Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  26 Rajab 1441 Na: 1441/07
M.  Jumamosi, 21 Machi 2020

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Uokovu wa Ummah kutoka kwa Majanga yake na Kuhifadhi Hadhi yake kunaweza Kupatikana tu kwa Kufuata Njia ya Uislamu Kile ambacho Waislamu wanahitaji Leo ni Watawala Wenye Ikhlasi Wanaotafuta Kuwahudumia wao na Kuwaondoa katika Maafa
(Imetafsiriwa)

Ummah wa Kiislamu umepitia kumbukumbu ya maumivu; ni kumbukumbu ya kuvunjwa kwa serikali ya Kiislamu ambayo misingi yake imeanzishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) mjini Madina, kisha kuendelezwa na Waislamu, kizazi baada ya kizazi. Walinyoosha yale yaliyo pindishwa kutokana nayo, na kupanga upya kile kilicho pasuka kutoka kwa muundo wake, kwa hivyo ikadumu takriban karne 13. Kwa kweli ilikuwa ni nuru ya haki, mlinzi wa hadhi, ngome ya wote wanaokandamizwa, na ukuta imara wa kujihami wa Ummah wa Kiislamu, kufukuza dhulma na watu madhalimu, na kueneza wema kwa watu kwa kubeba sheria ya Uislamu kwa mataifa ya ulimwenguni kupitia da’wah na Jihad. Na raia wake – Waislamu na Wasiokuwa Waislamu – waliishi ndani yake kwa usalama na maelewano.

Walakini, chini ya kutojali walinzi wake, kupotoka kwa tabia ya watu wake, njama kali na uovu kutoka kwa maadui zake, na msaada kutoka kwa Waarabu na wasaliti wa Uturuki, wakiongozwa wakati huo na mhalifu wa karne Mustafa Kemal, bidhaa ya Uingereza, adui wa Uislamu na Waislamu, na kisu chake cha sumu ambaye aliudunga moyo wa Ummah na kumsaliti Khalifah wa Waislamu, kwa hivyo akakomesha nidhamu ya utawala ndani yake: nidhamu moja ya Khilafah, kuanzisha serikali ya Kisekula isiyokuwa na utambulisho mwengine zaidi ya chuki ya Uarabu na Uislamu juu ya siku isiyoweza kuelezeka ya kumbukumbu kutoka kwa wale wenye ikhlasi kwa Mola wao na Itikadi yao ya Kiislamu; mnamo 28 Rajab Muharram 1342 H sawia na 03/03/1924 M. Kwa hivyo, ulimwengu ukatanda kiza, jua lake limetoroka, ukweli umeondoka, na wema ukapungua kwa miaka 99, huku misiba mikali zaidi na majanga ikiyatikisa mataifa.

Tangu wakati huo, Ummah ukawa safu ya upigaji mishale ya makafiri wavamizi, ambao wamezichafua ardhi zake, wakakiuka utakatifu wake, kupora neema zake na kuupasua kwa kuweka mipaka na mabwawa kati ya sehemu zake. Wakawasha moto wa ujinga kupitia mizozo ya kitaifa, kizalendo na mizozo ya kimadhehebu, waliondoa vifungu vya sheria ya Mwenyezi Mungu, ambayo iliongoza Ummah kupitia utawala wa Khilafah, na kubadilisha kwa sheria za kutungwa na Mwanadamu kutoka kwa mafundisho ya kikafiri ya Urasilimali, na wakavuvia moto wa vita kati ya ndugu wa dini wa milele, na kuuleta Ummah ukingoni mwa umaskini na unyonge, unaotawaliwa na ukosefu wa ajira, na kuuwawa na magonjwa kama vile Janga la virusi vya Korona ambavyo vimezidi leo hii na kuenea ulimwenguni. Waliweka juu ya watu watawala kama madalali ambao ni watiifu kwao na kutekeleza njama zao, bila ya harakati ya dhati ya kuwasaidia watu kutokana na yaliowapata, ukitoa mfano wa kuporomoka kwa masoko na machafuko ya kiuchumi, kama vile kushuka kwa bei za mafuta, huku wakiwa wamepora pesa za watu na kuwa matajiri. Mithili yao ni dola za kiburi na dhulma, ambazo hutumia pesa nyingi kuchunguza anga, kuzalisha silaha za uharibifu mkubwa, kuanzisha viwanja vya michezo na sinema, na kudhibiti madawa madhubuti kuhifadhi bei zao, bila kufanya kazi kusaidia watu wanaougua kutokana na magonjwa sugu na yasioweza kutibika.

Vipi Masikini tulivyokuwa – kama hivi ndivyo ilivyo – dola tukufu ya Khilafah na imamu muadilifu anayetafuta kuinua watu kutoka kwenye majanga yao na umaskini, na kufanya uadilifu kwa waliokandamizwa, na kusimamia mambo yao kwa njia ambayo inawahakikishia usalama wao na hadhi yao kwa kusuluhisha na sheria ya Mwenyezi Mungu kati yao, na kuitakasa nchi kutokana na kashfa za makafiri wa kikoloni.

[وَنُرِيدُ أَنْ نَمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ * وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ]

“Na tukataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika ardhi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi * Na kuwapa nguvu katika ardhi.” [Al-Qasas: 5-6]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
 Wilayah Iraq

#ReturnTheKhilafah      #YenidenHilafet     #TurudisheniKhilafah     #Covid19    أقيموا_الخلافة#

 

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu