Ijumaa, 17 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  27 Sha'aban 1444 Na: 1444/08 H
M.  Jumapili, 19 Machi 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Kenya

Wakutana na Wanazuoni Mashuhuri wa Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Kenya ukiongozwa na Ustadh Mahd Ali - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir nchini Kenya akifuatana na Ustadh Yusuf Ghasani na Ali Mwangi ambao wote ni wanachama wa Hizb ut Tahrir, walikutana na viongozi kadhaa mashuhuri wa Kiislamu walioko Mji Mkuu wa Kenya Nairobi miongoni mwao:

Naibu Kadhi Mkuu wa Kenya Sheikh Sukyan Hassan Omar

Sheikh Juma Amir Imam Msaidizi wa Msikiti wa Jamia, Nairobi

Daktari Mbarak Ahmed Awes Imam Msikiti wa Al-Hudaa South B Nairobi

Ujumbe huo wa Hizb ulipokelewa kwa mapokezi mazuri. Mkuu wa ujumbe huo, Ustadh Mahd Ali aliweza kushiriki majadiliano yenye maana na viongozi hao kuhusu LGBT na Da’wah ya Kiislamu kwa jumla. Aliwapa nakala ya kitabu, Khilafah, chapisho la Hizb ut Tahrir kinachoelezea ufaradhi juu ya Waislamu wa kusimamisha tena Khilafah.

Twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu azifungue nyoyo za Maulamaa wafanye kazi na Hizb ut Tahrir katika kufikia lengo la kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume.

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu