Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  10 Muharram 1444 Na: 1444 / 02
M.  Jumatatu, 08 Agosti 2022

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuifanya Sekta ya Umma kuwa ya Kisasa Kunaelekea Kufeli Chini ya Mfumo wa Kisekula wa Serikali
Uliotenganishwa na Usimamizi wa Maslahi ya Watu na Uchungaji wa Mambo yao

(Imetafsiriwa)

Waziri Mkuu, Bishr Al-Khasawneh, alitangaza matokeo ya Kamati ya Kuboresha Sekta ya Umma, baada ya kazi ya miezi 6, ambayo inafanya kazi ya kutathmini hali za idara na taasisi 97 za serikali. Alisema “wizara na idara za serikali zitaunganishwa katika kipindi cha kuanzia 2022 hadi 2024, na kuongeza kuwa vyombo hivyo vinalenga kwa dhati kutumikia watu na wale wanaoshughulikia sekta ya umma, ili kuendana na matokeo ya ruwaza ya kisasa ya kiuchumi na mfumo wa kisasa wa kisiasa ambao ulizinduliwa kwa kuingia kwa karne ya pili ya nchi hii. Alisisitiza kuwa awamu ya kwanza ya mpango kazi wa utekelezaji wa ramani ya utendakazi itamalizika mwaka 2025, kwani athari za mpango huo zitatathminiwa mwishoni mwa mwaka wa mwisho, ili awamu ya pili itengenezwe.

Kinachoibua mfadhaiko na kudharau mwamko wa umma kwa jumla nchini Jordan ni kurudia kwa serikali mtawalia mipango hiyo hiyo na miradi ya serikali tangu 1999 kwa kile kinachoitwa maendeleo ya sekta ya umma nchini Jordan, ambayo ilizidi mipango 12 pamoja na taasisi huru mbali mbali! Mipango na mikakati iliwekwa ndani ya droo za serikali zilizopita kwa kufeli kuavywa kwao na serikali mtawalia. Miongoni mwa maafa ya Ummah ni mateso yake kutokana na serikali kama hizi kiasi kwamba Wizara ya Maendeleo ya Sekta ya Umma kuanzishwa mwaka 2006 kwa lengo la kufanyia kazi maendeleo yake. Serikali mwaka 2019 na baada ya zaidi ya miaka kumi na mbili iliiondoa wizara hii, baada ya kuongozwa na mawaziri 21 katika miaka ya nyuma, bila mafanikio yoyote makubwa, lakini badala yake sekta ya umma bado inakabiliwa na ulegevu, usimamizi mbovu, ufanisi mdogo na urasimu unaochukiza katika ngazi ya watu binafsi na makundi ya uwekezaji, na ushahidi bora zaidi wa hili ni mpango huu mpya ambao utachukua miaka kukamilisha awamu yake ya kwanza, ambayo itakamilika 2025, kisha mpango mwengine utakaomalizika baada ya miaka 3 na kisha kumalizika baada ya miaka 10 kufikia sekta ya umma yenye uwezo!

Tafiti, hatua na mipango hii ya kinadharia havijaleta na wala havitaleta uboreshaji wowote katika utendaji wa sekta ya umma isipokuwa kuitoza Hazina ya Serikali mishahara ya mawaziri na wajumbe wa kamati na gharama za kuvunja, kuweka na kupanga upya wizara na taasisi katika katika upande wa majina na dori, kwa sababu yale yanayoitwa mamlaka ya utendaji hayatoki katika chanzo kimoja. Kwa vile serikali zimepewa dhamana ya kusimamia sekta ya umma zinataka kuufurahisha mfumo wa kisiasa wa serikali na uthabiti wake, ili sera yake katika uajiri wa umma iwe na utiifu, sio umahiri, na ushindani katika kufikia maelekezo ya mamlaka ya kifalme wakati wa kuunda serikali. Haihusiki na kufikia au kutofikia mafanikio yoyote katika sekta ya umma itakapokuwa imeondoka,  au kwa fedha zilizotumika na kupotea kwa mawaziri na kamati ambazo hazina maana. Badala yake, inajiringia mbinu zake za ukusanyaji mapato na kodi, na kushindana katika hilo na serikali mtawalia.

Matatizo ambayo umma kwa jumla unakabiliwa nayo kutokana na ulegevu, udhaifu wa kiidara, na hata udanganyifu katika utendaji, umahiri, utata, na kuahirisha mambo katika kuwezesha masilahi ya watu yanaonekana, na yanafanywa upya mara kadhaa, kama vile vifo vya watu wasio na hatia katika ajali za Hospitali ya Salts, Bahari ya Dead Sea na bandari ya Aqaba, pamoja na utata wa huduma za umma kwa watu binafsi katika huduma za afya, elimu, vyuo vikuu, ukosefu wa ajira na kodi kubwa, yote haya hayahitaji mipango ya kuboresha sekta umma, wala kwa mageuzi ya kiidara, bali inahitaji suluhisho msingi na mabadiliko ya kina ya misingi ambayo kwayo maslahi ya watu yanasimamiwa.

Utawala katika Uislamu hauko kupitia baraza la mawaziri (bunge) na mawaziri walio na taaluma, mamlaka na bajeti tofauti kwa kila mmoja kutokana na uhalisia na mamlaka, kama katika mifumo ya serikali ya iliyotungwa na mwanadamu leo. Mtu anaweza kuwa na mamlaka zaidi kuliko wengine, na ziada hiyo haichukuliwi kutoka kwa mmoja hadi mwingine isipokuwa kwa taratibu nyingi ndefu zinazoongeza utata katika kutatua maslahi ya watu; kutokana na mwingiliano wa wizara kadhaa katika kushughulikia maslahi sawa, badala ya maslahi ya watu kuwa ndani ya chombo kimoja cha utawala kinachowaleta pamoja.

Watu wameonja ugumu kutokana na usimamizi mbovu wa mfumo wa sasa. Sera ya usimamizi ambayo juu yake imeegemezwa Dola ya Khilafah ya Kiislamu, ambayo kwayo tunakulinganieni, imefupishwa katika mambo matatu: (usahali katika mfumo, umahiri wa yule anayeifanya kazi hiyo, na kasi ya kukamilisha kazi), na hili lichukuliwa kutoka kwa uhalisia wa kufikia maslahi. Mtu mwenye maslahi hutaka tu kuyapata kwa haraka, na kuyapata kwa ukamilifu zaidi, na Mtume asema:

»إِنَّ اللَّهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ«

…Hakika Mwenyezi Mungu amepitisha ihsan juu ya kila kitu, basi pindi munapouwa uweni kwa njia nzuri, na pindi mnapochinja chinjeni kwa njia nzuri Imesimuliwa na Muslim kutoka kwa Shaddad Bin Aus.

Hili linahitaji kuboreshwa kwa mifumo ya kiidara yenye kuzuia kuvuja kwa kasoro kwenye idara. Hivyo; Lazima kuwe na mfumo wa chombo cha idara, mfumo wa mtindo wa usimamizi, mfumo wa wafanyikazi, na mfumo wa uhusiano wa umma pamoja na usimamizi na wafanyikazi, ili mifumo hii ihakikishe kuwa wafanyikazi wa serikali wanatumikia watu, na kuhakikisha kuwanufaisha watu kwa ujuzi katika vyombo vya idara, bila kujali aina za madhehebu yao, na kuhakikisha uboreshaji wa mtindo wa usimamizi. Inazuia udhalimu wa wakubwa kwa wafanyakazi, pamoja na udhalimu wa wafanyakazi kwa umma, na kuruhusu maslahi kushughulikiwa haraka na kwa juhudi ndogo.

Mtume (saw) alikuwa akisimamia maslahi ya Waislamu na kutatua matatizo yao ya kiidara kwa urahisi, na akawateua baadhi ya Maswahaba kufanya hivyo. Kwa hivyo maslahi ya watu yatakuwa ni chombo ambacho Khalifa atakichukua au kumteua meneja mwenye uwezo wa kukisimamia, na hili ndilo tunalolitabanni, ili kumpunguzia Khalifa mzigo haswa kwa vile maslahi yametapakaa na kuongezeka, kwa hiyo kutakuwa na chombo kwa ajili ya maslahi ya watu chini ya usimamizi wa meneja mwenye uwezo na mbinu na njia zinazowezesha maisha ya raia, na kuwapa huduma muhimu bila matatizo, lakini badala yake kwa urahisi.

Ubainifu wa misingi ambayo juu yake usimamizi wa maslahi na uangalizi wa mambo ya watu umeegemezwa juu ya hukmu za Uislamu ambazo Khalifa anazitabikisha ndani ya dola ya Kiislamu, huufanya usimamizi wa maslahi kuwa ni kielelezo thabiti ambacho hakihitaji kubadilika, bali inahakikisha utulivu na dawama, ambayo haifikiwi na serikali za kisekula ambazo hazitenganiki na malengo ya mfumo wa utawala ulioundwa na mwanadamu na mtazamo wake wa sera ya kigeni ili kuoanisha usimamizi wa sekta ya umma na kuendana na mipango ya kikoloni ya Mfumo wa Fedha wa Kimataifa na kwa maslahi ya dola zenye tamaa, na makubaliano na umbile la Kiyahudi, hivyo mabwawa yanakaushwa ili kuhalalisha ununuzi  wa maji kutoka kwao, au makubaliano ya nia au hata miradi ya reli ili kuunganisha umbile hili na dola za Ghuba na kuifanya Jordan kuwa lango la uwazi ili kuliwezesha kiuchumi.

Mfumo wa utawala katika Uislamu, yaani, Khilafah, ni tofauti na aina za serikali zinazojulikana duniani, iwe ni katika msingi ambao umejengwa juu yake, au katika mawazo, fahamu, viwango na hukmu ambazo kwazo mambo yanashughulikiwa, au katika katiba na sheria yenye kuzitekeleza na kuzitabikisha kitendo, au katika umbo ambalo dola ya Kiislamu inawakilishwa. Ambalo huitofautisha na aina zote za serikali duniani. Dola ya Khilafah kihistoria imeweka mifano bora kabisa katika mtindo wa vyombo vyake vya kiidara na utimizaji maslahi ya raia, ambapo Khalifa huelewa maana ya kuchunga mambo ya watu na kutimiza maslahi yao. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

»مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ، وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ«

Mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atamtawalishia raia, kisha akafa siku ya kufa na ilhali amewahadaa raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu amemuharamishia Pepo.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu