Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 4 Sha'aban 1445 | Na: 1445 / 12 |
M. Jumatano, 14 Februari 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kisimamo cha Familia za Mashababu Wanaozuiliwa wa Hizb ut Tahrir mbele ya Bunge la Wawakilishi
(Imetafsiriwa)
Familia za Mashababu wa Hizb ut Tahrir nchini Jordan, wanaozuiliwa na Mahakama ya Usalama ya Serikali, walifanya walilaani mbele ya Bunge la Wawakilishi, asubuhi ya leo, Jumatano 14/02/2024, ambapo waliitaka Afisi ya Mkuu wa Bunge la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhuru wa Umma na Haki za Kibinadamu kufanya kazi na kuwasiliana na wale wanaohusika kwa ajili ya kuachiliwa huru mara moja kwa watoto wao waliowekwa kizuizini kwa sababu ya kutoa maoni yao ambapo hawakufanya kitendo chochote cha kigaidi, au uhalifu wowote kwa sheria za usalama wa serikali. Walihamishiwa katika mahakama ya usalama ya serikali kwa mashtaka ya kutekeleza kitendo cha kimakusudi ambacho kingehatarisha usalama wa jamii, kwa kukiuka vifungu vya Sheria ya Kuzuia Ugaidi!
Kukamatwa kwao kulitokea baada ya kusambaza toleo kutoka Hizb baada ya Swala ya Ijumaa mnamo Novemba 10, 2023, likitoa wito wa kuwanusuru watu wa Gaza na kuwahutubia watu wenye nguvu na majeshi kwa kusema: “Enyi Askari katika Majeshi ya Kiislamu.
[أَلَيْسَ مِنْكُمْ رَجُلٌ رَشِيدٌ]
“Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka?” [Hud 11:78]. Ndani yake, liliwaambia askari katika majeshi ya Kiislamu, likisema: “Je, damu ya ndugu zenu na dada zenu inayomwagwa huko Gaza Hashem haikuathirini? Je, kilio cha watoto, na maombi ya wanawake, na wazee hayakusukumini kuwapa nusrah (msaada)?” Kama ilivyoelezwa katika toleo la Hizb ut Tahrir: “Umbile la Kiyahudi sio watu wa vita au wapiganaji. Ni waoga na wadhalilifu na mafukara. Mnashuhudia vijana Waumini wa safu zenu wakiwa na silaha zisizolingana na za Mayahudi, lakini wanawashambulia kwa nguvu."
Ujumbe wa familia za wafungwa uliikabidhi Sekretarieti Kuu ya Baraza barua iliyotumwa kwa Afisi ya Mkuu wa Bunge la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Kamati ya Baraza la Uhuru wa Umma. Yafuatayo ni maandishi ya barua hiyo:
بسم الله الرحمن الرحيم))
الحمد لله رب العالمين، والصلاة والسلام على سيدنا محمد وعلى آله وصحبه أجمعين...
- Mstahiki Muheshimiwa Spika wa Bunge la Wawakilishi
- Mstahiki Muheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uhuru wa Umma na Haki za Kibinadamu.
Baada ya salamu na heshima:
Sisi ni kundi la familia za wafungwa wa uhuru wa maoni. Vyombo vya usalama viliwakamata watoto wetu Ijumaa iliyopita, tarehe kumi Novemba 2023, baada ya kuwataka wayataharaki majeshi kunusuru watu wetu huko Gaza Hashem, baada ya kuona kwa macho yetu ukubwa wa mauaji na uharibifu mikononi mwa watoto waovu wa Wazayuni na kwa ushirikiano wa dola zote za ukafiri zinazoongozwa na Marekani, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa.
Na nyinyi hapa munashuhudia kwa macho yenu, zaidi ya miezi minne baada ya uvamizi huu wa kikatili, uthabiti mkubwa wa watu wetu, kimya cha kimataifa, wito na maazimio ya kutaka kusitishwa kwa uvamizi na kuanzishwa kwa misaada, huku adui akiendesha hadaa na uhalifu wake, na mamia ya watu wetu wanauawa na kuhamishwa kila siku... Wengi wa watu wa nchi hii nzuri wamekinai kwamba hakuna njia ya kukomesha uhalifu huu dhidi ya watu wetu huko Gaza Hashem, isipokuwa kwa nguvu, kusonga majeshi, au hata kwa kutishia kuyapeleka majeshi.
Basi liko wapi kosa la jinai katika ombi hili na maoni haya sahihi ambayo watoto wetu wameyataka ambayo yalihitaji kukamatwa kwao, na hata kuwatia nguvuni na kuwawekwa kizuizini mbele ya Mahakama ya Usalama ya Serikali kana kwamba ni magaidi?!
Kwa hiyo, tunakuomba Mheshimiwa uitishe kuachiliwa huru watoto wetu ambao wamezuiliwa kwa zaidi ya miezi mitatu, kwa kuwa uhuru kati nchi hii umedhaminiwa na Katiba ya Jordan, na uhuru wa maoni na kuzungumza ni haki ya kiasili iliyo ndani ya Katiba.
Mnamo tarehe 14 Februari 2024
• Tunaambatisha hapa majina ya watoto wetu wanaozuiliwa:
1- Murad Shaher Jadem Shumailat |
7- Suhaib Yassin Saad Al Jaber |
2- Muhammad Yahya Mansour Al-Rai |
8- Bilal Muhammad Saleh Badran |
3- Ali Theeb Ahmed Majdalawi |
9- Ziad Salim Muhammad Abu Rizk |
4- Moaz Abdullah Muhammad Marzouqa |
10- Faisal Ghazi Mahyar |
5- Ahmed Khalil Salim Bakr |
11- Ali Suleiman Khalil Khalil) |
6- Malek Ayoub Muhammad Al-Fakhouri |
Mwisho wa barua …
Sisi, katika Hizb ut Tahrir tunathibitisha kwamba serikali hii haina udhuru wa kuwakamata vijana hawa kutoka Hizb ut Tahrir ambao ni wachamungu na wanaoilinda dini yao. Tunawahesabu kuwa hivyo na hatuwasifu yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Yote waliyoyafanya ni yale ambayo Dini yao ya Kiislamu imeamuru kwa kuyataka majeshi yawanusuru watu wanaodhulumiwa wa Gaza kwa kutii maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
“Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia” [Al-Anfal 8:72]. Vita dhidi ya Gaza vimeingia mwezi wa tano, kwa hiyo je kitendo hiki kinahitaji kukamatwa na kufunguliwa mashtaka katika mahakama ya serikali?! Au je, wito wa kutaka utabikishwaji wa hukmu za Uislamu ni tofauti na mkabala wa utawala katika kukaa kimya kuhusu jinai za umbile la Kiyahudi na kuiunga mkono Marekani, ambao wote wawili ni maadui. Kutojali ukweli kwamba watu wa Jordan wamesimama na ndugu zao huko Gaza na kuelezea kuridhishwa kwao na kile Mujahidina walichokifanya mnamo Oktoba 7, 2023, ni kinyume na inachodai Ikulu ya White House?
Tunasimama imara na familia za wanachama wanaozuiliwa katika Mashababu wetu na tunazitaka huduma za usalama kuwaachilia huru mara moja Mashababu wanaozuiliwa wa Hizb ut Tahrir. Tunasisitiza barua ya familia za vijana wetu kwa Bunge la Wawakilishi kufanya kazi kwa bidii ili kukomesha tuhma za mahakama ya usalama ya serikali na kuwaachilia huru, kwani ni mashtaka ya uwongo na ya dhulma dhidi ya wabebaji ulinganizi hao.
[وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ]
“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.” [Ash-Shu’ara 26:227]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |