Alhamisi, 22 Muharram 1447 | 2025/07/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  18 Muharram 1447 Na: H 1447 / 03
M.  Jumapili, 13 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mauaji ya Kikatili ya Sohag katika eneo la Midford la Mji Mkuu Dhaka, ni Matokeo Yasiyoepukika ya Siasa za Kisekula na za Kiwendawazimu zisizomtambua Mungu

(Imetafsiriwa)

Katika eneo la Mitford la mji mkongwe wa Dhaka, baadhi ya viongozi wa eneo la Jubo Dal, wakiongozwa na chama kikuu cha kisekula cha kisiasa nchini humu BNP, walimuua kikatili mfanyibiashara wa vyuma vichakavu aitwaye Sohag (39) kwa kumdunga kisu na kumpiga na jiwe kubwa mfululizo kwa kukataa kulipa pesa za ulaghai. Walioshuhudia walisema kwamba wahalifu hao hawakuishia kumuua tu, bali waliendelea kuonyesha unyama kwenye mwili mfu wa Sohag hata baada ya kifo chake kuthibitishwa. Mwili uliojaa damu, ulioganda uliachwa katikati ya barabara na wauaji wakasimama juu ya mwili huo huku wakisherehekea kiwendawazimu.

Sio mmoja, lakini wauaji kadhaa waliendelea kupiga pua, mdomo na kifua cha maiti hiyo. Aina hizi za mauaji na wazimu zimekuwa matukio ya kila siku chini ya mwavuli wa siasa za kisekula kwa miongo kadhaa. Mauaji ya Sohag yatakuwa mfano mwingine kwa watu kuamka kwa haraka dhidi ya siasa za kisekula. Chama kikuu cha siasa za kisekula-Awami League kilikuwa kimeweka mifano mingi ya wazimu wakati wa miaka kumi na tano iliyopita ya utawala chini ya uongozi wa Hasina aliyeanguka, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kikatili ya Biswajit na Abrar Fahad.

Kwa sasa, BNP tayari imeweza kuweka mifano ya kutosha ya kufuata nyayo za Hasina. Kwa sababu, njia kuu za maisha ya siasa hizi za kisekula iliyobuniwa na nchi za Magharibi ni pesa, nguvu ya misuli na madaraka, kutokana navyo viumbe wenye uchu wa madaraka, wasio na akili na wafisadi wanazunguka siasa hizi. Siasa za kisekula maana yake ni siasa za maslahi ya kibinafsi - ambapo hakuna uhusiano wowote na kumcha Mwenyezi Mungu (swt), kukabili hukmu katika maisha ya akhera na kupata Pepo kupitia kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Kwa sababu hiyo, ingawa nyuso za tabaka tawala zimebadilika katika miongo kadhaa iliyopita, lakini hatima ya watu haijabadilika.

Wafuasi wa usekula wa nchi hii wanataka kuficha sura mbaya ya siasa za kisekila kwa kuiita BNP fashisti mamboleo na wanataka kunyakua manufaa ya kisiasa. Swali ni je, BNP ya kisekula itakuwaje tofauti na Awami League ya kisekula? Na je chama chao cha kisekula kitakuwa tofauti vipi?

Wakati huo huo, wananchi hawajashuhudia chochote tofauti na siasa za jadi za Awami-BNP katika shughuli zao. Mwandishi mmoja wa habari aliyejadiliwa sana amejaribu kuficha hasira za wananchi kwa kuyaita mauaji haya ya kikatili kuwa ni mgogoro wa ndani wa BNP, akichukulia tukio hilo kuwa ni suala la BNP badala ya suala la watu; kama vile BNP ilivyolaani kama tukio la kipekee. Ilhali mamia ya viongozi na wanaharakati wao wameuawa katika vita vya kung’ang’ania madaraka katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Je, siasa zisizoweza kujenga umoja kati ya viongozi na wafanyikazi zinawezaje kuwaunganisha watu? Je, siasa zinazotengeneza uongozi wa kifisadi badala ya uongozi wenye tabia njema zinawezaje kuwajali wananchi? Kwa njia hii, wanasiasa na wasomi wa kisekula wanafunika kufilisika kwa falsafa yao ya kisiasa ya usekula. Watu wamesababisha kuporomoka kwa dhalimu Hasina kwa gharama ya kafara nyingi; huku wananchi wakitaka suluhisho la kisiasa kwa msingi wa Uislamu, kulinda maslahi ya watu na kulinda ubwana wa nchi katika Bangladesh mpya, wanasiasa na wasomi watiifu kwa nchi za Magharibi wana shauku kubwa ya kuendeleza suluhisho lile lile potovu la kisiasa la kisekula kwa wananchi kwa jina la mageuzi. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُوا فِي الأَرْضِ قَالُوا إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ]

Na wanapo ambiwa:Msifanye uharibifu ulimwenguni. Husema: Bali sisi ni watengenezaji. [Surah Al-Baqarah: 11].

Siasa katika Uislamu ni wajibu mtakatifu, ambao unaitwa ‘siasat’. Madhumuni yake ni kuhakikisha ustawi wa watu kwa kutekeleza katiba ya Kiislamu, kuweka uadilifu, na kuulinda Umma wa Kiislamu dhidi ya utawala wa kijeshi, kiuchumi na kithaqafa wa dola za kigeni; Zaidi ya yote, kueneza maadili ya kweli ya Uislamu duniani. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمْ الْأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لَا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ» “Walikuwa Banu Israil siasa zao (siasat) zilikuwa zikiendeshwa na Manabii, kila anapokufa Nabii badala yake alikuja Nabii mwengine, lakini hakuna Nabii atakayekuja baada yangu. Kutakuwepo na Makhalifa na watakuwa wengi” [Bukhari na Muslim].

Siasa za kisekula zilizopandikizwa na wakoloni makafiri wa Magharibi ni janga kwa Umma wa Kiislamu. Kuishi chini ya mfumo huu, kwa upande mmoja, tunashuhudia vifo vya kikatili vya ndugu na dada zetu wasiohesabika kama Sohag na kwa upande mwingine, tunazidisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) dhidi yetu. Watu lazima waungane pamoja na chama chenye ikhlasi cha Hizb ut Tahrir katika siasa za kusimamisha Khilafah. Siasa za Kiislamu pekee ndizo zitakazowakomboa Waislamu kutoka katika vurugu, mapigano na siasa za ulafi wa maslahi ya kibinafsi, na kuwaunganisha watu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu