Jumanne, 08 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  26 Rabi' II 1446 Na: H 1446 / 21
M.  Jumanne, 29 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kwa Kuifuta Katiba ya ‘72 na Msingi wake, Usekula, Watu wameungana katika Kuendesha Nchi Kwa Msingi wa Katiba ya Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Jumanne iliyopita (Oktoba 22, 2024), vuguvugu la wanafunzi la kupinga ubaguzi lilitaka kubatilishwa mara moja kwa katiba ya 1972 na kutangazwa kwa ‘Tangazo la Jamhuri’ kwa nia ya Mapinduzi ya Julai na uasi mkubwa. Kwa ajili hiyo, kwa kuviita tu vyama vinavyoitwa vya kidemokrasia kuunda umoja wa kitaifa, wamepuuza matakwa na matarajio ya watu wa nchi hii ya utawala wa Kiislamu. Kama munavyopaswa kujua, katika uchunguzi uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Marekani Pew Research Center, asilimia 82 ya Waislamu nchini Bangladesh wanapendelea Shari'ah. Taifa zima limeshuhudia kwamba wanafunzi wa shule-vyuo-vyuo vikuu-maarufu wameibua matakwa ya utawala wa Kiislamu. Wameonyesha hisia zao kwa kubeba bendera ya Kalima mikononi mwao; kwa hivyo, jaribio lolote la kusuluhisha siasa za nchi kwa kupuuza Uislamu ni hatua ya kujiua. Kwa hakika, kama tunavyojua sote, kupinga kuibuka kwa utawala wa Shari'ah katika ardhi za Kiislamu ndiyo sera ya msingi ya “vita dhidi ya Uislamu” vya Magharibi kwa jina la “vita dhidi ya ugaidi”. Utawala wa Hasina uliong'olewa madarakani, ulifanya kazi kama chombo cha nchi za Magharibi kuendesha “vita dhidi ya Uislamu,” ulichukua msimamo dhidi ya idadi kubwa ya watu wa nchi hii na kuwakandamiza Waislamu wa nchi hii, na hii ni moja ya sababu kuu za uasi wa wananchi dhidi ya utawala wa Hasina. Kwa hiyo, hatuna budi kuifutilia mbali katiba ya 1972 na msingi wa katiba hiyo, yaani, usekula kutoka kwa jamii na serikali yetu, na kuungana kwa msingi wa Uislamu, kwa sababu, usekula na demokrasia ni kinyume na imani, fikra na hisia za watu na ndio chimbuko la ubaguzi, ufisadi na uonevu wote.

Amerika imejigamba kama watetezi wa demokrasia na haki za binadamu, lakini kauli mbiu za watu wake zinazochochea ‘sisi ni 99%’ na 'maisha ya watu weusi ndio yanajalisha’ zimethibitisha kwamba mfumo wa Kidemokrasia-Kibepari ni wa kibaguzi na umefeli. Na Uingereza, nchi nyingine ya kiliberali ya kidemokrasia, imezama katika migawanyiko ya kijamii na mgogoro wa kisiasa kiasi kwamba hakuna kati ya serikali zao inayoweza kumaliza muda wake. Kwa hivyo, ikiwa katiba mpya itaandikwa kwa njia ya Amerika na Uingereza, je ubaguzi utaondolewa vipi katika jamii na serikali? Je, katiba hii itatimiza vipi matarajio ya wananchi? Mwenyezi Mungu (swt) anatutahadharisha kuhusu wale Waislamu wanaowaendea Makafiri wa Magharibi licha ya suluhisho la kila kitu kuwa katika Uislamu:

[أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُوا بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِنْ قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَنْ يَتَحَاكَمُوا إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُوا أَنْ يَكْفُرُوا بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا]

“Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali.” [Surah an-Nisa': 60].

Je, ni ipi Bangladesh mpya ambayo watu wanataka kuiona? Watu hawatakubali katiba ambayo haitatimiza matakwa yao na kamwe hawataungana chini ya katiba hiyo. Umma kwa jumla unataka maisha ya utulivu, haki adilifu, usalama, na haki kutoka kwa sheria. Vijana wanataka ajira na mustakabali salama. Wafanyikazi wanataka mishahara yao ya haki. Watu wenye ufahamu wanataka watawala ambao sio vibaraka wa nchi ya kigeni na sio mafisadi, na nchi huru isiyo na uvamizi na ushawishi wa kigeni. Madai haya ya wananchi yameonekana katika harakati na mapambano mbalimbali. Katika miongo mitano iliyopita, kumekuwa na mavuguvugu mbalimbali nchini Bangladesh, mageuzi kumi na saba ya katiba, mabadiliko katika nyuso za tabaka tawala, maendeleo ya kipodizi, lakini hakuna hata moja ya matarajio ya wananchi ambayo yametimizwa. Katiba ya Kiislamu imehakikisha kwa wote, bila kujali dini-rangi-kabila, mahitaji msingi yaani makao-mavazi-chakula cha kila raia pamoja na haki zao yaani elimu-afya-usalama na haki. Katiba ya Kiislamu imeharamisha ubinafsishaji wa sekta ya nishati ya gesi ya nchi na kuamuru kufukuzwa makampuni ya kibepari ya ndani na nje kutoka katika sekta hii ya nishati, na kuamuru mali hizo zitumike kama mali ya umma kwa ustawi wa umma chini ya usimamizi wa serikali. Imepiga marufuku mikataba yote na nchi adui kama vile Marekani-Uingereza-India, ikijumuisha mikataba ya kijeshi ambayo inatutawala. Uislamu uliamuru kuimarisha jeshi ili kulinda mamlaka ya nchi kwa kuanzisha viwanda vizito vyenye mwelekeo wa ulinzi. Kwa hiyo, katiba ya Kiislamu pekee ndiyo yenye uwezo wa kutimiza matakwa ya watu. Kuhusiana na hili, Hizb ut Tahrir imewasilisha “Katiba (Rasimu) ya Dola ya Khilafah” yenye maelezo ya kina ambayo imetungwa kwa kuzingatia Quran-Sunnah. Zaidi ya yote, wananchi wameungana katika kuitawala nchi kwa katiba ya Kiislamu, na Hizb ut Tahrir imejitayarisha kikamilifu kuitawala nchi kwa katiba hii.

Enyi Watu, hasa Wanafunzi-Raia Wanamapinduzi! Kataeni jaribio lolote la kuhifadhi mwendelezo wa mfumo wa kibepari wa kisekula uliofeli wa Magharibi kwa kufanya mabadiliko fulani ya kivipodozi kwa jina la marekebisho ya katiba au kuiandika upya. Lazima muimarishe matakwa ya katiba ya Kiislamu na mfumo wa Kiislamu. Unganeni chini ya uongozi wa Hizb ut Tahrir katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, na mutoe wito kwa watu wenye madaraka wahamishie mamlaka kwa Hizb ut Tahrir ili kutimiza matarajio ya watu.

[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu …” [Surah Ali-Imran: 110].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu