Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  28 Shawwal 1445 Na: 1445 / 12
M.  Jumanne, 07 Mei 2024

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Surat Al-Ahzab:23]
(Imetafsiriwa)

Kwa nyoyo zenye subira na kuridhia, Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq inamuomboleza mmoja wa Mashababu wake, ndugu mheshimiwa:

Nafea Al-Mahlawi (Abu Anas)

ambaye aliaga dunia kwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu usiku wa kuamkia Jumanne, 28 Shawwal 1445 H sawia na 7 Mei 2024 M.

Abu Anas, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa miongoni mwa Mashababu waliokuwa wakijitahidi kuhuisha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Alikuwa kielelezo cha bidii na ukakamavu, akitafuta kila lililo jema, akiwapendelea wengine kuliko yeye mwenyewe, mpaka alipopatwa na ugonjwa mkali. Alipigana nao kwa miaka mingi kwa uvumilivu na kuridhia hadi kifo chake.

Mwenyezi Mungu amrehemu marehemu wetu, na amjaalie rehema kubwa, na amuingize katika Mabustani yake Makubwa. Mwenyezi Mungu aijaalie familia yake na vipenzi vyake malipo makubwa, subira na faraja.

[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Surah Al-Baqara:156].

Hatusemi ila yale yanayomridhisha Mola wetu: “Wallahi hakika sisi tumehuzunishwa kwa kuondoka kwako ewe Abu Anas.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu