Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  26 Rajab 1444 Na: 1444/06 H
M.  Ijumaa, 17 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Kenya Yaandaa Maandamano Baridi kwenye Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuanguka kwa Khilafah

(Imetafsiriwa)

Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 102 tokea kuvunjwa kwa Khilafah, Hizb ut-Tahrir Kenya iliweza kuandaa maandamano baridi baada ya swala za Ijumaa mnamo tarehe 17 Februari 2023 M sambamba na tarehe 26 Rajab 1444 H.

Maandamano haya yalikusudiwa kukumbusha Umma hali tete inayoendelea kukumbana nayo tokea kuangushwa kwa Khilafah tarehe 28 Rajab 1342 H, sawa na tarehe 3 Machi,1924. Tokea tukio hili la kuhuzunisha, umma wa Kiislamu umegawanywa kupitia mradi wa kikoloni wa Sykes-Picot uliopelekea pia ardhi zao kukaliwa kimabavu na kutawaliwa na ukoloni. Damu za Waislamu zikimwagwa huko Syria, Yemen na China bali katika nchi zote za Kiislamu, hali inayoonesha kiwango kikubwa cha maumivu umma unayopitia. Mtetemeko wa ardhi hivi karibuni huko Uturuki, ardhi ambayo Khalifah wa mwisho alifukuzwa kufuatia mkataba wa khiyana wa Lausanne umeonesha kiwango cha juu cha utepetevu cha serikali za ulimwengu wa Kiislamu. Leo kwa hakika walimwengu wote wanakumbwa na hali ngumu ya kiuchumi, uongozi fisidifu na maovo ya kijamii kama natija ya kuvunjwa kwa Khilafah.

Huku idadi ya Waislamu ikikurubia bilioni 2, lakini idadi hii imekuwa mithili ya povu la bahari kwa kutoweka kwa Khilafah mlinzi na ngao ya Waislamu. Umma wa Kiislamu umekosa heshima, utukufu na mlinzi. Umepoteza kibla chake cha kwanza katika biladi tukufu ya Isra wal Miiraj. Na ni kwa kupitia Khilafah pekee ndio kibla hiki pamoja na biladi zilizokaliwa na Wamagharibi zitarudishwa mikononi mwa Waislamu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atusimamishie kwa haraka Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, Naye Mwenyezi Mungu ni Muweza wa jambo lake lakini watu wengu hawajui.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb utTahrir

Kenya

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu