Alhamisi, 07 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  15 Shawwal 1443 Na: 10 / 1443 H
M.  Jumapili, 15 Mei 2022

 Barua ya Wazi kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu, Wasomi, na Vyombo vya Habari

Serikali ya Denmark Yatekeleza Ubabe wa Kimaoni na Kukitishia Chuo Kikuu cha Copenhagen!

(Imetafsiriwa)

Mnamo Machi 25, 2022, mhadhiri, mdahili, na mwanachama wa Hizb ut Tahrir, Taimullah Abu Laban, alialikwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Kiislamu (MSA) Bewa la City kutoa mhadhara katika Kitivo cha Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu cha Copenhagen (KU). Hafla hiyo ilipewa anwani: "Je, Uislamu ufanywe kuwa wa kisasa?".

Kwa wote walioshiriki, ilikuwa wazi kwamba hafla ilikuwa ya mafanikio - mjadala ulikuwa wa wenye ukweli, kusisimua, na muhimu mno.

Hata hivyo, mwitikio wa kisiasa uliofuata haukuwa na shaka. Ulikuwa wa kiadui, kama ambavyo tumeona mara nyingi hapo awali, wakati Waislamu wakijieleza hadharani kwa mtazamo usio wa kisekula. Shinikizo kubwa la kisiasa liliwekwa kwa Mkuu wa Kitivo cha Sayansi za Jamii wa Chuo Kikuu cha Copenhagen kwa kuruhusu hafla hiyo.

Spika wa zamani wa Bunge la Denmark, Pia Kjærsgaard, aliitisha taarifa kutoka kwa Waziri wa Utangamano. Msemaji wa chama cha serikali alitoa maoni ya hasira ambapo alimshambulia mkuu huyo moja kwa moja.

Lakini, shambulizi hilo la kisiasa la kutisha halikuishia hapo. Baada ya mkuu huyo kukataa kujisalimisha kwa shinikizo hilo la kisiasa, serikali ilijihusisha moja kwa moja katika mjadala huo. Katika mahojiano na BT, Waziri wa Elimu na Utafiti alimshambulia mkuu huyo mara kadhaa kwa kuruhusu hafla hiyo na akakituhumu kitivo hicho kwa "kuunga mkono mtazamo wa kizamani wa usawa".

Waziri huyo pia alimtuhumu mkuu huyo kwa kuwa "mjinga sana" kwa sababu alisema kwamba wanafunzi wenyewe walichagua viti vyao. Ikiwa mtu anaamini kwamba Waislamu wanatenda kwa hiari kwa mujibu wa imani yao wenyewe katika nchi hii, mtu huyo atakuwa ni mjinga wa wazi.

Wakati huo huo, muhusika alikuwa wamealikwa na MSA Bewa la Southern kwenye mjadala pamoja na profesa wa KU yenyewe, Thomas Hoffmann, mnamo tarehe 17 Mei, chini ya kichwa "Uhalifu wa Magenge: Je, Uislamu Ndio Tatizo au Suluhisho?". Kwenye Facebook pekee, karibu watu 700 walikuwa wamesema kwamba wangehudhuria au kuwa na hamu na hafla hiyo. Lakini serikali ilikuwa na mawazo mengine.

Waziri mpya aliyeteuliwa hivi karibuni wa Uwiano, Kaare Dybvad Bek, ana mengi ya kuyatekeleza baada ya watangulizi wake wawili, inapokuja katika milipuko ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Alitoa mahojiano na Weekendavisen na kuandika maoni marefu kwenye Facebook, ambayo yote yalikuwa msururu mrefu wa mashtaka, yaliyojaa vitisho vipya dhidi ya mkuu huyo wa kitivo, ambaye waziri alimkumbusha kuhusu "mshahara wake mzuri". Waziri alifikia hatua ya kuahidi vikwazo vya kisheria au kulazimisha "miongozo" kwa chuo kikuu hicho endapo mkuu huyo wa kitivo mwenyewe hataipiga marufuku Hizb ut Tahrir kutokana na hafla zijazo.

Matokeo? Mjadala ulifutiliwa mbali. Bodi ya MSA iliitwa, kinyume na utaratibu wote, kwa mkutano wa kushangaza na wakuu wa vitivo wasiopungua wawili na mkurugenzi wa kitivo. Kwa "sababu zisizojulikana", mkutano unaweza tu kufanyika muda mrefu baada ya tarehe ya mjadala uliopangwa.

Katika hali hii, ningependa kusisitiza yafuatayo:

- Serikali ya Denmark inadai kwamba Hizb ut Tahrir na wengineo, wanaoegemeza maadili na mitazamo yao juu ya Uislamu, wanatishia mshikamano, demokrasia na maadili huria ya uhuru. Lakini ni ukweli unaojulikana kote duniani kwamba kazi ya Hizb ut Tahrir ni ya kisiasa na kifikra pekee. Ikiwa demokrasia na maadili huria ya uhuru hayahimili mjadala, basi yana thamani gani?

- Hakuna kinahujumu kanuni zinazodaiwa kuwa takatifu zaidi katika jamii ya Denmark, kwa ufanisi zaidi kuliko sera lazimishi yenye kuongezeka kuendelea ya kubadilisha serikali kwa miaka 20 iliyopita.

- Kufutilia mbali hafla ya mdahalo iliyopangwa tarehe 17 Mei huko KU kunajiri kama matokeo ya moja kwa moja ya shinikizo la kisiasa na vitisho kutoka mahali pa juu zaidi vinavyoelekezwa kwa usimamizi wa kitivo. Inaweza tu kuelezewa kama ubabe wa maoni na udhibiti.

- Serikali inahujumu uhuru wa kujiamulia wa KU, inawakataza wanafunzi na wasomi wengi ambao walikuwa wametazamia kuhudhuria mdahalo huo, na kumhujumu profesa wa KU kama mtaalamu na mdadisi pinzani anayefaa.

- MSA iko chini ya ubaguzi na kuzuiwa kuandaa mjadala wa hali ya juu unaohusiana sana na jamii, licha ya kufuata sheria zote na miongozo yote ya chuo kikuu.

- Uhuru wa kujieleza, kwa mara nyingine tena, unathibitisha kuwa ni chombo cha kisiasa ambacho kinachofaa sana pindi Waislamu wanapokabiliwa na chuki kutoka kwa wanasiasa, lakini ni marufuku kabisa wakati wanapotaka kupiga marufuku maoni "yasiofaa" kwenye mjadala. Kwa upande huo hakuna jipya.

Kwa wanafunzi na wasomi wa vyuo vikuu:

Fursa zenu za mijadala ya wazi na muhimu zinapunguzwa kutoka mahali pa juu zaidi kisiasa siku hizi. Ili taasisi za elimu ya juu zisigeuke kuwa chumba cha mwangwi wa maoni "ya kawaida", yanayoamriwa na hali ya kihisia ya mawaziri, majibu yanahitajika. Katika hali hii, ni muhimu kwamba usimamizi wa KU ueleweshwe kwamba kushughulikia kwake kesi hii ni kielelezo cha uti wa mgongo unaonyumbulika isivyo kawaida, na kwamba wanafunzi na watumiaji wa chuo kikuu, tofauti na usimamizi, wanathamini kanuni zaidi kuliko hatari ya kukaripiwa na wanasiasa wasaka tonge.

Kwa vyombo vya habari vya Denmark:

Katika kisa hiki, kama ilivyo katika visa vingine vingi, mengi yanaweza kuvuliwa kutoka kwa yale ambayo hamuyaangazi. Wakati mashambulizi ya kibinafsi yalipozinduliwa baada ya halfa ya awali ya MSA, hakukuwa na uhaba wa wamiliki wa maikrofoni waliokuwa tayari. Lakini isipokuwa rai moja katika Gazeti la Weekendavisen kutoka kwa Thomas Hoffmann aliyevunjika moyo, kumekuwepo na kelele na ukimya usio wa kukosoa kuhusiana na kufutiliwa mbali kwa mjadala wa kisiasa mnamo tarehe 17 Mei. Ni wazi hamjali mijadala ya wazi katika vyuo vikuu. Hitimisho linaonekana kuwa kana kwamba mtu anaweza ima kushikilia maoni yale yale kama ya waziri wa uwiano au kujifunza kukubali dhihaka na kejeli – chaguo ni huru!

Mimi, na Hizb ut Tahrir/Denmark, tutaendelea kuwa wachangamfu katika mijadala. Tukiwa pamoja au bila ya Chuo Kikuu cha Copenhagen. Tukiwa na au bila ya idhini ya serikali. Tofauti na wanasiasa wa Denmark, sisi kwa hakika tunasimama na maoni yetu.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu