Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  12 Rajab 1444 Na: 1444 / 09
M.  Ijumaa, 03 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hennis-Plasschaert: Ufisadi nchini Iraq: “Ni wa Kimfumo”
(Imetafsiriwa)

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq. Ndiyo, Hennis-Plasschaert; ufisadi nchini Iraq upo kwa mujibu wa mfumo ulioundwa na Marekani tangu siku ya kwanza ya kuikalia kwa mabavu Iraq. Baada ya kuitengenezea katiba yake inayosimamia ufisadi huu ili kuleta machafuko na uharibifu nchini, ambalo ndilo lengo kuu la kuikaliwa kwa mabavu ili kuendelea kupora mali yake, na kuizuia kufanya kazi ya mwamko wa Ummah kwa sababu Iraq inawakilisha tishio kwa uwepo wa kikoloni, kutokana na eneo lake, nyenzo na nguvukazi, na kina kielimu. Huu hapa ni mfumo wa ufisadi uliohalalishwa kwa mujibu wa katiba iliyoundwa na Amerika, iliyo na kitovu cha kisiasa ambacho ilikileta kwa uvamizi wake wa Iraq:

Kwanza: fikra ya madhehebu: Iraq iliunda madhehebu na makabila kila moja likiwa na maregeleo yake, jambo ambalo linapelekea kamwe kutowaunganisha katika jambo la kisiasa isipokuwa kwa yale ambayo Amerika inayalazimisha, kutokana na maono tofauti ya maregeleo hayo. Baya zaidi ya hilo ni kwamba imeyaweka chini kuwa mipaka ya mapigano, migogoro na uharibifu.

Pili: migao: ambayo ilifungua milango ya ugavi wa nyadhifa na nafasi za kazi, kufikia kiwango cha mfanyikazi wa huduma, bila kuzingatia utoshelevu, na kuweka asilimia ya bajeti ya vyama, ambayo huporwa kupitia mawaziri na mameneja, ambayo rasmi na kisheria ilifungua mlango wa wizi na kuuza nyadhifa.

Vipengele muhimu zaidi vya katiba hii vilijumuisha nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii:

Katika ngazi ya kisiasa: fikra ya madhehebu na migao ilijenga hali ya ukosefu wa umoja, na dira moja ya kisiasa inayoonyesha umoja wa nchi na maslahi yake makuu. Kwa hivyo, mafungamano ya pembeni yalifanyika na nchi jirani za kikanda, ambazo ziliongeza mzozo kutokana na maslahi tofauti kati ya nchi hizi.

Katika ngazi ya kiuchumi: mhalifu Amerika, kwa sababu ya kizuizi chake na uvamizi wake wa nchi hii, iliharibu miundombinu ya viwanda na kilimo, na baada ya hapo ilifanya kazi kutoijenga tena, hasa miradi msingi ya viwanda na umeme. Mbali na miradi mikubwa ya kilimo na mabwawa yaliyopendekezwa, yote yalisababisha udhaifu au kutokuwepo kwa uzalishaji wa ndani na kutegemea kikamilifu nchi jirani kuagiza umeme, vyakula na bidhaa za matumizi. Badala yake, ilifungua milango kwa makampuni ya kigeni, na makampuni ya mafuta kwa jumla, kuwekeza bila usimamizi. Mapato ya kifedha ya serikali yalitoka kwa mapato ya mafuta pekee, ambayo mengi ya zaidi huibiwa.

Kinachosalia, asilimia ndogo yake huenda kwenye ujenzi upya wa kindoto. Asilimia kubwa zaidi yake huenda kwenye kuajiri watu kama waajiriwa au kutoa fidia na misaada, bila kujali masuala ya kilimo au viwanda. Hii inamaanisha kwamba serikali inabidi kuajiri idadi kubwa ya wafanyikazi, isiyoweza kuimudu, na matokeo yake ni upungufu katika mizani ya malipo, na kupata deni kutoka kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, na hii inamaanisha kudhibiti sera ya kiuchumi ya serikali, maeneo yake ya matumizi, kuamua bei ya mafuta, na kuamua thamani ya ubadilishanaji wa dinari ya Iraq dhidi ya dolari ya Marekani, na haya ndiyo tunayoyashuhudia sasa ya kuporomoka kwa thamani ya dinari, ambayo inatarajiwa kufikia dinari 2000 kwa dolari moja!

Ama katika ngazi ya kijamii: Katiba na tamko lake la kutabanni usekula, na kutoheshimu maadili ya kidini kwa kutilia mkazo uhuru wa kibinafsi na wa kiitikadi, kumefungua mlango wa upagani na vitendo vingi vya kihalifu. Ikisaidiwa katika hili na kundi la mifumo ya elimu endelevu ambayo Amerika na Umoja wa Mataifa zinataka kuilazimisha katika nchi za Kiislamu kupitia kuunda mashirika nchini humu ambayo yanaitangaza na kuitetea, ikiwemo ushoga na unyanyasaji wa kinyumbani.

Ndio, umesema ukweli na wewe ni mrongo, Ewe Hennis-Plasschaert! Ni mfumo uliopangwa, lakini inabidi useme hivyo kwa Umoja wa Mataifa na ukubali kwamba ulikuja pamoja na uvamizi, mfumo wake na katiba yake uliyolazimisha juu ya Ummah wa Iraq, na katika nchi yoyote inayoingia ili kufikia malengo yake.

Enyi Waislamu: Lengo la vitendo vyote hivi vilivyofanywa na Marekani na Magharibi kafiri kwa jumla ni:

1- Kuzuia Umma wa Kiislamu usirudishe fahari na izza yake, na kuzuia kusimamishwa kwa dola yake ambayo itawaokoa wanadamu kutokana na dhulma na giza la usekula na mfumo wake wa kidemokrasia wa kibepari.

2- Kupora bidhaa za nchi hizi kwa manufaa ya makampuni ya kibepari, na kuendeleza mfumo unaoporomoka wa dhulma, ambao unawakilisha idadi chache tu kutoka kwa wanadamu.

Enyi Waislamu wa Iraq: Nyinyi na Ummah mzima lazima mjue kwamba hamna budi ila kuasi dhidi ya maadili mabovu ya kisekula na mfumo wake mbovu wa kidemokrasia wa kibepari ambao Marekani inauwakilisha katika hali yake mbaya zaidi, ili kukomesha dhulma na kuifanya haki itawale kupitia kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu ardhini, na kumnusuru Mwenyezi Mungu na Dini yake, na Mwenyezi Mungu ndiye msaidizi wenu, na Yeye yu pamoja nanyi.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah   #EstablishKhilafah
 #ReturnTheKhilafah  #TurudisheniKhilafah
 #KhilafahBringsRealChange  #بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي
 أقيموا_الخلافة#  كيف_تقام_الخلافة#
 #YenidenHilafet  #HakikiDeğişimHilafetle
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu