Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  12 Sha'aban 1442 Na: 1442/16
M.  Jumanne, 23 Machi 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Huduma za Usalama za Serikali Nchini Jordan
Zaendelea Ukaidi na Kumkamata Mwanachama Mwengine katika Mashababu wa Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Jioni ya Jumapili, 21/03/2021, Huduma za Usalama za serikali nchini Jordan zilimkamata Ustadh Adel Sarsour kutoka nyumbani kwake na kisha kumpeleka hadi kituo cha usalama, kisha akahamishiwa hadi Idara ya Ujasusi, na kukamatwa huku kulijiri baada ya majaribio kadhaa ya kumkamata kupitia njia ya uwongo na udanganyifu uliofanywa kwa mashababu wengine, kwa kumwita kwa kisingizio cha ajali na gari lake na walipokuwa hawakufanikiwa, walimkamata kutoka nyumbani kwake.

Haishangazi kwamba serikali nchini Jordan imewakamata wabebaji wa ulinganizi Uislamu, kwani ni serikali ambayo chimbuko lake ni magofu ya utawala wa Uislamu, ilivuruga sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikanyenyekea kwa ukoloni wa Magharibi mkoloni kafiri, na kutia saini mikataba na makubaliano ya kudhalilisha, wa mwisho wake ukiwa ni Mkataba wa Ushirikiano wa Ulinzi na Amerika, na wasifu wake wote umejaa kuwapotosha watu kutoka kwa njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Lakini serikali hii na ijue kuwa ukamataji huu hautawazuia wabebaji wa Dawah kutoka kwa ulinganizi wao, kwani wako tayari kilicho na thamani zaidi na wanachokipenda zaidi kwa ajili yake, na hawatadhuriwa na wale wanaowavunja moyo au wale wanaotafuta uadui kwao, na watabaki thabiti katika hilo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mpaka ushindi wa Mwenyezi Mungu utakapokuja, na ushindi Wake umekaribia, ahadi Yake kwa waja Wake itatimizwa, na mamlaka ya Waislamu yatarudi na Khilafah Rashida itasimamishwa hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na pua za wahalifu zitakuwa chini.

]وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ]

Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.”]Ash-Shu’ara: 227[

 

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu