Jumatatu, 11 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  29 Ramadan 1443 Na:
M.  Jumamosi, 30 Aprili 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waziri Mkuu wa Denmark aidhinisha Sera ya Umwagaji damu ya India dhidi ya Waislamu

(Imetafsiriwa)

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, atafanya ziara rasmi nchini Denmark Mei 3 - 4. Atakula chakula cha jioni na Malkia pamoja na kushiriki katika mkutano wa kilele wa Indo-Nordic, ulioandaliwa na Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen.

Modi ni mfuasi aliyetangazwa wa vuguvugu la vurugu na la kifashisti la Hindutva. Mnamo mwaka wa 2019, alikuwa nyuma ya uunganishaji wa kikatili wa jimbo la Kashmir lililo na Waislamu wengi, ambalo watu wake kwa miongo kadhaa wamekuwa wakikamatwa, kutekwa nyara, kuteswa na kubaka kiholela yanayofanywa na Jeshi la India.

Narendra Modi na chama chake cha Kitaifa cha Kibaniani, BJP, wameendeleza sera hiyo ya chuki dhidi ya Uislamu tangu walipoingia madarakani mwaka 2014 kiasi kwamba wachunguzi kadhaa wa kimataifa wanaamini kuwa India inaelekea kwenye mauaji ya halaiki ya Waislamu wa nchi hiyo!

Katika mkoa wa Assam kaskazini mashariki mwa India, serikali ya India imekuwa ikifanya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa eneo hilo. Asili ni sera ya Narendra Modi ya kuwatenga baadhi ya Waislamu wa India kwa kuwatangaza “wahamiaji haramu”.

Haya yote pia yalikuwa yakiendelea katika kipindi ambacho Mette Frederiksen alikuwa katika ziara rasmi ya kiserikali nchini India. Kama ilivyokuwa kwa ziara iliyokaribia ya Modi nchini Denmark, wakati huo hakukuwa na kivuli cha utangazaji muhimu wa vyombo vya habari au kuangazia mateso ya Waislamu wa India na sera za vurugu za Modi.

Waziri Mkuu, wakati huo huo, alisifu kauli mbiu ya Modi, “taifa kwanza”, ilipozungumza nchini India. Kauli mbiu ambayo kwayo serikali ya India imetangaza kuwa Waislamu walio wachache ni marufuku.

Huku Mette Frederiksen akiuita ukatili wa Urusi nchini Ukraine “uhalifu wa kivita”, hana la kusema kuhusu uhalifu unaofanywa dhidi ya Waislamu wa India kila siku, unaoongozwa na Narendra Modi. Hata amesema kwamba vita vya Ukraine vitakuwa ndio mada ya mazungumzo wakati wa ziara yake ijayo!

Ni wazi kwamba kuna uendekezaji unaopatikana kwa mwelekeo wa India wa itikadi kali na chuki dhidi ya Uislamu katika Denmark ya kisiasa. Mwelekeo ambao Denmark yenyewe imekuwa ikiufuata kwa miongo miwili iliyopita.

Waziri Mkuu wa Denmark na vyombo vya habari vya Denmark visivyo kosoa vimeweka wazi jambo moja: Mateso ya kikatili dhidi ya Waislamu wa India sio tatizo kwa Denmark.

Ni nadra mtu kuwahi kushuhudia mandhari kichefuchefu ya wazi zaidi ya ubaguzi wa kibinadamu ambao umeenea katika siasa za Denmark na Magharibi.

“Maadili" yote ya hali ya juu ya Magharibi ambayo wanajaribu kuwalazimishia Waislamu kila siku yanatupiliwa mbali bila kusita kunapo patikana msingi wa pamoja wa chuki kwa Uislamu, na maslahi ya kiuchumi yanayopaswa kukusanywa.

Hizb ut Tahrir / Denmark inalaani vikali muhuri rasmi wa Denmark wa kuidhinisha mateso ya kinidhamu na ya umwagaji damu dhidi ya Waislamu nchini India. Mtu yeyote mwenye utu na hisia ya haki anapaswa kufanya vivyo hivyo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu