Jumapili, 05 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  7 Rajab 1444 Na: 03 / 1444 H
M.  Jumapili, 29 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uchomaji Quran! - Serikali Zinahusika kwa Makosa Haya Yanayojirudia

(Imetafsiriwa)

Baada ya tukio la hivi majuzi la kuchomwa moto Qur'an, kwanza mbele ya ubalozi wa Uturuki jijini Stockholm mnamo Januari 21, na hivi karibuni zaidi kwenye swala ya Ijumaa mnamo Januari 27, mbele ya msikiti mmoja jijini Copenhagen, wanasiasa ghafla wako mbioni kuosha mikono yao. Huku balozi wa Denmark akiitwa nchini Uturuki, Waziri wa Mambo ya Nje Lars Løkke Rasmussen aliiambia DR kwamba “anajitenga mbali sana” na kile alichokiita “uchokozi”. Kwa maneno yake mwenyewe, anaona “kuwa ya kuchukiza sana” kwa mtu kufanya vitendo kama hivyo, ambavyo kwa mujibu wa Lars Løkke “kamwe haiwakilishi Denmark”.

Sauti hii isiyo ya kawaida na ya kinafiki mno kimaumbile inakuja katika muktadha wa hamu ya Uswidi kujiunga na NATO, ambayo inaweza tu kufanywa kupitia idhini ya Uturuki.

Ingawa vitendo hivi vya chuki haviwakilishi raia wa kawaida wa Denmark, vinawezeshwa na serikali ya Denmark, na kwa kiwango cha juu kabisa ni matokeo ya miongo miwili ya sera ya chuki dhidi ya Uislamu katika nchi hii na nyinginezo za Ulaya. Tangu miaka ya 2000, uhuru wa kujieleza umekuwa silaha inayopendelewa zaidi ya wanasiasa wa Denmark na vyombo vya habari linapokuja suala la kutekeleza ukiukaji na chuki dhidi ya Waislamu. Waziri wa Mambo ya Nje labda anadhani kwamba kila mtu amesahau kwamba alikuwa sehemu ya serikali iliyohimiza vikaragosi vya chuki, ambavyo vilipaswa kuwalazimisha Waislamu kukubali “dhihaka, matusi na kejeli”. Serikali hiyo hiyo iliyoitupa Denmark katika vita vya kichokozi vya Marekani dhidi ya nchi za Kiislamu, ambapo nakala za Qur'an zilinajisiwa kwenye kambi ya mateso, Guantanamo Bay, na ambako askari walizifyatulia risasi nakala za Qur'an nchini Iraq na kuzichoma moto kwenye Kambi ya Bagram nchini Afghanistan.

Uhuru wa kuzungumza umefichuliwa kwa muda mrefu kama chombo cha nguvu ya kisiasa. Marufuku na ushurutishaji huanzishwa kote Ulaya linapokuja suala la misemo na desturi za Kiislamu. Tunaliona hili kwa kupigwa marufuku kwa hijabu, sheria maalum zinazowalenga maimamu, kuyatia hatiani maadili ya familia ya Kiislamu, kufungwa kwa misikiti na shule za Kiislamu nk. Huku katika kesi nyingi nyengine jamii nzima inalazimika kutembea juu ya maganda ya mayai ili kutohukumiwa au kushutumiwa kwa matamshi ya chuki, chuki iliyojengeka kisiasa juu ya Uislamu, ambayo imerutubisha haki iliyokithiri, inakuzwa na kulelewa.

Rasmi, Denmark ya kisiasa, pamoja na serikali zinazobadilika, kwa zaidi ya miongo miwili imefanya uadui dhidi ya Waislamu na mapambano dhidi ya Uislamu - sio kwa mabishano na mijadala yenye ukweli - lakini kwa vita, sheria maalum za kibaguzi, uchochezi na ukiukaji - fadhila huru na nidhamu ya kisiasa. Vitendo vya chuki vya watu waovu dhidi ya Waislamu ndivyo vinavyowakilisha kwa usahihi kabisa Denmark ya kisiasa.

Hii inashuhudia udhaifu mkubwa wa kifikra katika Ulaya ya kiliberali, ya kisekula, ikiwemo Denmark. Uislamu na Waislamu wana utamaduni tajiri wa mijadala ya kukosoa, lakini kamwe hatutashitushwa na matusi ya chuki! Wao wanasubutu hata kuwataka Waislamu wapuuze pale wanapokabiliwa na chuki. Sera ya kimpangilio dhidi ya Uislamu ya serikali mtawalia, ikiwemo na hii ya sasa, haiwezi na haifai kunyamaziwa.

Tunaweka jukumu pale linapostahili, kwa chuki na uadui dhidi ya Waislamu ambao umeenea kutoka Kasri la Christiansborg hadi kwa jamii pana. Wakati huo huo, tunasisitiza kwamba Waislamu barani Ulaya na kwengineko wataendelea kuwa hatarini maadamu hatuna mamlaka ya dola ambayo kwa hakika inawakilisha imani na mapenzi ya Waislamu. Kwa hiyo tunatoa wito kwa kila Muislamu kushiriki katika kazi ya kusimamisha tena Khilafah katika ardhi za Waislamu - Khilafah Rashida, ambao kwa njia zote zile; kiuchumi, kidiplomasia na, ikibidi, kijeshi, italinda matukufu ya Uislamu.

Elias Lamrabet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Denmark

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu