Alhamisi, 09 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  28 Muharram 1444 Na: 01 / 1444 H
M.  Ijumaa, 26 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pendekezo la Kupiga Marufuku Hijab ni Tangazo la Vita dhidi ya Jamii ya Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Serikali mbalimbali za Denmark kwa muda mrefu zimefuata sera ya chuki dhidi ya Uislamu iliyo dhihirishwa kwa sheria zinazolenga maadili na mfumo wa maisha wa Kiislamu. Serikali ya sasa inataka kupiga hatua kubwa mbele katika mapambano yake ya kidhalimu ya kuwaoanisha kwa nguvu Waislamu nchini Denmark.

Kupitia tume iliyoundwa na serikali, inayoongozwa na Meya wa Kidemokrasia ya Kijamii, na ambayo wanachama wake wengine wanajumuisha watu wasio na uwezo wanaochukia Uislamu, imechagua kukabiliana na marufuku ya hijab ya Kiislamu katika shule za msingi na sekondari.

Marufuku kama hiyo haiwezi kueleweka kuwa kitu chengine isipokuwa tangazo la wazi la vita dhidi ya umma wa Kiislamu. Inajulikana vyema nchini Denmark - na pia kote ulimwenguni - kwamba hijab ni faradhi kubwa ya Kiislamu. Fauka ya hayo, hijab imekuwa ni nembo ya kitambulisho cha Kiislamu, na inadhihirisha maadili matukufu kama vile adabu, uongofu na hadhi ya kuheshimika ya wanawake katika Uislamu. Haya ni maadili madhubuti ya Kiislamu, ambayo serikali ya Denmark tayari inapambana nayo vikali.

Kwa hoja ya "kupambana na udhibiti wa kijamii", udhibiti zaidi wa serikali wa Waislamu unatakwa na serikali kupitia kuwavua nguo kwa lazima wasichana wa Kiislamu na kuongezeka kwa ufuatiliaji wa familia za Kiislamu. Vitendo ambavyo haviko mbali na kufanana na sera ya kibabe ya utawala wa China dhidi ya Waislamu wa Uyghur.

Kuwavua nguo kwa kulazimishwa wasichana wa Kiislamu, hata hivyo, kutafichua tu ubaya wa mfumo wa kidemokrasia uliojengeka kwa dhuluma-ya-idadi ya wengi na kufilisika kwa maadili huria ya uhuru. Katiba ya Denmark, ambayo wanasiasa mara nyingi huwataka Waislamu kula kiapo cha utiifu, inahujumiwa na wao wenyewe.

Katika ugumba wa nguvu za kiroho mbele ya fikra za ushawishi za Uislamu na maadili ya kweli, walinzi wa demokrasia wamechagua kuvunja nguzo zinazoimarisha msingi wa jamii ya Denmark. Katika kutapatapa kwao kuwatiisha Waislamu, wanapigilia misumari ya mwisho kwenye jeneza la demokrasia.

Wanasiasa hao wameshindwa kuwakinaisha wasichana na wanawake wa Kiislamu kwamba mtazamo mchafu wa thaqafa ya Kimagharibi kuhusu wanawake na uasherati ndio njia ya maisha huru na yenye furaha. Kwa hivyo, wanakimbilia kuharamisha na kulazimisha. Lakini wasichana wa Kiislamu wanasisitiza kuishi maisha ya kimaadili na kuvaa kwa heshima, huku wakizidi kujiweka mbali na mtazamo duni wa Kimagharibi wa wanawake.

Tunataka kuweka wazi kwa serikali ya Denmark na umma kwamba Waislamu kamwe, hawatakubali kupigwa marufuku kwa hijabu.

Tutapambana na kila kitu tulicho nacho ili kuzuia marufuku kama hii kuwa uhalisia. Tutapigania haki yetu ya kuvaa kama Muumba wetu alivyotuamuru, na jukumu letu la kuwalinda dada na binti zetu wapendwa.

Wasichana na wanawake wa Kiislamu lazima waweze kuvaa hijab zao kwa fahari kila mahali: shuleni, sehemu za kazi na katika maeneo ya umma. Wanasiasa wanaochukia Uislamu bado hawaonekani kufahamu kwamba tutapigania hadi pumzi zetu za mwisho kwa ajili ya kitambulisho na maadili yetu.

Sisi katika Hizb ut Tahrir tunawalingania Waislamu wote kusimama pamoja, kufanya kazi pamoja na kupigana bila kuchoka kwa namna ya Kiislamu hadi mwisho kwa ajili ya jukumu hili tukufu la Kiislamu ambalo hatutaliacha kamwe.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu