Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 11 Rajab 1445 | Na: 1445 / 10 |
M. Jumanne, 23 Januari 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Bajeti ya Janga ya Kikoloni na Amana za Benki za Dolari Bilioni 60 ni Kizuizi cha Mzunguko wa Kiuchumi na Vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake!
(Imetafsiriwa)
Benki Kuu ilisema kwamba amana za mfumo wa benki zilifikia dinari bilioni 43.292 mwishoni mwa Novemba iliyopita. Amana za benki ziliongezeka kwa 2.8% ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2022, huku idadi inayokadiriwa ya wakopaji kutoka benki za Jordan ikifikia takriban watu milioni 1.2. Deni lililosalia la benki linalohusishwa na watu binafsi lilizidi dolari bilioni 17. Faida za benki zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Amman ilifikia takriban dinari milioni 815.8 (dolari bilioni 1.2) katika miezi sita ya kwanza ya 2023, ikionyesha kiwango cha ukuaji cha 37.1% ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Awali serikali ilikuwa imewasilisha Bungeni bajeti ya 2024, ambayo inaendana na watangulizi wake kwa kutoendana na mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaoathiri nchi mwaka nenda mwaka rudi. Mgogoro huo unadhihirishwa na kuongezeka kwa deni, ukosefu wa ajira, viwango vya riba, na kushuka kwa ukuaji wa uchumi. Bajeti hiyo inategemea mapato ya ushuru, mikopo, na madeni ya riba kusimamia shughuli za kila siku za serikali, huku ikihakikisha utengaji wa fedha kwa taasisi za serikali zinazodumisha usalama na utulivu wa serikali nchini Jordan, kama vile bajeti ya ulinzi iliyozidi dinari bilioni mbili.
Imedhihirika wazi kuwa, utawala wa Jordan na serikali yake tangu kuanzishwa kwake, haujaonyesha kujali sana hali mbaya ya kiuchumi inayozidisha hali ngumu ya maisha na umaskini unaowakabili wananchi wa Jordan. Maadamu wanashikamana na kujiweka sawa na vazi na mipango ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa wa kikoloni wa Kimarekani, na usaidizi unaotolewa na Amerika, ahadi ambazo utawala wa Jordan umeshikilia tangu mwanzoni mwa miaka ya 1950 kwa badali ya utiifu wa kisiasa, kujisalimisha, huduma za kijeshi, ikiwa ni pamoja na uanzishwaji wa kambi za kijeshi na muungano katika kutumikia maslahi ya Marekani. Hii ni pamoja na kutoa msaada wa kijeshi kwa umbile lililo katika vita na Gaza kupitia Mkataba wa Jordan na Marekani wa Ulinzi wa Pamoja na Ushirikiano wa Kiuchumi.
Kulingana na bajeti ya 2024, kuna uwezekano kwamba ongezeko la jumla la deni la umma kwa mwaka wa 2023 litafikia takriban dinari bilioni 2.324. Deni la riba linalotokana na serikali na watu binafsi linaongezeka kiastronomia huku kukiwa na kuzorota na kushuka kwa ukuaji wa uchumi, ikizingatiwa kuwa kuna ukuaji mkubwa wa uchumi na uwekezaji. Jumla ya deni la umma lilifikia dinari bilioni 41.157 mwishoni mwa Oktoba mwaka uliopita, ikiwa ni asilimia 114.2 ya Pato la Taifa (GDP), bila kujumuisha madeni ya ndani na ya kijeshi, ambayo baadhi ya makadirio yanadokeza kuwa yanaweza kuwa maradufu ya deni la umma. Kiasi cha malipo ya deni la umma, yaani riba iliyoharamishwa, kiliongezeka hadi dinari milioni 1703 baada ya tathmini ya mwaka wa 2023. Inatarajiwa kuwa mgao wa malipo ya deni mnamo 2024 utaongezeka kwa dinari milioni 278, na kufikisha jumla ya dinari milioni 1980 (dolari bilioni 2.8), zikiwakilisha zaidi ya 5% ya Pato la Taifa. Asilimia hii inawakilisha riba iliyoharamishwa inayolipwa na serikali, pamoja na kuongezeka kwa kiwango asili cha deni.
Inasikitisha na ni aibu kwamba idadi ya watu katika Ummah (watu milioni 1.2) wanashiriki kujihusisha na ukopaji wa riba ulioharamishwa kutoka kwa benki na taasisi za fedha za riba. Deni la mtu binafsi kwa benki zenye faida kubwa limefikia dinari bilioni 11.8 (dola bilioni 17), huku faida za benki zilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Amman ilifikia takriban dinari milioni 815.8 (dolari bilioni 1.2) katika miezi sita ya kwanza ya 2023. Sehemu kubwa ya faida hizi zinatokana na riba iliyoharamishwa, na ni pamoja na uuzaji wa mali za wale ambao wanang’ang’ana kulipa madeni yao, ikijumuisha sehemu kubwa ya wadaiwa.
Kutokana na fikra dhalimu za kiuchumi za kibepari na kutawala utajiri wa watu walio katika mazingira magumu, hivi karibuni serikali iliunga mkono kile kinachojulikana kama Mfuko wa Mitaji na Uwekezaji wa Jordan. Chini ya hili, mfuko ulitoa ahadi ya mtaji wa dinari milioni 275 (dolari milioni 388). Mfuko huu umeundwa na muungano wa benki 16 za Jordan, zikilenga zaidi sekta ya chakula na kilimo. Zaidi ya hayo, inazingatia uwekezaji katika teknolojia ya elimu, ufungaji, viwanda vya dawa, kujipanga na uboreshaji wa maono ya kiuchumi. Uwekezaji huu wa kibinafsi kimsingi hunufaisha benki zenye faida kubwa, ukizingatia miradi inayolenga watumiaji badala ya ile yenye natija. Inaelezwa kama ubinafsishaji uliopachikwa wa miradi kwa manufaa ya umma, ambapo, kwa mfano, inadaiwa kuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (yaani, pesa za watu) haujumuishwi.
Licha ya utasa wa mfumo wa uchumi wa kibepari na dhuluma na ukandamizaji wake, na kuwaondolea watu kanuni za msingi zaidi za mgawanyo wa mali, tunaona kwamba mfumo huu, wakati huo huo, unautumia kuzidisha ufisadi wa kiuchumi na kuzidisha mzozo wa kiuchumi nchini Jordan kwa manufaa ya kipote cha watawala wafisadi. Haya yanajiri kwa ushirikiano wa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, Benki ya Dunia, na misaada ya Marekani, zote zikichangia ushawishi na udhibiti.
Matatizo ya kiuchumi ya Jordan na nchi zote za Kiislamu kimsingi ni masuala ya kisiasa, yanayofungamana na utegemezi wa dola zinazogombana za kikoloni zinazogombania ushawishi na rasilimali katika nchi zetu, hasa miongoni mwao ni Marekani na Uingereza. Dola hizi za kikoloni zinapeana majukumu kwa serikali zinazotawala ili kufikia maslahi yao ya kikoloni, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa na usalama wa umbile la Kiyahudi, pamoja na ushirikiano wake wa kiuchumi katika miradi ya kiuchumi ya ndani na ya kieneo. Kusitasita na kufeli kwa utawala huu kuwanusuru watu wa Gaza kwa kupeleka vikosi vyake kupigana dhidi ya Mayahudi, na badala yake, kujihusisha kwake katika mradi wa Marekani na Ulaya wa kutatua kadhia ya Palestina—hauwezekani tena, kwa mujibu wa madai yake, chini ya suluhisho la dola mbili – na uimarishaji wa misingi ya umbile la Kiyahudi, yote ni sehemu ya gharama inayolipwa na serikali katika kutafuta miradi fisidifu ya kiuchumi, deni kubwa na migogoro isiyoweza kuepukika.
Mfumo wa riba za benki ndio mzizi wa maafa katika uchumi wa kibepari, kuruhusu benki kukusanya pesa za watu kwa jina la amana na kuziweka kwenye mifuko ya matajiri na wafanyibiashara. Hii imepelekea kulimbikiza mali za watu mikononi mwa watu wachache. Mfumo wa mikopo yenye riba ni tatizo kubwa la kiuchumi, hasa ikizingatiwa kuwa Uislamu unaharamisha riba kwa serikali na watu binafsi. Kwa hiyo, tunatoa wito kwa vijana na mabinti wa Ummah wanaojihusisha na riba kuacha mara moja miamala hiyo na kushikamana na hukmu za kisheria, kwani hili liko ndani ya uwezo wenu.
Mnaombaje msaada wa Mwenyezi Mungu kwa watu wa Gaza wakati huo huo mkitangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kujishughulisha na mikopo yenye riba inayonufaisha benki za kibepari pekee?! Amana wanazoweka watu katika mabenki na mikopo ya riba, kwa msingi wa riba, ni sawa na tangazo la vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:
[فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللهِ وَرَسُولِهِ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ]
“Basi mkitofanya jitangazieni vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe.” [Al-Baqara:279].
Isitoshe, ni sehemu ya mfumo fisadi wa kibepari, unaogeuza mali kuwa chombo cha utawala miongoni mwa matajiri, badala ya kuitumia kwa miradi inayochochea uchumi. Hii ni licha ya vizuizi vilivyowekwa na serikali dhalimu kwa uwekezaji, kama vile kodi, ada na faini.
Kutegemea rasilimali zake yenyewe, kama inavyofafanuliwa na Sharia, katika bajeti yake kwa mapato na matumizi, na kukataa misaada ya kimataifa na mikopo kutoka kwa benki za riba, huwezesha serikali kuwa na udhibiti wa maamuzi yake ya kisiasa. Kwa hiyo, inaweza kutumia fedha katika miradi yenye natija inayoingiza mapato ya kutosha kukidhi mahitaji ya wananchi wake. Mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unaweza tu kuleta matunda yake kwa kuutabikisha ndani ya dola ya Khilafah, ambayo hivi sasa inaadhimisha miaka mia moja na tatu tangu kuvunjwa kwake masiku haya.
Hivyo basi, tunatoa wito kwa Waislamu kufanya kazi katika kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, yenye lengo la kumaliza umaskini, njaa, ukosefu wa ajira, na unyonyaji wa rasilimali zenu. Tunatoa wito kwenu, enyi Waislamu.
[وَمَنْ يَتَّقِ اللهَ يَجْعَلْ لَهُ مَخْرَجاً * وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللهِ فَهُوَ حَسْبُهُ]
“Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha.” [At-Talaq:2-3].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |