Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  25 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 1444 / 17
M.  Jumatano, 14 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pesa za Waislamu ziko Mifukoni mwa Wafisadi
(Imetafsiriwa)

Hatimaye, baada ya majadiliano marefu kati ya serikali na wawakilishi wa Bunge, mizozo na maafikiano kati ya kambi za kisiasa zilizoendelea kwa muda wa miezi mitano, Baraza la Wawakilishi lilipiga kura mnamo Jumatatu, sawia na 12/6/2023, kuhusu rasimu ya sheria ya bajeti ya serikali ya Iraq kwa miaka ya fedha (2023, 2024, 2025), baada ya kuongeza ibara mpya inayoelekeza kutoshughulikia maandishi, sheria, au uamuzi wowote unaokinzana na sheria ya bajeti, na kifungu kinachoelekeza nyongeza ya mishahara ya Baraza la Mwamko (Sahwat) kutoka dinari 250,000 hadi dinari 500,000 kutoka bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Mambo ya Ndani, na kifungu kuhusu tofauti za Vikosi vya Uhamasishaji, pia vinavyojulikana kama Kamati ya Uhamasishaji ya Wananchi, na nyingine zinazoelekeza uhamishaji wa mikataba iliyosalia katika Uchaguzi wa Tume hadi kuwa kandarasi za utenda kazi.

Bajeti hii imesifiwa kama mlipuko, inayofikia dinari trilioni 198 na bilioni 910 (dolari bilioni 153) kwa mwaka, na nakisi ya takriban trilioni 64.36 za dinari za Iraq (dolari bilioni 49), ambayo ni kiasi kikubwa kinachoweza kutatua shida zote za kiuchumi ikiwa wezi wafisadi hawakuchukua sehemu kubwa yake. Haya ndiyo yaliyozungumzwa katika kumbi za Bunge ambapo ilishuhudiwa kelele, vilio na ghasia, hasa kati ya kambi ya chama cha Kidemokrasia na Muundo wa Uratibu kuhusu mgao wa eneo la Kurdistan pamoja na faili la mafuta katika eneo hilo jambo ambalo lilipelekea Chama cha Kidemokrasia cha Kurdistan kusifu sheria ya bajeti na marekebisho yaliyotokea kama kutowatendea haki watu wa Kurdistan. Kiongozi wa chama cha Kidemokrasia, Kamal Kirkukli alisema, "Kilichotokea na kinachoendelea kutokea katika vikao vya bunge la Iraq ni makubaliano ya ajenda mbili zinazotiliwa shaka." Kirkukli alieleza, "La kwanza lilikuwa mafuriko ya chuki kubwa ya fikra ya kihuni iliyokita mizizi, na hamu kubwa ya kulipiza kisasi."

Akikusudia muundo wa uratibu, "Ama kuhusu ajenda ya pili, iliwakilishwa katika anguko la kundi la wasaliti kwenye bonde lenye kina kirefu la uhaini na utiifu, ambalo kwalo haikuwezekana kutoka humo. Kikundi kisichojali na kilichochoka ambacho kinatumai kuwa usaliti utakirudishia faida," akikusudia Chama cha Wazalendo cha Kurdistan (PUK), na akaongeza, "Muungano wa wenye chuki na wasaliti na watiifu ulibadilisha mchakato jumla wa kutunga sheria kuwa uwanja wa vita na hatua ya kugombania zabuni na kusafirisha ushindi wa uwongo."

Enyi Waislamu nchini Iraq: Makadirio ya bajeti ya kila mwaka yanatokana na yale mafuta ambayo Iraq inayasafirisha nje kwa mwaka mzima. Shariah imefafanua aina za miliki: miliki ya mtu binafsi, miliki ya umma, na miliki ya dola, na imeeleza kuwa kinachofanana na chanzo cha maji yanayotiririka ni kutoka kwenye miliki ya umma, mafuta ni sawa na hayo, ni mali ya umma, hukmu ni kuyasambaza kwa raia katika mali au huduma. Shariah ilimkabidhi mtawala uelekezaji utaratibu huu na kuutumia kwa maslahi ya Ummah, na Mwenyezi Mungu (swt) amemuonya yeyote anayechukua kitu chochote, hata kiwe kidogo kiasi gani, kutoka katika fedha hizi bila ya haki. Mwenyezi Mungu (swt) asema;

[وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ثُمَّ تُوَفَّى كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ]

“Na haiwezekani kwa Nabii yeyote kufanya khiyana. Na atakaye fanya khiyana, atayaleta Siku ya Kiyama aliyo yafanyia khiyana, kisha kila mtu atalipwa kwa aliyo yachuma, kwa ukamilifu; wala hawatadhulumiwa.” [Aal-i-Imran: 161].

Watawala wasaliti na wadanganyifu pia wanaonywa kuwa Pepo itakuwa haramu kwao. Yeye (saw) amesema: «مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلّا حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ» “Mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atampa usimamizi wa raia, kisha akafa siku ya kufa huku akiwa anawahadaa raia wake, isipiokuwa Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo.”

Lakini baada ya kukosekana mtawala muadilifu anayetawala kwa sheria ya Mwenyezi Mungu, na warithi wake ni Ruwaybidah (wazembe) wezi ambao ni vibaraka wa Magharibi, milki ya dola na milki ya umma ikawa ngawira kwao na mabwana zao, na hata milki ya mtu binafsi. hawakuepushwa na dhulma zao, kwani wanawabebesha watu mzigo wa kodi na mrahaba, na kuendesha kiwango cha ubadilishaji kati ya sarafu ili kuiba juhudi zao baada ya kuiba nchi na utajiri wake.

Kwa sababu hiyo, tuliwaona kwenye kumbi za bunge wakichapana makonde kwa wizi huo na hisa zao mithili ya punda. Wote wanadai maslahi yao kwa watu wa nchi, lakini hamu yao ni kundi ambalo wanaliwakilisha, kama mshairi alivyosema: "Na kila mtu anadai kuwa ameunganishwa na Layla ** na Layla hatambui hilo kwao!"

Enyi Waislamu: Ukafiri umeungana dhidi yenu, na mataifa yamekusanyika kupigana dhidi yenu, na nyinyi ni Umma wa bilioni moja na nusu, na wamiliki wa itikadi tukufu kabisa.

Na Mwenyezi Mungu ameibariki ardhi yenu kwa mali na neema, basi kwa nini msiuondoe udhalilifu mabegani mwenu, na muitikie wito wa Mola wenu Mlezi kwa kutowapa makafiri mamlaka juu yenu?

Na je, haya yatafikiwa isipokuwa kwa dola ya Khilafah na kiapo cha utiifu kwa imamu anayemcha Mwenyezi Mungu (swt) katika yale aliyokabidhiwa na (swt), imamu ambaye ni ngao ambayo watu wanapigana nyuma yake na wanalindwa naye?

Kwa ajili ya kheri ya dunia hii na Akhera, tunakulinganieni, enyi Waislamu, muwe pamoja na wafanyao kazi kwa ikhlasi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu