Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  11 Sha'aban 1443 Na: 1443 / 16
M.  Jumatatu, 14 Machi 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hairuhusiwi Kushiriki katika Uchaguzi wa Manispaa chini ya Utawala wa Kisekula kupitia Uteuzi au Uchaguzi.
(Imetafsiriwa)

Uchaguzi wa manispaa ya Jordan, ambao unajumuisha mabaraza ya majimbo, mabaraza ya manispaa, na Baraza la Manispaa ya Amman, utafanyika mnamo tarehe 22/3/2022, kulingana na Tume Huru ya Uchaguzi ilivyotangaza. Naibu Waziri Mkuu - Waziri wa Serikali za Mitaa - alisisitiza wakati wa hotuba yake aliyoitoa katika mkutano na waandishi wa habari kuzindua kampeni ya kitaifa ya kupigia debe chaguzi hizi, ambayo ilichapishwa na Al-Ghad: "kwamba wananchi wanawajibika kwa uchaguzi wowote unaofanyika, kwani mwananchi ndiye anayegoma kwenda kupiga kura, na yeye ndiye anayemchagua anayemwakilisha, "na ufisadi upo popote pale na kuna mpango wa kuanzisha uangalizi kwenye mabaraza ya manispaa".

Haya yamejiri huku kukiwa na hofu ya kusitasita sana kushiriki katika uchaguzi wa manispaa za Jordan, kama ilivyotokea katika uchaguzi wa bunge. Kulingana na uchunguzi wa hivi punde wa maoni uliofanywa na Kituo cha Rasid kuhusu mitazamo ya watu kuhusu uchaguzi ujao, takriban asilimia 23 ya wananchi wa Jordan wananuia kupiga kura. Kinyume chake, asilimia 60.9 kati yao hawataki kushiriki katika chaguzi zijazo, jambo ambalo ni kielelezo kuwa hawaoni thamani yoyote inayoweza kupatikana kutokana na uchaguzi huo, iwe kwa ukosefu wa uadilifu au ufisadi uliokithiri katika idara na usimamizi chini ya utawala wa serikali ya kisekula, ambayo Waziri wa Serikali za Mitaa aliukiri kuwepo katika serikali kwa kusema, "Ufisadi ipo kila mahali", kana kwamba hauwezi kuepukika.

Kuhusiana na hili, tutaeleza hukmu ya Shariah juu ya kushiriki katika uchaguzi wa manispaa, ambao serikali ya utawala wa Jordan inaulingania:

A- Chaguzi za manispaa kwa upande wa huduma kwa wananchi na mambo ya kiutawala zinajuzu kwa msingi huu ila zimekabidhiwa kazi nyingi mpaka zimekuwa, haswa katika nchi yetu, chombo cha serikali kinachoshughulikia sera za serikali na kukusanya watu kwa ajili ya kuziunga mkono, pamoja na kutoa leseni kwa mambo yaliyoharamishwa katika Shariah.

B- Uhalisia wa manispaa ni kwamba haijitegemea yenyewe na hutoa huduma za kiidara. Badala yake, ni chombo cha utendaji ambacho kinahusishwa kivitendo na serikali, na mamlaka inailazimisha kwa shughuli zozote za kisiasa inazotaka, pamoja na kwamba hutumia pesa zake kinyume cha sheria; kwa hivyo, hukmu ya Shariah juu yake haitokani na ukweli kwamba ni taasisi ya kiidara na huduma isiyo huru na mamlaka ya kisiasa, bali inafungamana na vyombo vya utawala, sio tu kwa jina pekee, bali kiutendaji, kwa hivyo Serikali inaweza kufutilia mbali maamuzi ya Baraza la Manispaa, hata kama yatachukuliwa kwa itifaki.

C- Hivyo basi, hairuhusiwi kushiriki ndani yake kutoka kwa upande huu, hata ikiwa umejengwa juu ya "huduma na vitendo vya kiidara" ndani ya mipaka inayoruhusiwa, inaruhusiwa kushiriki ndani yake. Kwa maana nyengine, hatushiriki katika chaguzi hizi maadamu uhalisia wa manispaa hizi ni kama ulivyo elezwa Ama kuhusu ni wakati gani kushiriki inaruhusiwa, ni wakati ambapo manispaa hizi zinakuwa ni taasisi tu za kiidara pekee bila ya kuingiliwa na mamlaka ya kisiasa ndani yake.

Ni wazi kwamba chaguzi hizi huchukua tabia ya kisiasa chini ya tawala za sasa. Zinafanyika chini ya ushindani wa kisiasa wa vikundi vya "vyama" au kwamba vyama hivi vinasusia, kama inavyotokea kwa chaguzi hizi. Sio taasisi huru za kiidara, na ushahidi ni kwamba vyama vinazisusia, vinashiriki ndani yake, au serikali kuziitisha kwa sababu zinahusishwa na sera za dola, na ushindani wa kisiasa ndani yake unaonekana kama kiashiria cha uchaguzi ujao wa bunge au mwingine, au kama kipimo cha ushawishi katika mchezo wa siasa za kisekula.

Enyi Waislamu, Enyi Watu Wetu nchini Jordan:

Uchaguzi wa manispaa unafungamana na utawala wa kisiasa ya kisekula unaozitenga hukmu za Uislamu maishani, uchaguzi ni aina ya uwakilishi, na kwa hivyo hukmu ya Shariah katika suala la ushiriki wa uchaguzi inahusiana na uhalisia wa kile ambacho uchaguzi unafanywa kwa ajili yake. Ikiwa uchaguzi unahusiana na vitendo ambavyo vimeharamishwa kufanya, ambayo ndio hali hapa, basi ushiriki katika uchaguzi wa manispaa hauruhusiwi kwa sababu ni kutoa idhini ya kufanya vitendo vilivyo haramishwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu