Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Canada

H.  30 Dhu al-Hijjah 1439 Na: 1439 H/01
M.  Jumatatu, 10 Septemba 2018

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Canada imetumana ujumbe kwa Ubalozi wa Pakistan kutaka kuachiliwa kwa Dada Romana na Dada Roshan ndani ya Pakistan

Hizb ut Tahrir / Canada imetumana ujumbe rasmi kwa Ubalozi wa Pakistan ndani ya Toronto ukiomba kwa mamlaka za Pakistan kutimiza jukumu (Fard) lao la Kiislamu la kuwaachilia Dada Romana na Dada Roshan. Kama ilivyoelezewa katika taarifa kwa vyombo vya habari waliyokabidhi ubalozi ikiwa ni sehemu ya ziara hii, dada hawa walitekwa nyara na mamlaka za Pakistan na sehemu waliko haijulikani. Katika mkutano na naibu balozi, ujumbe uliwasilisha kukasirishwa kwake na vitendo vya mamlaka za Pakistan ambao wamefikia kiwango cha kumteka nyara mama kutoka kwa watoto wake, na kuwaacha watoto katika hali ya majonzi na kuwakatisha tamaa. Ujumbe pia uliweka wazi hali ya mamlaka za Pakistan kutozingatia Shari’ah ya Mwenyezi Mungu (swt) ambayo inaharamisha utekajinyara watu. Mamlaka za Pakistan zimefikia kiwango duni cha kufikia hatua ya kuwateka nyara wanawake ambao uhalifu wao ni kulingania kutekelezwa kwa Dini ya Mwenyezi Mungu (swt) ndani ya Pakistan.

Huku ni kukiuka haki bali ni mfano wa dhuluma nyingi zinazotekelezwa na mamlaka za Pakistan dhidi ya watu wa Pakistan na kwa mara nyingine tena inadhihirisha umuhimu wa kubadilisha nidhamu fisadi ya utawala ndani ya Pakistan na ile ya dola ya kweli ya Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni kupitia tu dola hiyo ndipo watu wa Pakistan watahisi uadilifu na utawala unaofuata sheria.

Hizb ut Tahrir – Canada

#WawacheHuruRomanaNaRoshan

Fuatilia Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari kwa ajili ya Dada Roshan na Romana

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Canada
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu