusuru ndugu na dada zetu wanaokandamizwa nchini Palestina na sehemu zengine za ulimwengu. Kwa kulinda mipaka hii ya kitaifa iliyowekwa na Magharibi, vibaraka hawa wa Magharibi wanataka kuyafanya masaibu ya Waislamu wa Palestina kuwa tatizo la ‘Wapalestina, sio la Umma. Wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliuelezea Ummah kuwa ni mwili mmoja, na inapotokea sehemu yoyote yake inaumia, mwili mzima hujibu kwa kukosa usingizi na homa.

Enyi Waislamu, Hizb ut Tahrir haitachoka kukumbusheni kwamba njia pekee ya kuikomboa ardhi iliyobarikiwa ya Palestina kutokana na uchafu wa Mayahudi waliolaaniwa ni kusimamisha tena Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ni lazima muwatake maafisa wanyoofu wa majeshi wavunje mipaka batili ya migawanyiko ya uzalendo iliyowekewa na wakoloni, wawapindue watawala hawa waoga wasaliti kutoka katika ardhi zetu, na kutoa nusrah (msaada wa mada) kwa Hizb ut Tahrir ili kurudisha mara moja mfumo wa Uislamu - ulioahidiwa Khilafah ya pili. Kando na hili, njia nyengine zote zitakushusheni kwenye shimo la udhalilifu na fedheha duniani na Akhera.

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [An-Nisa: 75]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu